Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Mkuu hapo labda tuwaombe uhamiaji washikilie nyaraka zake za kusafiria just in case🤣🤣🤣
 
Ambacho hujui ni kwamba mgombea mwenza wa urais wa ccm huteuliwa na wana CCM wenzake sio mgombea urais, hivyo Jpm hakuwa na namna yoyote ya kumkataa Samia
Pia kwa mujibu wa katiba rais hana mamlaka ya kumfuta kazi makamu wake wa rais, hata kama ingekuwa hivo hilo haliwezi fanyika ngazi ya familia labda usalama wa taifa, jeshi au chama
 
Unaifahamu The Commonwealth Capacity Building Programme ???

Watanganyika/Watanzania wangapi walisomeshwa duniani kote kupitia hii ???
​
Over a long period of time ndiyo utapata idadi kubwa ya watu wa kutosha kujaza nafasi za idara,nakumbuka kwenda kusoma nje ilikua kama kwenda peponi,hapo UD mpaka 2003 ilikua ikidahili watu elfu nne kwa mwaka,dai lako la timua timua idarani na kujaza wasomi wa vyuo vikuu si la kweli,mpaka 1990s idara ilikua na watumishi majority wasio na shahada ya chuo kikuu
 
Mkuu MALCOM LUMUMBA
Ni bahati mbaya sana hukumwelewa Lissu kwa ile akili yake kubwa alipokuwa analiongelea lile suala kama ambavyo baadhi humu hawakuelewi kwa hoja zako ambazo wengi tumekubaliana nazo.

Twende taratibu.

Wewe leo una amini kila kitu kilichosemwa kwenye ripoti za Prof Osorro na Mruma kilikuwa sahihi? Zile figures za madini na kodi zilikuwa sahihi? Hakukuwa na kupandisha makisio?

Twende kuhusu MIGA na ICSD. Tuseme hukuelewa hoja kuu ya Lissu ilikuwa kwa njia tunayoenda tutashtakiwa na kujikuta tunalipa gharama kubwa?

Labda nikuulize maana najua unajua. Vipi Acasia walitulipa tulichosema tunawadai? Kama hawakutulipa kwa nini tulikubali kulipwa kidogo? Hicho kidogo tumelipwa? Wanatulipa? Wanatulipaje?

Vipi kuhusu kufuta retension licence? Hatukushtakiwa? Hatushtakiwi? Mpaka leo Serikali imelipa kiasi gani kutokana na makesi mbalimbali tuliyofunguliwa?

Lissu sio mropokaji. Lissu ni mshauri mzuri wa kisheria. Na kama unamsikiliza vizuri Lissu huwa anatoa ushauri mzuri sana. Alimshauri Magufuli vizuri kuhusu njia ya kufuata badala ya kwenda kuzuia makinikia. Na ukweli unaujua. Serikali ilikuja kugundua imekosea steps za kuchukua ikawalazimu kuja kuwashtaki kina Mwanyika ili ku justify tuhuma walizokuwa wanawashutumu Acasia. I Know you know kesi ya kina Mwanyika ilikuwa AFTERTHOUGHT baada ya kuona hawana basis ya kwenda na Acasia kwenye International tribunals.

Tukija kuhusu Muungano. Wewe unaona hoja za Lissu kuhusu Zanzibar hazikuwa sahihi? Umewahi hudhuria vikao kuhusu kero za Muungano? Unajua mijadala inayojadiliwaga kuhusu nafasi ya Zanzibar?

Maneno ya Lissu kuhusu Muungano hasa Zanzibar kuona kuonewa na Tanganyika hayajawahi kuwa uongo. Kwa miaka mingi Zanzibar imekuwa ikikopa kwa kuweka dhamana mali na mitaji ya bara.

Najua pia unajua kuna kesi Ameshtakiwa Serikali ya Zanzibar kwenye masuala ya Uwekezaji ila Serikali ya Muungano tumejumuishwa kwa sababu ya kuhusishwa kulipia kiasi wanachodaiwa Zanzibar.
 
Kwamba lissu akili kubwa,mnapimaje hizi akili..
Nadhani acacia haipo duniani, update your infos
 
Nashukuru sana, wewe umeelewa nilichokizungumza hapa.

Siku zote nimekuwa nikiwaambia WATANGANYIKA kuhusu haya matatizo ya kimfumo yaliyoachwa na Mzee Nyerere lakini wamegoma kunielewa. Haya sasa naomba niongee kitaalamu katika hili kwa kumtumia msomi wa Kijerumani, Professor Max Webber ambaye aliandika kuhusu aina tatu kuu za utawala (Three Types of Administration) kwenye jamii zetu za kileo (Contemporary Society).

