Tusipokubaliana na mtazamo wa Godbless Lema, CCM itaendelea kutawala na katiba ya Sitta itapita

Tusipokubaliana na mtazamo wa Godbless Lema, CCM itaendelea kutawala na katiba ya Sitta itapita

Umeongea sahihi kabisa,hembu ona walimu wanakatwa mishahara eti wajenge maabara,jee kikwete na baraza lake la mawaziri watakatwa hizo pesa pia?Wanajua waalimu ni dhaifu waoga ndio maana wanawachezea hivyo!Ingekua nchi zilizoendelea rais angekua hana kazi muda huu

Unajua kufanya kz ya ualimu hapa Tz unatakiwa sehemu ya Ubongo wako ama iwe domanti au imekufa vinginevyo utapata shida sana.

Tujiulize mbona zahanati na hspl zinapojengwa hatusikii kama madaktari wanakatwa kuchangia, au au uwanja wa ndege, Barbara tukasia kuwa wafanyakazi Katuka idara hz wanakatwa mshahara kuchangia?

Kama ningekuwa mwalimu hata shilingi Moja tu kukatwa kwa Maelezo ya kiwendawazimu kama haya ilikuwatosha kuacha kz
 
pasco nyamaza kimya huijui arusha, umeitaja unga ltd hiyo kata ipo ccm arusha tunataka vitendo sio maneno. maneno yenu uongo hatuyataki siipendi ccm siipendi chadema
Mkuu , sio tuu naijua Arusha, bali nimeishi Arusha, nimesoma Arusha, na kampeni za Lema, nimehudhuria!

Naomba nikukumbushe hapa
Wanabodi

Nilipata ka vakasheni kafupi, hivyo nikaamua kwenda kujipumzisha mikoa ya Moshi na Arusha
juzi na jana.

Kwa Upande wa Arusha, jana nimehudhuria kampeni za Mgombea wa Chadema, Godbless Lema pale Levolosi Desemba na kumalizia kampeni za Mgombea wa CCM, Dr. Batilda Burian Pale Kaloleni,.
Wakaazi na wenyeji wa mji wa Arusha nchi yetu iko kwenye matayarisho ya uchaguzi mkuu October 2010.Nimeona ni vyema na haki tukawajadili wagombea ubunge wa vyama vitatu ambavyo nini hakika wataleta ushindani mkali.

Mgombea Ubunge wa CHADEMA
Godbless Lema elimu yake haijulikani kabisa na ni moja ya mambo yaliyochangia kupunguza kura zake katika uchaguzi wa mwaka 2005.Anadai anacheti cha Computer lakini hatakia kutaja jina la chuo alichosoma wala mwaka aliomaliza.Anadai alimaliza kidato cha sita lakini hataki kutaja jina la shule aliyosoma wala mwaka na alama alizopata ??????????.
Godbless Lema haijulikani anafanyakazi gani haswa, mara nyingi anapenda kujiita mfanyabiasha za madini na wakati mwingine anadai kununua vitu mbali mbali Dubai & Japan.Hana ofisi ya biashara inayojulikana muda wake mwingi anapenda kukaa mitaani kuzungumzia mambo asiyoyajua vyema kwa kujidai anayajua kuliko mtu mwingine.

Godbless Lema ni dalali mzuri wa siasa za upinzani anajua kucheza karata zake vizuri sana huku akiyatanguliza maslahi yake binafsi.Bwana Lema anahusika bila shaka yoyote alifanikisha deal ya kumuondoa Diwani wa TLP Sombeti Bwana Mawazo na kumpeleka CCM kwa ujira wa pikipiki za mafisadi na kiwanja.Baada ya kutimuliwa TLP akakimbilia CHADEMA na amefanikwa kujinyanyua hadi akapitishwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA .wanamageuzi bado wanakumbuka jinsi alivyoiondoa kesi ya kupinga ushindi wa Mheshimiwa Felex Mrema mahakamani bila kuwashirikisha viongozi wa chama wakati chama kilitoa fedha za kugharamia kesi.Ilikuja kubainika Bwana Lema alipewa kitu kidogo ili kuiondoa kesi mahakamani.

Godbless Lema akifaniwa kuwa mbunge wa Arusha mjini ataongeza idadi wa viti vya wabunge wa upinzani jambo ambalo ni jema na afya kwa demokrasia ya Tanzania lakini hatakuwa na mchango wa maana bungeni kama akina Dr Slaa na Zitto Kabwe sana sana ataongeza idadi tu.
Godbless Lema anategemea zaidi umaarafu wa CHADEMA kuchaguliwa anatamani sana wapiga kura wasahau alivyorubuniwa na CCM mara mbili.
[1] Kumpeleka Mawazo CCM.
[2] Kufuta kesi ya kupinga ushindi wa Felex Mrema .
[3] Atapenda wapiga kura wasihoji elimu yake.
[4] Atapenda wapiga kura wasihoji kazi yake.
[5] Atapenda wapiga kura wampigie kura kwasababu ya umaarafu wa CHADEMA na Dr Slaa.

