Iko hivi kwa tathmini yangu,tatizo linaanzia kwa maafisa elimu kata.
Wao inapofika January wanatakiwa wafanye yafuatayo
1.afisa elimu kata aangalie Ana shule ngapi za msingi zenye darasa la Saba wangapi,kwa mfano Ana shule 7 za msingi Kila shule Ina wanafunzi wa darasa la Saba 60 ,maana yake 60*7 sawa na wanafunzi 420 wa standard seven, Hawa unaweka asilimia tisini watafaulu,maana yake 400 wataenda sekondari.
Unaangalia shule zako za sekondari hapo katani ni ngapi kwa mfano ziko 3,sawa,Kila shule Ina uwezo wa kuchukua form one wangapi? Mfano uwezo ni 300 wanafunzi,kwa hiyo 100 hawatakua na nafasi wakifaulu,unalipeleka, kwenye kikao Cha maendeleo ya kata na kwa afisa elimu na mkurugenzi umemaliza.