Webber kwenye nadharia yake ya utawala (Theory of Legitimate Domination) anasema hivi kuhusu tawala:

1. TRADITIONAL LEADERSHIP STYLE
Hizi ndiyo zile za zamani ambazo msingi wake mara nyingi hutokana na tamadunia za muda mrefu za jamii husika. Hapa uhalali (Legitimacy) ya kiongozi hutegemea miiko ya kiutamaduni na imani za jamii ambayo aniongoza. Mtu anazaliwa kuwa kiongozi hata kama hana sifa, anapewa uongozi. Mfano. Ufalme (Monarchies) na Uchifu (Chieftain).

UDHAIFU: Kwenye aina hii ya utawala sheria zinakuwa hazijaandikwa, bali watu wanazaliwa wamezikuta tu zimetengenezwa na watu hulazimishwa kuzifuata hata kama hawataki. Hakuna haki ya kuuliza-uliza kiongozi wako kwanini anatawala au kwanini hatumpigii kura. Yeye atakutawala hata usipomtaka.

2. CHARISMATIC LEADERSHIP
Aina hii ya uongozi ni ile inatokana na sifa na uwezo binafsi wa kiongozi ambao unampa uwezo wa kukusanya wafuasi ambao huamini kabisa huyu ndiyo mtu anayewafaa. Watu kama hawa mara nyingi huamini kwamba wana uwezo au nguvu ya ziada kutoka kwa MUNGU, kuliko watu wengine. Kiukweli kwenye aina hii ya uongozi, mtawala huwa na vigezo vizito siyo mchezo.

Watu mfano wa Muhammad S.A.W, Gandhi, Hitler, Napoleon, Stalin, Lenin, Nyerere, Nkhrumah na wengine. Watu hawa Uhalali (Legitimacy) yao ya kutawala inatokana na matendo yao wanayowafanyia watu wao, hivyo matendo yakipungua uhalali wao nao unakwisha.

UDHAIFU: Ni kwamba mara nyingi sheria hazifuatwi, na matakwa ya kiongozi ndiyo hugeuka sheria. Mara zote, tawala za namna hii huwa zinaanguka pale kiongozi anapokuwa amaendoka maana watu hupata ugumu wa kuvaa viatu vyake. Hapa ndipo tunamsema Mzee Nyerere kwamba yeye binafsi alijitahidi kutawala, na hakuwa mwizi, lakini alituachia matatizo akitegemea kwamba wengine watakuwa kama yeye.

Jambo hili ndilo naliona kwa watu wengi hata ambao ni wanaharakati, kama Humphrey Polepole ambao wanataka CCM irudi kwenye misingi, lakini ukweli ni kwamba nchi inahitaji mfumo mpya (A New System of Governance). Neither CCM nor CHADEMA are parts of the new system, which I'm proposing here. Ndugu Polepole anaongea ukweli, lakini mimi siamini kwamba bila CCM basi hakuna Tanganyika. SIAMINI HATA KIDOGO.

3. LEGAL-RATIONAL AUTHORITY
Aina hii ya utawala ni ile ambayo uko kitaasisi na kimfumo. Uhalali (Legitimacy) wake unatokana na utawala wa kisheria (Rule of Law) na siyo kitu kingine. Ndani ya aina hii ya utawala ndiyo kuna kile kitu Professor Avey Dicey alikisema, "The Predominance of Regular Laws, Against Arbitrary Actions of Leadership", and "Equality Before The Law".

Kiongozi atakuwa na uhalali pale tu anapofuata sheria za nchi na miongozo yake, siyo sheria za CCM au CHADEMA. Hata vyama visipofuata sheria za nchi zilizotungwa na bunge vitatupiliwa mbali huko. MAHAKAMA (Judiciary), pia huwa zinakuwa na nguvu mno, ambapo hawezi akaamka kiongozi akaanza kujifanyia mambo yake anayotaka tu, kisa He's Charismatic.

UDHAIFU: Ni kwamba mkitegemea peke yake aina hii ya uongozi mnaweza kuwatenga baadhi ya wananchi kwenye suala zima la maendeleo. Hivyo basi, kwenye Legal-Rational Authority, kuna baadhi ya wenzetu huchanganya na Traditional Authority na kutengeneza A Mixed Government kama Uingereza. AU, Legal-Rational Authority na Charismatic Leadership, kama kipindi cha FDR na New Deal kule Marekani. A Balance has to be struck.