Ngongo, asante kwa uchambuzi yakinifu kuhusu kinyanganyiro cha ubunge Arusha.
Uongozi ni kipaji na uwezo na sio elimu, japo elimu ni just an added advantage, kama mtu ana uwezo wa uongozi hata darasa la saba, atakuwa kiongozi bora, ndio maana kuna mababu zetu hawakusoma, lakini walikuwa viongozi wazuri tuu wenye busara. Wapinzani lazima waungane, vinginevyo Arusha hiyo...CCM!.
Heshima kwako Pasco,

Nakubaliana tena na hoja yako kwamba uongozi ni kipaji na uwezo lakini pia elimu ina nafasi yake kubwa sana.Kuna mambo ya hovyo yaliyowahi kufanywa na Bwana G Lema amabayo ukiyatafakari unagundua pia ukosefu wa elimu ulichangia sana.Mkuu Pasco unaweza kuchagua wabunge wenye elimu ya darasa la saba au chini ya kiwango hicho Korogwe,Iringa,Mbeya na Rorya lakini mbunge mwenye elimu hiyo hafai kabisa Arusha hasa tukizingatia mazingira yake kama mji wenye pilika pilika za mikutano ya kimataifa,makao makuu ya EAC na mashirika mbali mbali ya kimataifa.
.
Ngongo, sina ubishi kuhusu umuhimu wa elimu kwa mtu yoyote na inapokuja kwa mgombea ni muhimu zaidi, kati ya majimbo yaliyoitekeleza ilani ya CCM kwa asilimia 100% ni jimbo la Masilingi, lakini kwenye kura za maoni, CCM wamempiga chini kisa miongoni mwa washindani wake kuna aliyekuwa nshomile zaidi, na kwa wenzetu kadri ulivyo nshomile zaidi, ndivyo unavyoheshimika zaidi.

Kwa Moshi na Arusha mjini, heshima ya mtu ni fungu ambalo hujionyesha kwa life stlye, unafanya nini, unaishi vipi, unaendesha gari gari, unakunywa wapi, na unajichanganya na kina nani. Kama kijana yuko fiti hizo idara nyingine zote, bado jimbo la Arusha lina nafasi ya kuangikia upinzani.Tatizo la huyo mgombea wa Chadema kwa upande wangu, ni ubishoo tuu wa kutaka mambo makubwa, kujifanya yuko juu ili hali ni mtu wa kawaida tuu, ila kwa kukubalika na machalii wa mjini hapo, anakubalika.
Pasco
 
Pasco

We jamaa mnafiki sana wewe!Ulikuwepo Arusha ipi wakati wa uchaguzi?
Unawajua waliosimamia matokeo halisi ya uchaguzi yatangazwe pale kwa mkuu wa mkoa?
Arusha hawaishi kwa kutegemea bahasha..mburula nyie.

Kwa taarifa yako maandamano hujumuisha watalii vile vile...

Arusha ni nyumba ya upinzani toka enzi na enzi.Kaa huko huko bongo uendelee kuishi kwa vibahasha Arusha huijui!!!
 
Last edited by a moderator:
Pasco

We jamaa mnafiki sana wewe!Ulikuwepo Arusha ipi wakati wa uchaguzi?
Unawajua waliosimamia matokeo halisi ya uchaguzi yatangazwe pale kwa mkuu wa mkoa?
Arusha hawaishi kwa kutegemea bahasha..mburula nyie.

Kwa taarifa yako maandamano hujumuisha watalii vile vile...

Arusha ni nyumba ya upinzani toka enzi na q.Kaa huko huko bongo uendelee kuishi kwa vibahasha Arusha huijui!!!
 
Last edited by a moderator:
Sawa pasco ila wewe unaonaje mwalimu kuambiwa achangie maabara ni saw a hiyo?mbona sijasikia mjeshi aambiwe kujinunulia kombati kwasababu anavaa mwenyewe na analichakaza mwenyewe,daktali achangie kununua vifaa vya hospital?hapo ndo utaona upole wa mtanzania.Leo nimeona mwigulu anajisifu kachangiwa hela ya fomu ya uraisi kwanini asitumie fursa hiyo kufanya harambee ya kitaifa juu ya Ujenzi wa maabara kuna watanzania watachangia vizuri zaidi ya mwalimu anayeonewa
 
Ili CCM itoke madarakani, CHADEMA jifunzeni kwanza kutoogopa wale jamaa wa FFU.
 
