Tusipokubaliana na mtazamo wa Godbless Lema, CCM itaendelea kutawala na katiba ya Sitta itapita

Tusipokubaliana na mtazamo wa Godbless Lema, CCM itaendelea kutawala na katiba ya Sitta itapita

Lema Arusha anabebwa na Wachagga wenzake.. Siasa za Arusha zimejaa ukabila na udini

Lema ashukuru sana Arusha kuna wachagga wengi

Godbless Lema ni think tank ya CHADEMA kwa sasa na kwa maana hii, CHADEMA kinafanya vizuri sana katika uwanja wa siasa!.

Eti CCM hawawezi kushinda Arusha.

Eti Watanzania ni waoga.

Eti Godbless Lema ni jasiri.

Mnatoa matamko, mnahamasisha migomo na maandamano lakini watanzania wanawapuuza siyo kwa sababu ya uwoga wao bali kwa sababu ya hekima na busara zao.

Kama kweli Godbless Lema ni jasiri na ana mbinu za kisiasa za kuishinda CCM, ilikuwaje katika kampeni hii,




Kwa nini hakutumia ujasiri wake na kulichukua jimbo la Kalenga?

Busara kama za laki si pesa za kufanya wachaga si raia wa nchi hii si ndio? Wachaga wapo wanawaangalia tu watafanya maamuzi katika mda muafaka.
 
MwanaDiwani
Mkuu MwanaDiwani, asante kwa ukweli huu japo ni mchungu kwa wapinzani ila ndio ukweli wenyewe!.

Kuna watu humu, wanawasifu sana wabunge wa Chadema kuwabwaga CCM, huku sifa zikipelekwa kwa hao wabunge individually, huku tukiwajua fika sio tuu ni weupe kisiasa, hata vichwani mwao, hamna kitu kabisa!. Hili la baadhi ya wabunge wapinzani kuukwaa ubunge kwa makosa na udhaifu wa CCM ni kweli kabisa na katika uzi wangu huu, CCM Imechokwa; CHADEMA Haijajipanga!, nililisema wazi.

Ila pia kuna maeneo CCM kamwe hamuwezi kuyagomboa, unless aliyepo aamue mwenyewe kuwa ubunge sasa basi!, haya ni majimbo ya Moshi Mjini, Moshi Vijijini na Bariadi Mashariki kwa Ndesa, Mrema na Cheyo!, respectively, ambao wote wameisha jichokea kabisa!, na wakisomama tena, wataishia njiani, ila licha ya uchovu vote huu, hanu maandalizi yoyote ya warithi wao, na hata wakisimama katika uchovu walio nao, CCM haiwezi kuwang'oa!.

Ila kwa Arusha, ni kweli ile 2010, CCM mlifanya makosa!, na Lema sio kisiki kabisa, hivyo 2015 kama CCM iko makini, Lema anang'oka!, na hili likitokea, Chadema ndio watakuwa wajinga wa mwisho kuwa underestimate wakazi wa Arusha, baada ya kuchagua "kiazi!" ile 2010, na 2015 inawarudishia tena "kiazi" kile kile bila mabadiliko yoyote!.

Pasco.
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana wana wa Lumumba ukweli wa Arusha ni chadema Ccm yanaangaika mpaka yanashikana mashati officini lakini chama pendwa Arusha nichadema natutaendelea pendwa sana ccm nimakapi
 
Bravo!! Wewe ni mtu makini sana pasco. Hili liaweda pamoja na elimu yake kubwa limebaki hivyo hivyo lilivyoanza chuo, ie ametoka kama alivyoingia
Na wewe nawe umeshikiwa akili na Pasco? Huna akili za kujiongoza mwenyewe?? Kweli CCM kumejaa misukule tu.
 
Mikael P Aweda

Hata hueleweki, nani kakwambia eti Godbles sio mwoga! Hilo jamaa ni tangu lishughulikiwe jela, ni joga balaa! Muulize maandamano haya aliandamania wapi? Msimpe sifa isiyo yake. Arusha na Moshi kuwa ngome ya chadema haitokani na ushawishi wa Lema, bali ni sehemu ambako saccos hii ilikoanzia ya wapiga dili, na unawajua watu wa huko,kila kitu kinachohusu hela kwao ni dili.
 
Last edited by a moderator:
Unajichanganya mara useme arusha ccm imechokwa mpaka basi mara useme itashinda ebu acha kuwa popo
Mkuu KABERWA2013, asante kwa hii!.
CCM kuchokwa ni kweli, na nikaeleza kuna maeneo imechokwa mpaka basi kiasi kwamba hata Chadema ingesimamisha jiwe!, hilo jiwe lingepita!, ni baada ya wananchi kulichagua jiwe na kujikuta kumbe hilo haliwezi kufanya chochote kuwaletea maendeleo, sasa ukilirudisha tena kwa matarajio litachaguliwa tena!, wananchi hao sio wajinga kuendelea kuchagua jiwe!, bali sasa watamchagua mtu hata kama ni kutoka chama cha mazwimwi!.

Mimi huyu nimetyamka humu sio mara moja wala mara mbili kuwa CCM imechokwa!, lakini bado ni mimi huyu huyu ambaye kila siku ninaeleza humu kuwa uchaguzi wa 2015 ni CCM tena!. Nenda kanisome hapa CCM Imechokwa; CHADEMA Haijajipanga!.

Ila pia humu jf, tuna watu waelewa, hawa huwa wananielewa vizuri mimi Pasco wa jf!, pia tuna watu wajinga, hawa wakielimishwa huwa wanaelewa, kama nilivyokuelimisha wewe ukanisome kwenye uzi huo niliokuelekeza!. Kuna wajinga wakielekezwa kwenda soma, kwa kutaka kujua, huwa wanakwenda kusoma na kuelewa!, ila pia humu jukwaani tuna mijitu mijinga!, hii mijitu mijinga, haina uwezo wa kiwango cha ufahamu kuelimishwa ikaelimishika, na kuelewa, hii hata uwezo wa kusoma na kuelewa maana halisi huwa ni kazi!, na hata ikiambiwa ikaseme ili kuelewa na kuachana na ujinga!, huwa haijisumbui hata kusoma maana haita elewa!, ni mijinga hii ndio iliyo idadi kubwa na ni mijinga ya aina hii, CCM inaitegemea sana kuwaletea ushindi!.

Wawe Mkuu,KABERWA2013 uko kundi lipi?!.

Pasco
 
Mazombi ya CCM yanaruka na kukanyagana. CCM Arusha ni taka iliyooza.
 
Pasco unapotosha. Nani amekwambia Lema hapendi maendeleo? Watu wa Arusha ni walipaji wa kodi wazuri, na kwa taarifa yako mapato ya jiji la arusha yamepanda sana toka madiwani wengi na mbunge kuwa wa cdm. Maandamano ya amani ni haki ya kikatiba mambo yanapoenda ndivyo sivyo.
Mkuu Tindo, asante kwa hii, ila nani amesema Lema hapendi maendeleo?!, mimi nimezungumzia sula la kupenda hapa?!, kuleta maendeleo ni issue ya kupenda?!, au ni uwezo?!.

Kupenda ni one thing, na uwezo wa kupata hicho unachopenda is another!.

Mfano mimi napenda kumiliki usafiri wa motokari, uwezo wa kipato changu ndizo zile buku 7 saba la Lumumba kwa wiki!. Hata nipende vipi motokari, nitaweza vipi kuimiliki kwa kipato hicho, sana sana nikijitahidi hadi mwisho wangu ni kukopeshwa baisikeli, au kuisubiria ile neema ya "Mwamba wa Kaskazini!", kutokopesha tuku tuku!.

Kupenda ni one thing, uwezo ni another!.

Pasco.
 
Umeongea sahihi kabisa,hembu ona walimu wanakatwa mishahara eti wajenge maabara,jee kikwete na baraza lake la mawaziri watakatwa hizo pesa pia?Wanajua waalimu ni dhaifu waoga ndio maana wanawachezea hivyo!Ingekua nchi zilizoendelea rais angekua hana kazi muda huu

acha uongo mbona wa kwangu aujakatwa na mm si dhaif ni kamanda wa front lne.
 
Pasco

Unaonyesha post zako zinategemeana kama episodes za tamthilia ya days of our lives.itakuwa ngumu kukufuatilia.nashauri uandike content moja inayojitosheleza.ili uweze kufanya hivi kwanza jiulize possible questions kutoka kwa watakaokusoma kisha zijibu.kumbuka wote tukishinda jf kusoma kila post na kurudia za nyuma tutashindwa kujenga taifa hili changa.ni lazima ku-spare muda wa kufanya mambo mengine.ukitaka kujua niko kundi soma vizuri hii post yangu alafu unipe jina niko kundi gani kwa mtazamo wako
 
Last edited by a moderator:
pasco nyamaza kimya huijui arusha, umeitaja unga ltd hiyo kata ipo ccm arusha tunataka vitendo sio maneno. maneno yenu uongo hatuyataki siipendi ccm siipendi chadema nampenda mbunge wangu. hata lema akiamia ccm nitamchagua kwa kukuonyesha tunapenda vitendo alienda jela mwenyewe akarudi mandela kenyatta baba wote walipita jela mwambie january makamba aende hahahahahahaha
 
pasco nyamaza kimya huijui arusha, umeitaja unga ltd hiyo kata ipo ccm arusha tunataka vitendo sio maneno. maneno yenu uongo hatuyataki siipendi ccm siipendi chadema nampenda mbunge wangu. hata lema akiamia ccm nitamchagua kwa kukuonyesha tunapenda vitendo alienda jela mwenyewe akarudi mandela kenyatta baba wote walipita jela mwambie january makamba aende hahahahahahaha

Kwa hiyo unampenda lema kwa sababu ameenda jela?
 
Pasco,jifunze siasa za kimataifa ndo utaelewa nguvu na maana ya maandamano MF.hong Kong fuatilia kwanini wanaandamana na watafaidika nini baada ya kusikilizwa,sijawahi sikia nchi ya watu walioelimika kukomaa kisiasa na RAIA kujua haki zao wakaulizwa mnataka maandamano au barabara muujiza hiyo naiona TZ kwasababu wananchi wengi hawajui haki zao na wajibu wao ndomaana wanayumbishwa.ila iko siku wataelewa tu na kutaka kujua kwanini kuna kodi na inatumika vip
 
Umeongea sahihi
kabisa,hembu ona walimu wanakatwa mishahara eti wajenge maabara,jee
kikwete na baraza lake la mawaziri watakatwa hizo pesa pia?Wanajua
waalimu ni dhaifu waoga ndio maana wanawachezea hivyo!Ingekua nchi
zilizoendelea rais angekua hana kazi muda huu

weee! walm wanachangia kama wazalendo wengne syo wanakatwa, acha upuuz!
 
Back
Top Bottom