=====================================================================
Mimi msimamo wangu unabaki kuwa palepale. Tutengeneze KANUNI na MIFUMO imara ya kiutawala. KATIBA MPYA ni sehemu ya kwanza, lakini bina UWAJIBIKAJI wa WANASIASA waliochangia kutufikisha hapa, hiyo KATIBA MPYA itavunjwa na kusiginwa kihuni tena. Hivyo Laws+Sanctions= Proper Detterent.

Hivi ndugu NGURUVI, unadhani WAZUNGU wametuzidi sisi kitu kwenye UTAWALA ?
HAPANA, walichotuzidi ni UTAMADUNI WA UWAJIBIKAJI ambao ulijengeka baada ya matumizi ya sheria kusulubisha watawala wakandamizaji na wanyonyaji. Uingereza, walinyonga Mfalme wao (Charles I). Ufaransa, walinyonga Mfalme wao (Louis XVI). Baada ya kuonesha kwamba hadi Mfalme anagusika kulikuwa na adabu.

Marekani ndiyo taifa pekee duniani lililoanza vizuri. Mwaka 1782 wanamaliza vita na Uingereza na kutengeneza katiba walihakikisha kwamba kila mtu anahusishwa kwenye mchakato ili kuondoa maneno. Ile Marekani imepitisha katiba lakini wananchi wakalazimisha irudi bungeni ili kufanyiwa marekebisho wawekewa BILL OF RIGHTS kuzuia watawala wafalme (1St Amendment), na wakaenda mbali kutaka waruhusiwe kumiliki silaha zao ili kama Raisi akisumbua waingie mtaani (2nd Amendment).

Ndiyo maana Marekani kuna adabu, watawala wanafahamu fika kwamba siku ambayo watavuka mpaka, WAMAREKANI na mabunduki yao wataingia mtaani kufungua BUCHA. This is a serious state, a good form of governance. Serikali yoyote ile yenye nia njema na wananchi wake huwa haiogopi kuweka nguvu mikononi mwao na kutawala kwa kupitia GENERAL CONSENSUS. Serikali imewaamini raia wake na bunduki. MADIKTETA HUWA YANAOGOPA WATU kuwa na nguvu, ndiyo maana huamini sana katika utendaji binafsi na siyo mifumo imara.

=====================================================================
WATANGANYIKA tupo zaidi ya milioni 60. Ukiona kiongozi anakaa hadharani na kujifanya anasikiliza maoni ya watu na kero zao ili azitatue ufahamu fika hapo mnapigwa. Wewe unaweza kufanya hivyo kwa taifa zima ??? Huo uwezo utatoa wapi hata kama wewe ni SUPERMAN.

KANUNI + TAASISI IMARA + MFUMO, ndiyo vitatuepusha na DEMAGOGUES and POPULISTS. Kama taasisi hazitatui kero za watu, kamata hao watu funga, wengine nyongelea mbali, tena mbele ya ummah nchi itakuwa na adabu. Ila haya ya kutegemea watu ndiyo waje kutuokoa, nawaambia tutasubiri sana. MPAKA SASA HAKUNA MTU AMBAYE HAFAHAMU KWAMBA ADUI MKUBWA WA TANGANYIKA ni CCM.
​
 
Unaifahamu The Commonwealth Capacity Building Programme ???

Watanganyika/Watanzania wangapi walisomeshwa duniani kote kupitia hii ???
​
 
Mkuu MALCOM LUMUMBA
Ni bahati mbaya sana hukumwelewa Lissu kwa ile akili yake kubwa alipokuwa analiongelea lile suala kama ambavyo baadhi humu hawakuelewi kwa hoja zako ambazo wengi tumekubaliana nazo.

Twende taratibu.
Binafsi nawafahamu hata watu walioandaa nyaraka za Tanzania kwenye London Court of International Arbitration (LCIA). Tundu Lissu alijidanganya na akatudanganya. Kikawaida, kama kesi imefika kwenye Arbitration nchi huwa hazichomoki hata kidogo, maana ule huwa tu siyo uvunjifu wa CONCESSION bali BIT. Kama Acacia na Barrick walikuwa hawana makosa kwanini walikubali kuitoa kesi LCIA na BARRICK kuamua kuja mezani ???

Mikataba ya uwekezaji huwezi kuivunja tu, maana ina matabaka mawili. Tabaka la kwanza ni lile la kitaifa (At State Level) na Tabaka la pili ni lile la taifa na muwekezaji (At State vs Investor Level). Hivyo mtaishia kurekebisha mkataba wa Taifa na Muwekezaji. Na kuhusu yale makadirio, ilikuwa ni mbinu ya kuwaleta BARRICK mezani kwasababu ukweli ni kwamba ACACIA ilikuwa haina usajili wowote ile, hivyo ni kampuni hewa la kijanja-janja tu.

