gallow bird
JF-Expert Member
- Aug 10, 2024
- 14,889
- 18,593
Kwamba John alikua na akili mno!!.. taratibu bro!!.. sijaona dalili za akili kwa lissu,labda unipe definition yako ya akiliCongratulations, you have escaped the matrix of intellectual lobotomy.
Kuna mtu aliwahi kusema humu ndani kwamba Tundu Lissu is an upgrade of John Pombe Magufuli with bugs fixed. Alikuwa sahihi mno. Lissu kama John, wote ni watu wenye akili nyingi mno (Highly Intelligent), wana tatizo la sifa (Egotistical), wote hawawezi kutawala hisia zao (Lack of Emotional Stamina), waropokaji (Loose lips) na hawana uwezo wa kupembua nyakati (Lack of discernment). Sina shaka na uzalendo wao hata chembe, wala utendaji kazi wao.
Tatizo ni kwamba kuwa kiongozi mzuri inahitaji zaidi ya kuwa BOOK-SMART. Inahitaji mtu uwe unaweza kusoma alama, nyakati na majira. Ni lazima ujifunze mambo ya msingi kuhusu utawala (State-Craft), kama ifuatavyo:
Mosi, kuna vita nyingine unashinda kwa kushindwa.
Pili, kunyamaza kimya saa nyingine siyo udhaifu bali ni busara na mkakati-vita.
Tatu, Vita zote kubwa duniani huwa zinapiganwa kwenye gizani kusipoonekana.
Ndiyo maana hata unapomfundisha mtoto kucheza CHESS ni lazima umwambie kwamba kuna sehemu lazima akubali PAWNS waliwe ili KING au KNIGHT aweza kuzunguka vizuri kwenye ubao. Ukishafahamu kwamba dunia hii inatawaliwa na watu waovu basi ni lazima utahitaji kuwa mtawala wa aina yake. KARATA ZOTE HAZIWEKWI JUU. Tanzanians are also not ready for this conversation.
So wali-recruit toka 'vyuo vikuu' vya nje?, palikua na wanafunzi wa kutosha watz huko vyuo vikuu vya nje kiasi cha kuweza kujaza nafasi baada ya 'safisha safisha' idarani?Nani kakwambia kwamba kila Mtanzania alisoma chuo hapa nchini ???
PoleniTaifa limeshapotea
So wali-recruit toka 'vyuo vikuu' vya nje?, palikua na wanafunzi wa kutosha watz huko vyuo vikuu vya nje kiasi cha kuweza kujaza nafasi baada ya 'safisha safisha' idarani?
So tunapaswa kuwa tumetumikia jeshi kama commissioned officers Ili tuelewe uzi wako?..Umewahi kutumikia jeshi kama Commissioned Officer ???
Bila kuwa Commissioned Officer hata nikikupa mifano lukuki huwezi kuelewa.
Umeandika vizuri sana lakini unasisitiza sheria na kanuni tuzifuate. Je, kwa unavyoona muelekeo wa nchi na viongozi tulionao kweli kuna sheria zitafuatwa??
Hebu weka solution ya kudumu ambayo itasaidia hao watu wafate kanuni ili hata siku chama chochote au mtu yeyote akikabidhiwa funguo za ikulu asiende kinyume na sheria na kanuni..!!
So tunapaswa kuwa tumetumikia jeshi kama commissioned officers Ili tuelewe uzi wako?..
BOOKMARK THIS: Ndugu Humphrey Polepole na Ndugu Tundu Lissu hawapikiki chungu kimoja. Kuanzia KIFIKRA, KIITIKADI na KIMALENGO. Atakapotoka nje, Tundu Lissu ambaye anataka kuitoa CCM madarakani ndiyo tutafahamu kwamba kweli Ndugu Polepole anataka nini.
Mpaka sasa nitaendelea kumsikiliza, maana baadhi ya mambo anayoyasema yana ukweli nusu-nusu. MOST OF YOU ARE NOT READY FOR THIS DEBATE.
Mimi huko sipo,tulipoanzia ni ulipodai 1975 ilifanyika safisha safisha idarani na wakaanza ku-recruit vyuo vikuu, tanzania 1975 ilikua na chuo kikuu kimoja tu,hivyo vingi unavyovitaja vikitoka wapi?NDIYO, kwasababu huu uzi ni barua maamulum kwa wahusika.
Nikuulize tu sasa, KAR ilivyovunjwa mwaka 1964 Kambona na Nyerere walifanyaje ?
Mimi huko sipo,tulipoanzia ni ulipodai 1975 ilifanyika safisha safisha idarani na wakaanza ku-recruit vyuo vikuu, tanzania 1975 ilikua na chuo kikuu kimoja tu,hivyo vingi unavyovitaja vikitoka wapi?