Pasco
Acha kuhadaa watu Pasco unataka kituamhia hapa Lema asinge hamasisha watu kulinda kura kwa nguvu zote nakuwapa ujasiri angepita kuwa mmbunge? tuliona kilichotokea shinyanga mjini kwa Marehemu Shirumbishela alishinda uchaguzi tatizo uwoga wa Raia kura zikaongezwa kama Sita vile bungeni ha ha haaaaaa!Pasco bana!leo umecheka analysisi yako.
 
Last edited by a moderator:
Jackbauer
Mkuu Jakibawa, asante kwa hili, nilikuwa Arusha ipi mbona nimeeleza!, tena ushukuru sana sijayaelezea yaliyotokea Impala wakati wa Kampeni!. Kuhudhuria mikutano ya kampeni hakuna uhusiano wowotw na kuwajua waliosimamia uchaguzi, nimesema nilihudhuria kampeni na sio kuhudhuria uchaguzi!.

Hilo la bahasha, Arusha ndio mwake mwake!, na kwa taarifa kila nikitia timu Arusha siku hizi, huja kuzimwaga hizo bahasha, kuanzia tarehe 20-26 nitakuwa hapo Naura, kuja kuzigawa bahasha nene za nguvu!. Afadhali ya Dar, hata bila bahasha mambo yanakwenda!, kwa Arusha bila bahasha!, hakiendi kitu!.

Pasco wa jf ni Arachuga kwa sana tuu!.

Pasco.
 
Last edited by a moderator:
WILLAFRICA Pasco: Umeteleza kiufikiri kijana jipange upya.

Mara nyingi Pasco hujipambanua kama mwanafikra ila nadhani partiality inamnyina kuwa pragmatic and objective thinker.
 
Pasco

Kusoma post zako niburudani unapima upepo tulisha jua janja yako wewe palilia ugali wako Lowassa akiwa Rais utakuwa Mkuu wa mkoa Arusha lazima uje si nyumbani kwa Lowassa eti kwenu!!
 
Last edited by a moderator:
Mikael P Aweda

Mtu yeyote mwenye Maono na Hekima nilazima atafakari Jambo lolote kabla yakutenda! matokeo yake kwa jamii katika mitazamo yote miwili hasi na chanya.Pengine sijamwelewa mleta mada Mana lema hatumii maarifa au akili badala yake ni nguvu ya mwili "Mfano maandamano kwa watu ili maswahiba wake wafanye maasi yakuiba mali za watu,wengine wafe ili tu yeye apate umaarufu na neema kwa familia yake"Tofauti na hapo anatumia nguvu na sio akili na ndipo watu wakaliba yake au namna yake huona ndio akili halisi.Hata hivyo hakuna mwovu aliye mwoga.Pole mleta mada ni mawazo yako ila umefikiria kidogoooo! Think BIG
 
Last edited by a moderator:
Pasco

Ni kweli ila hapo unajaribu kucheza na maneno kwani naona kabisa unalazimisha hoja yako. Unaposema Lema ni kiazi nikueleweje wakati kabla hajaingia madarakani waliokuwepo ni wabunge wa ccm. Kama kweli maendeleo yalikuwepo ilikuwaje mapato ya halmashauri yawe machache? Unapozungumzia uwezo ni upi labda ni wa kutoa pesa zake mfuko ajenge mabarabara, mahosptal, au awagaie makanisa ili apate uungwaji mkono ama wa darasani? Kama ni hivyo mbona kwenye katiba hii, japo naona hata wewe unajua kabisa ni ushindi wa mezani wameweka kipengele cha mtu kujua tu kusoma na kuandika ambavyo Lema anavyo muda mrefu tu.Kama kweli Lema ni kiazi ni yupi basi bora yeye Lema anayewataka wananchi waandamane kwa amani dhidhi ya watawala kwa kuminya haki, ama ni hao watawala wasomi waliotuingiza kwenye hii mikataba ya kinyonyaji mpaka kufikia tunalipa umeme bei ya juu sana, na unaweza kukatika mara kwa mara na tusiweze kuhoji?