Mnyonge-mnyongeni, Haki yake Mpeni: Kwenye hili JPM aliwaweza wazungu. Ulikuwa ni mwanzo mzuri wa kutuma ujumbe kwamba nchi inafahamu kuwa BARRICK mnachukua madini zaidi ya yale yaliyokubaliwa kwenye mkataba.

Ukiuliza kwamba kulikuwa na umuhimu wowote ule wa kutishia kwamba nchi itashitakiwa MIGA sijui, halafu ukweli ni kwamba hata utaratibu wa kwenda MIGA nao akatudanganya. Aliwachota wengi ambao hawafahamu INTERNATIONAL LAW and INVESTMENT LAW. Ila uhalisia ni kwamba alitetea kampuni hewa na kutumika bila kujua. Mimi namkubali sana Lissu ila nafahami fika FRIJI LAKE HUWA HALIGANDISHI VIZURI.
​
 
Unaifahamu The Commonwealth Capacity Building Programme ???

Watanganyika/Watanzania wangapi walisomeshwa duniani kote kupitia hii ???
​
As I said earlier, baada ya muda wa kutosha ndiyo utapata idadi kubwa ya watu waliosomeshwa na hiyo program, shahada ya chuo kikuu ilikua lulu nchi hii,kama mpaka 2006 form six alionekana msomi
 
Ngoja nikupe scenario. Mfano Lowassa angefanikiwa kuwa Rais. Lissu labda angepewa uwaziri mkuu, Mbowe umakamu mwenyekiti. Rostam, swahiba mkubwa wa Lowassa angekuwa na influence kubwa kama aliyokuwa nayo kipindi cha Kikwete au sasa kipindi cha Samia.

Ufisadi ungeongezeka maradufu kupitia hao madalali watatu, Lowassa, Mbowe, Rostam na machawa wao. Lissu angekuwa sehemu, kiungo muhimu cha hao mafisadi kama waziri mkuu. Huoni hapo Lissu alikosea kufanya maamuzi sahihi, kukosa msimamo kumpambania Fisadi kuu na kumkaribisha kwenye chama kisa kuongeza viti vya wabunge. kupata madaraka. Inaonyesha lack of good judgement, foresight. The point is hakuna mkamilifu 100%.
 
Mkuu kwa haya unayoyaeleza hapa ili KUFANIKIWA ni lazima kupata mtu wa kaliba ya JPM sasa swali kubwa ni kwamba je Watanzania wana u tayari wa kuongozwa na mtu anayesimamia makubaliano(Sheria & Kanuni?)

Wapuuzi ni wengi sana Tanzania na wengi wataumia kwa kwa mazoea ya kupuuzia Sheria na taratibu.

Kwa nionavyo mimi na kwa mfano halisi niliojionea mwenyewe (JPM akiwa Madarakani) nachelea kusema

Watanzania bado hawana utayari huo wa kupitia mchakato huo au kuongozwa na mtu mwenye kusimamia misingi na hata hawa watu wa mtandao ni bure tu mnawatupia lawama ila ukweli ni kwamba watanzania wengi ndio wanapenda style hiyo ya maisha

Style ya kubebana bebana, kuchekeana chekeana na kikubwa zaidi kupeana uongozi siyo kwaajili ya kuwatumikia watu bali kama pumziko na sehemu ya kulainisha maisha baada ya msoto/kupigika.

Watanzania wanapoangalia maendeleo ya nchi kama China wanayatamani sana, lakini hawapo tayari kabisa kupitia mchakato huo mgumu waliopitia wachina hadi kufikia hayo maendeleo waliyoyapata wachina.
 
JPM alipata nafasi ila alishindwa kuzitumia katika kutengeneza mifumo ila aliamini katika yeye Mwenyewe na tatizo likaendelea kubwa kama angetambua kutengeneza mifumo Leo tungekuwa Taifa lenye thamani kubwa sana
 
Thank you brother, kuna vitu kuntu nimechukua hapa 🙏
 
Malcom hivyo story nyiiiingi japo zingine kama zina kitu hivi na ndefu zote zililenga kumponda slowslow je,kwanini apondwe na kwa maslahi ya nanii?Taifa ama Mtu ama Watu ama Kakikundi ka Watuuu?
 
Malcom hivyo story nyiiiingi japo zingine kama zina kitu hivi na ndefu zote zililenga kumponda slowslow je,kwanini apondwe na kwa maslahi ya nanii?Taifa ama Mtu ama Watu ama Kakikundi ka Watuuu?
Case in point.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…