Hili nimelitaja huko nyuma,kama ni kusoma chuo kikuu tofauti na UD basi ni nje ya nchi, palikua na watz wangapi nje ya nchi wakisoma vyuo vikuu kiasi cha kujaza nafasi idarani baada ya timua timua?..vyuo vingine kama cbe cha 1965 hakikua chuo kikuu,sua imeanza 1984Kwani kila msomi wa nchi hii ya Tanzania alisoma UDSM ???
Hili nimelitaja huko nyuma,kama ni kusoma chuo kikuu tofauti na UD basi ni nje ya nchi, palikua na watz wangapi nje ya nchi wakisoma vyuo vikuu kiasi cha kujaza nafasi idarani baada ya timua timua?..vyuo vingine kama cbe cha 1965 hakikua chuo kikuu,sua imeanza 1984
Kitu ambachoo na kuguarantee na mm sio Nabii, siku Samia akikabidhi nchi kwa mtu mwengne basi makazi yake anaamishia kwenye nchi za Kiarabu kwa msingi anaenda kupumzika ila kiukwel ni atakuwa anaenda kuangalia upepo utakavyokuwa ikiwa nchi ikitaka kufukua uchafu uliofanyika kipindi chake.Dawa ya kutovunja katiba ni ndogo sana.
Kuondoa kinga ya kushtakiwa kwa Viongozi wote wa Kisiasa na kuweka makosa ya kukiuka katiba kuwa makosa ya Jinai.
Alafu vyeo vyote vikuu vya kiutendaji unaviwekea ulinzi wa Kikatiba. Wanateuliwa ila hawawezi kutenguliwa.
Mbona simple sana
Nyerere alifanya kosa gani?Nakubaliana na wewe kwamba WATANGANYIKA inabidi TUUNGANE.
Kila mtu asimame kutetea nchi katika nafasi yake. Nathamini sana mchango wa Humphrey Polepole, nathamini sana mchango wa Maria Sarungi, nathamini sana mchango wa Mange Kimambi, nathamini sana mchango wa Evarist Chahali na nathamini michango ya watu mbalimbali mitandoani na kwenye vyama vya siasa.
Jambo moja tu ambalo sitalichanganya ni lile la kuamini kwasababu anazungumza kichagga basi ni lazima huyu atakuwa ni Mchagga. Tuna kasumba mbili kubwa kwenye siasa zetu. Mosi, kuamini kwamba kila anayezungumza lugha sawa na sisi au kufanana na sisi basi ni mwezetu. Hili lilimgharimu sana Mzee Nyerere hata kwenye diplomasia ya nchi. Hili limebaki hadi kwetu, WATANGANYIKA tunaamini kwamba kila mtu anawaza mema kama sisi na ana moyo mkunjufu kama sisi.
Huwa yanatukuta tukiwa tumeshachelewa mno, ndiyo tunazinduka usingizini kwamba kumbe huyu hakuwa mwenzetu.
Pili, ni kutopenda kuwajibika kisiasa hata pale ambapo ni dhahiri tumefanya makosa makubwa yanayoonekana. Tunakarisika kabisa tukiambiwa ukweli. Ndiyo maana hadi leo hii Mzee Nyerere alifanya makosa na wengi hatupendi kuyaanisha hayo makosa ili tujifunze, tunaishia kujificha kwenye kivuli cha NIA NJEMA. AU kisipokuwa hicho tutasema ni hujuma za MABEBERU. Nothing is ever our fault. Sasa huu utamaduni wa kutopenda KUWAJIBIKA usipojengwa hapa nchini, tutakuwa na hali mbaya hata kama wapinzani watachukua nchi.
Sasa basi mimi naungana na wote wanaosema ukweli. Lakini sitajiingiza kwenye dhambi ya kuamini kwamba wote wanaipenda TANGANYIKA wala kuiwazia mema. Umri nilio nao unatosha kunifundisha mengi kuhusu siasa za Tanzania.
Kuna mambo muhimu ya kuzingatia katika kujadili hizi hoja;UTANGULIZI:
Habari ndugu MTANGANYIKA, leo ni mambo mengi kweli ya kusema ambayo yanatatiza sana moyo wangu. Nimejaribu kuandika wiki kadhaa lakini naishia kufuta kila nikimaliza kuyaaandika. Mengine nikiyasema hadharani yanaweza kuwaumiza sana moyo na mkaishia kukata tu, tamaa. Ila itoshe kusema kwamba TANGANYIKA ISHAUZWA.
1.TANGANYIKA KUTETEWA NA WANAHARAKATI WALIOWAHI KUTUHUJUMU:
Ndugu Humphrey Polepole na pamoja na wanaharakati wengine wa mtandaoni kama Mange Kimambi na Maria Sarungi, watu ambao kwa nyakati tofauti waliwahi kuwa wanufaika wa mfumo na hata kutumika kuhujumu wananchi. Mtu pekee ambaye amekuwa akisema ukweli siku zote ni kaka yangu Evarist Chahali (He has been very Consistent and Objective).