Nyinyi waandishi kwa sehemu kubwa ndio tatizo la nchi hii, huwa nakuangalia unayemtetea hapa nachoka kabisa. Sikatai ndio demokrasia lakini kumbuka ni vizuri ukawa upande sahihi na sio kumshabikia ambaye kwenye jamii amechafuka. Nadhani hiki kinachoendelea huku mitandaoni dhidi yenu toka kwa akina Chabruma kinadhibitisha hilo. Ni nani anayetaka Tz ijayo kuuongozwa na watoa rushwa? Kwanini nyinyi kama waandishi wa habari wangalau mkikutano huko msiweke utaratibu wa kuita think tank wa nchi hii ili waendeshe mijadala ya wazi, watoe mawazo ya kuendeleza nchi na kutoa utambuzi kwa umma juu ya viongozi wazuri na sio watoa rushwa? Au ndugu yangu wewe hukuwa unaona kinyaa watu kukata mauno siku ile bungeni watu wakishangilia ushindi wa mezani kwa rasimu ya hila itakayoendeleza tatizo letu la msingi la uongozi mbovu? Au wewe unaamini kwamba wakulima, wafugaji, nyinyi waandishi wa habari mtapa haki zenu toka kwenye katiba ijayo kwa viongozi walioamua kujitengezea katiba ya kuwafanya mungu watu? Pasco una watu tunaokuheshimu na tutaendelea kukuheshimu japo tatakupuuza kuwa sehemu ya kushabikia viongozi wenye doa. Au na wewe ndugu yetu umekulia kwenye hiki kizazi cha propaganda za amani, wakati wanaosema mjali amani wanaficha mikataba, wanachakachua kura, wanatumia dola kubaki madarakani lakini sio uwezo wa hoja na mawazo chanya ila kuongoza kwa mazoea baada ya kukamata mrija katika shamba la bibi?
 
Last edited by a moderator:
Sawa pasco ila wewe unaonaje mwalimu kuambiwa achangie maabara ni saw a hiyo?mbona sijasikia mjeshi aambiwe kujinunulia kombati kwasababu anavaa mwenyewe na analichakaza mwenyewe,daktali achangie kununua vifaa vya hospital?hapo ndo utaona upole wa mtanzania.Leo nimeona mwigulu anajisifu kachangiwa hela ya fomu ya uraisi kwanini asitumie fursa hiyo kufanya harambee ya kitaifa juu ya Ujenzi wa maabara kuna watanzania watachangia vizuri zaidi ya mwalimu anayeonewa

Ajabu unaweza kukuta hata hao watu wanaojifanya wamemchangia Mwigulu ni yeye mwenyewe kawapa hela.
 
Ajabu unaweza kukuta hata hao watu wanaojifanya wamemchangia Mwigulu ni yeye mwenyewe kawapa hela.
Ni kweli unachosema ila concept ya kuchangisha ingewekwa katika mambo ya maendeleo ningekubali zaidi,mfano mwigulu angefanya harambee jimboni kwawadau wa maendeleo kumchangia maabara badala kumminya mtumishi
 
Arusha inahitaji kutumia busara kuhakikisha Lema haendelei kuwa Mbunge, wakiendekeza matakwa ya "machalii" Mji utaendelea kudorora kama tuonavyo sasa, Lema hana akili ya ziada...zaidi ya kusisitiza vijana "acheni uoga" hakuna mbinu mbadala alizowasaidia wajikomboe.

Amewatumia vijana kumpigania tofauti zake na Meya, leo hii waliokufa wameshasahaulika yeye na huyo Meya bado wanakula maisha.....mnawajaza vijana ujasiri wa kijinga kwa manufaa binafsi.

Kama serikali ya Uganda wangemdhibiti Kibwetere mapema asingefikia kuangamiza roho za watu kama vile.....Lema ni Kibwetere.
 
Pasco

Unapoongelea ukiazi wa baadhi ya wabunge wa CDM... kama waTz wangekuwa wanachagua watu kwa uwezo wao (kiuelewa na kitaaluma) nafikiri wabunge wengi wa chama tawala wasingekuwa wabunge leo hii, mf jah people, Kibajaj, etc.

Sidhani kama swala la kutokuwa kiazi ni factor kubwa kwenye kuchaguliwa kwa nchi hii. Ingekuwa hivyo tusingeshuhusia mipasho na vitorondo vikichezwa kwenye bunge letu, tungeshuhudia watu wakitofautiana kwa hoja tu.
Arusha ni sehemu ambayo, hata kiazi kikiweje ilimradi ni cha CDM kina nafasi kubwa zaidi ya kupita vinginevyo CCM wachakachue kura, Chalinze ni sehemu ambayo hata kiazi kikiwaje ilimradi ni cha CCm kitapita tu hata kama upinzani ungekuwa madarakani
 
Last edited by a moderator:
tindo

Pasco ameamua kujivua ufahamu. japo kuna wakati anataka kuonyesha kwamba yeye hayupo upande wowote ila ukisoma between the lines unaelewa anachokishabikia. Kilichobaki kwa sasa aachane na habari ya kujaribu kufanya critical analysis, aweke mambo hadharani tu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom