Pasco
Ndugu Pasco,
Ninashukuru kwa hoja yako ambayo inafikirisha kwa wale wapevu wa fikra.
Naomba uelewe kuwa CCM ni chama ambacho kina uwezo wa kujitathmini, kugundua makosa na kujisahihisha.
Uwezo huo umekiwezesha/unakiwezesha kurudisha Majimbo ambayo kilipokonywa na wapinzani.
Naomba uelewe kuwa, CCM ilishalishawahi kulichukua tena jimbo Arusha Mjini kutoka kwa Makongoro Nyerere. Vile vile kuna majimbo mengi tu ambayo CCM ilipoamua kuyarudisha, iliyarudisha. Baadhi yake ni kama Kigoma Mjini ya Dr Walid Kaborou (CHADEMA) ambaye alidodoshwa na Peter Serukamba. Jimbo la Temeke kutoka kwa Mrema, Mwibara kutoka kwa Mutamwega, Ubungo kutoka kwa Lamwai, Siha kutoka kwa Makidara Mosi, Kyerwa kutoka kwa Benedicto Mtungurehi. Etcetera, etcetera
CCM imejipanga tena kurudisha majimbo kama Arusha Mjini, Vunjo, etc.
Ni kweli kuna maeneo mengi ambayo CCM iliwapa majimbo wapinzani kutokana na makosa na udhaifu wake wa kiuongozi. Mchakato wa kuchagua wagombea na uwepo wa makundi ulikidhoofisha chama wakati wa kampeni za kitaifa.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Kikwete alishawahi kugusia matatizo yaliyokifanya chama kupoteza majimbo mbali mbali.
Mwenyekiti alisema,"Kama kiongozi unatosha kwenye mchakato wa chaguzi za ndani utapita na kama hautoshi huwezi kupita. CCM inaweza kuingia madarakani mwaka 2015 iwapo uteuzi wa wagombea utafanyika vizuri bila dhuluma, kuoneana na kukasirisha watu. Tusifanye makosa haya tena kwa kuwa siku hizi watu wana chaguo mbadala, wanaodhani kila anayeteuliwa na CCM atashinda, hawako dunia hii kwani kuna maeneo tulifanya makosa tukaona adhabu yake.
"Tusiwaonee watu katika uchaguzi, tusiwadhulumu na kuwasukuma ukutani bila sababu, kama ipo tuwaeleze ukweli. Tusiifikishe CCM mahali sipo, ambapo tutakuja kujuta, itafika mahali tutapata Rais halafu tukawa na wabunge wengi wa upinzani, au Rais akawa wa upinzani wabunge wengi wakawa wa CCM, itakuwa ni hatari, tutaendesha vipi Serikali,"
Mwenyekiti wa Chama aliendelea kusema, "Ikifika mahali CCM ina wanachama milioni sita, lakini wakati wa uchaguzi kura za mgombea wa CCM na za mgombea wa upinzani ukijumlisha kwa pamoja zote hazifikii idadi hiyo, basi viongozi mmeshindwa kuongoza wanachama wenu,".
Usishangae kwa nini viongozi wa CCM tokea Mkutano Mkuu umalizike wako sehemu mbali mbali wakiwatembelea wananchi achilia mbali mikakati mengine ambayo haiwekwi kwenye public domain.
Wahenga walisema, kufanya kosa siyo kosa bali kurudia kosa ndiyo kosa!