Miundombinu mingi ambayo Samia anaitumia kututesa WATANGANYIKA, ilitengenezwa na Raisi John Pombe Magufuli. Humphrey Polepole na Dr.Bashiru Ali Kakurwa walikuwa ni wahandisi wakuu wa kisera. Ilifika kipindi hadi Dr. Bashiru alitamka wazi kwamba CCM inaweza kuvunja katiba ili kubaki madarakani kwasababu ndiyo imeshika dola.
Hawa wengine kama Maria Sarungi, na Mange Kimambi tunafahamu kwamba madai mengi yalianza kama maslahi binafsi. Hasahasa Binti Sarungi ugomvi wake mkubwa na JPM chanzo ni mambo ya kifamilia ambapo yeye kama munfaika wa mfumo alikutwa na SHOCK-THERAPY ya JPM. Alikuwa na mwenzake Fatma Binti Karume, ambaye mlimbatiza jina na kumwita Shangazi, lakini awamu hii rangi zake naye mshaziona.
Mange Kimambi, ni mamluki. Alishawahi kuwa upande wa CCM, baadaye dhidi ya Lowassa, baadaye upande wa Lowassa dhidi ya Magufuli. Baadaye kushangilia msimba wa Magufuli na kumnadi Samia, na saa hizi yuko dhidi ya Samia. WATANGANYIKA hatufahamu kesho atakuwa dhidi ya nani.
Hii dhambi naona inatafuna wengi mno hadi maafisa usalama ambao binafsi nawafahamu waliwahi kuwa mstari wa mbele kutetea kila ujinga unaofanywa na dola, ambapo mamia ya WATANGANYIKA walipoteza uhai, kuumizwa, kufungwa au kufilisiwa. Hata humu JF wengi nawafahamu, naona kabisa mwelekeo wao ni watu aliyepagawa na pepo au kapata wazimu.
WATANGANYIKA, ili kuepukana na kadhia hii ya kubebwa na kila aina ya upepo wa kimaslahi wa watu ni lazima WASOMI wajifunze kusimamia kitu kinachoitwa KANUNI (Principles). Hata pale ambapo mwanasiasa unayempenda anakosea, wewe inabidi uufunde moyo wako kusimamia KANUNI.
RAI YANGU KWA WATANGANYIKA, hasa WANAUSALAMA: Kwenye BIBLIA, Daudi alikuwa ni mtenda dhambi mkubwa kama sisi tu, lakini tunaambiwa ni moja kati ya watu walipata kibali kikubwa sana kwa MUNGU. MUNGU alisema wazi kabisa kwamba anampenda Daudi kwasababu MOYO WAKE HAUNA HILA. Daudi alikuwa ni mtu mwenye kusimamia KANUNI.
Mfalme Sauli alikuwa anamuwinda amuue Daudi. Mara mbili Daudi alipata nafasi ya kumuua kabisa Sauli, kwa mambo aliyomtendea lakini Daudi alisimamia KANUNI. Alikataa kumuua na kusema HUYU NI MPAKWA MAFUTA WA MUNGU, atamalizana na MUNGU wake.
Daudi alikuwa ni KIONGOZI MKARIMU (Equittable). Kuna sehemu kwenye BIBLIA ilitokea vita, na baadhi ya askari wake walichoka wakashindwa kwenda vitani. Waliporudi na kupata ushindi mkubwa na mali nyingi, kuna baadhi ya askari wakasema hawa ambao hawakwenda na sisi vitani wasipewe chochote kile. Daudi aliwakemea na kusema aliyekwenda vitani, na aliyebaki kulinda mji wote watapata mali sawa. Akimaanisha kwamba kila mtu ana umuhimu ndani ya jamii.
Daudi alikuwa ni KIONGOZI MUUNGWA. Alikosea mno kwa kuiba mke wa mtu na kumpa mimba, huku akimuua mume wake. Baadaye alipofutwa na nabii Nathani kuambiwa ukweli, wala hakutafuta vijisababu, bali alikuwa mpole na kwenda kuomba msamaha mbele ya taifa zima. Hakusema kwamba yeye alikuwa na nia njema, ila alisema wazi kwamba amekosea.
SASA BASI: wale ambao mliwahi kuwakosea WATANGANYIKA, na kusababisha vifo, misiba, umasikinui na majeraha ombeni TOBA KWA MUNGU, OMBENI TOBA KWA WATANGANYIKA, lakini kubwa zaidi TOBA YA KWELI huambatana na mabadiliko ya moyo. Jaribuni kukaa kwenye viatu vya watu kama Wazazi wa Ben Saanane, Familia ya Gwanda, Familia ya Soka, Familia ya Akwilina na wengine kisha mtafahamu kwamba WENGI HAMKUISHI VIAPO VYENU.