Tusipofanya sasa, Tutajuta Milele, ni lazima Wamasai waondoke Ngorongoro

Tusipofanya sasa, Tutajuta Milele, ni lazima Wamasai waondoke Ngorongoro

Hivi kiuhalisia hamna sehemu nyingine ya kuishi zaidi ya kuishi pamoja na wanyama huko Ngorongoro?
somehow nakubaliana na comment yako, lakini jee unajua ni kwa nini hasa serikali inataka kuwahamisha wamasai? Kama ni kuwatunza wanyama ni kwa nini basi serikali inataka kukodisha sehemu hiyo kwa kampuni ya kigeni ili waendehs biashara ya trophy hunting?
 
Sasa kama wa hapahapa tetra maslahi ya Tanzania. Hadi wabunge wa Chadema waliopo Bungeni na waliostaafu kina Salome Makamba, Esther Matiko, Mchungaji Msingwa wamesimama na maslahi ya Tanzania pamoja na wabunge WAZALENDO wa CCM wewe kwa nini usisimamie maslahi ya Tanzania?
Hao ni mazuzu. Wana akili gani wale waliolazimisha kwenda bungeni kwa kuogopa njaa? Bila udhamini wa chama chao. Wana akili hao? Mtu mwenye njaa kali hawezi kuwa na akili.
 
Kama wewe ni mkenya kubali tu kuwa Tanzania imeamka. Lazima Ngorongoro tuilinde na maslahi ya Tanzania tuyalinde ili utalii uzidi kutuingizia fedha
Unajua kuwa sehemu hiyo inauzwa/inakodishwa ili kuanzishwe biashara ya trophy hunt? Tatayalindaje maslahi ya tanzania ikiwa tutaruhusu wanyama wetu wawe wakiuliwa kimchezo na wageni kutoka ulaya na nchi nyengine za mbali ya afrika?
 
Lete uthibitisho kuwa hii sehemu inauzwa au inakodishwa
Unajua kuwa sehemu hiyo inauzwa/inakodishwa ili kuanzishwe biashara ya trophy hunt? Tatayalindaje maslahi ya tanzania ikiwa tutaruhusu wanyama wetu wawe wakiuliwa kimchezo na wageni kutoka ulaya na nchi nyengine za mbali ya afrika?
 
Lete uthibitisho kuwa serikali inataka kukodisha Ngorongoro/ Loliondo kwa airing ya trophy hunting
somehow nakubaliana na comment yako, lakini jee unajua ni kwa nini hasa serikali inataka kuwahamisha wamasai? Kama ni kuwatunza wanyama ni kwa nini basi serikali inataka kukodisha sehemu hiyo kwa kampuni ya kigeni ili waendehs biashara ya trophy hunting?
 
Amani iwe nanyi

Kama kichwa cha uzi kinavyosema, Kama Mtanzania ninayeipenda nchi yangu, ninayejali maendeleo ya Watanzania wote vizazi na vizazi, leo nasema kwa Sauti moja, Kama tunajali maendeleo ya Tanzania yetu, Ni lazima wamasai waondoke Ngorongoro ili lile eneo liendelee kuwa na wanyama wengi na kuvutia watalii ambao ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato kwa Taifa letu

Kwa nini nasema haya?

1. Ngorongoro ni moja ya sehemu chache hapa Tanzania ambazo mtalii ana uhakika wa kuona wanyama walio kwenye hatari ya kupotea Duniani yaani Tembo, Faru, Simba, Nyati na Chui.

Nimefika ngorongoro kusema ukweli hadi Tour guides wanakwambia hivi karibuni imekuwa ngumu sana kuwaona baadhi ya hawa wanyama na sio tu hawa bali hata wanyama wengine ambao huko mwanzoni walikuwa ni wengi na wanaonekana kirahisi na kuvutia watalii wengi na kuongeza mapato mf pundamilia, pofu na wengineo. Hii ni kwa sababu wanadamu wameongezeka sana Ngorongoro na asili ya wanyama pori ni kuwa hawapendi kuchangamana na binadamu na shughuli za kibinadamu zikizidi huwa wanahama.

2. Kuna taarifa za uhakika kuwa Wanyama wanaohama Tanzania wanahamia upande wa pili yaani Kenya hivyo Kenya anafaidika kwa kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu Ngorongoro ambazo zinahamishia wanyama wetu Kenya. Hii ni hatari sana kwa uchumi wa Tanzania kwa sababu siku si nyingi, Watalii hawataona umuhimu wa kuja Ngorongoro na hivyo kwenda Kenya na kufanya nchi yetu kukosa Mapato.

3. Kuna taarifa za uhakika pia kuwa Wamasai waishio Ngorongoro hawana hata makabuli. Hivyo ikitokea mmasai amefariki anaachwa aliwe na fisi na mbweha. kibinadamu hii si sawa.

Napenda kumaliza kwa kusema imefika wakati sasa kwa maslahi mapana ya Tanzania, Wamasai wahamishwe Ngorongoro. Eneo hili ni nyeti na Tanzania nzima tunalitegemea kimapato. Likiangamia, Tanzania imeangamia. Ni wakati sasa Fedha zinazotengwa kuwalisha wamasai takribani bilioni 3-4 kwa mwaka zielekezwe sasa kuwajengea makazi ya kudumu wamasai hawa eneo jingine na kuwapatia teknolojia ya kufuga wanyama wachache tena kibiashara na kuachana na Maisha yale ya kijima

Naomba kuwasilisha!
Naona jamaa wa Dubai wanakusumbueni kwelikweli.

Ila Wamasai wa Ngorongoro hapo ni sehemu yao na muwaache waendelee kuishi hapohapo.

Huo uroho wenu wa fedha utajawatokea puani.
 
Naona jamaa wa Dubai wanakusumbueni kwelikweli.

Ila Wamasai wa Ngorongoro hapo ni sehemu yao na muwaache waendelee kuishi hapohapo.
Nakuona mkenya kwenye ubora wako! Watanzania kwa sauti moja tumeamua kuilinda Ngorongoro na kulinda mapato yetu yanufaishe vizazi na vizazi. Nyie na mipango yenu ya kutuulia Ngorongoro yetu jueni tu mmeshindwa
 
Kati ya November 2015 na March 17 2020 wapigaji hamkuthubutu kuja na hizo ngonjera zenu.
 
Tunga ngonjera nyingine wewe pandikizi la Kenya
Weye si ndie uloleta hio ngonjera yako?

Wataka Wamasai waondolewe sehemu yao ya asili na wameishi na wanyama miaka nenda rudi.

Hizo ni akili kweli?

Wamasai, wasandawe, wamang'ati na makabila mengine yaishio kiasili (weye waita Ujima) waachwe waishi kwenye maeneo yao.

Kwa Ngorongoro, kama mwataka fedha zaidi za utalii boresheni maeneo hayohayo ili wanyama waendelee kuishi kiasili na wamasai nao wandelee kuishi kiasili.

Ila tabia za kupenda fwedha si nzuri kwani siku ukiaga dunia utawaacha hao wamasai, Ngorongoro na hao waarabu wawindaji wenu.
 
Mbona tuna vivutio kibao. Why Ngorongoro Conservation Area?
 
Lete uthibitisho kuwa serikali inataka kukodisha Ngorongoro/ Loliondo kwa airing ya trophy hunting
Kwa vile mie siko serikalini, siwezi kukuletea ushahidi kamili wa documents za kuthibitisha hili wala lolote lile ambalo serikali inapanga kufanya mahali popote pale. Sijui mwenzangu kama unakuwa na uwezo kama huo wa kuona kwa udhati kabisa mipango yote ya serikali. However ninacho elewa mimi ni kuwa habari zinazoripotiwa na vyombo vya habari mbali mbali vya nje ya nchi ambavyo naamini wana source za uhakika kuliko mimi na wewe. Vyombo hivi ndivyo vinavyotaja kampuni moja tu OBC kuwa imekodishwa (vyombo vyengine wanasema wameuziwa, but that is no the point here). Sasa basi OBC ni kampuni ya mawindo inayomilikiwa na UAE royal family, kampuni hii hii ndio ambayo ina share ya aina ya trophy hunting nchini south africa na Botwana.

Kwa taarifa hiyo basi ikiwa serikali inakusudia kuwakodisha au kuwauzia OBC sehemu hiyo basa biashara ya kuwavutia watalii wanayokuja kuifanya OBC ni ya trophy hunting tu na wala silo jengine!

Nitamaliza kwa kukugeuzia meza kidogo, tupatie taarifa ya ukanushi kutoka serikalini ya kuwa haikukusudii kuliuza au kukodisha sehemu hii kwa kampuni ya OBC.

Kumbuka tu kwa upande wangu haya sio mabishano ila ni maelekezano.
 
Kwa kukiri tu kuwa huna ushahidi/ ushahidi hutakiwi kuendelea kuongea lolote.

Kalale. Sio kipindi cha propaganda hiki
 
Mbona tuna vivutio kibao. Why Ngorongoro Conservation Area?
Ngorongoro ni moja ya vituo 3 vinavyoliingizia Taifa mapato makubwa zaidi kutokana na shughuli za kiutalii.

Ikifa Ngorongoro ni sawa na kusema sekta ya Utalii imecollapse Tanzania
 
Weye si ndie uloleta hio ngonjera yako?

Wataka Wamasai waondolewe sehemu yao ya asili na wameishi na wanyama miaka nenda rudi.

Hizo ni akili kweli?

Wamasai, wasandawe, wamang'ati na makabila mengine yaishio kiasili (weye waita Ujima) waachwe waishi kwenye maeneo yao.

Kwa Ngorongoro, kama mwataka fedha zaidi za utalii boresheni maeneo hayohayo ili wanyama waendelee kuishi kiasili na wamasai nao wandelee kuishi kiasili.

Ila tabia za kupenda fwedha si nzuri kwani siku ukiaga dunia utawaacha hao wamasai, Ngorongoro na hao waarabu wawindaji wenu.
Kwa maslahi mapana ya Taifa, ni lazima wahame
 
Back
Top Bottom