Tusipokubaliana na mtazamo wa Godbless Lema, CCM itaendelea kutawala na katiba ya Sitta itapita


Unajua kufanya kz ya ualimu hapa Tz unatakiwa sehemu ya Ubongo wako ama iwe domanti au imekufa vinginevyo utapata shida sana.

Tujiulize mbona zahanati na hspl zinapojengwa hatusikii kama madaktari wanakatwa kuchangia, au au uwanja wa ndege, Barbara tukasia kuwa wafanyakazi Katuka idara hz wanakatwa mshahara kuchangia?

Kama ningekuwa mwalimu hata shilingi Moja tu kukatwa kwa Maelezo ya kiwendawazimu kama haya ilikuwatosha kuacha kz
 
pasco nyamaza kimya huijui arusha, umeitaja unga ltd hiyo kata ipo ccm arusha tunataka vitendo sio maneno. maneno yenu uongo hatuyataki siipendi ccm siipendi chadema
Mkuu , sio tuu naijua Arusha, bali nimeishi Arusha, nimesoma Arusha, na kampeni za Lema, nimehudhuria!

Naomba nikukumbushe hapa
Pasco
 
Pasco

We jamaa mnafiki sana wewe!Ulikuwepo Arusha ipi wakati wa uchaguzi?
Unawajua waliosimamia matokeo halisi ya uchaguzi yatangazwe pale kwa mkuu wa mkoa?
Arusha hawaishi kwa kutegemea bahasha..mburula nyie.

Kwa taarifa yako maandamano hujumuisha watalii vile vile...

Arusha ni nyumba ya upinzani toka enzi na enzi.Kaa huko huko bongo uendelee kuishi kwa vibahasha Arusha huijui!!!
 
Last edited by a moderator:
Pasco

We jamaa mnafiki sana wewe!Ulikuwepo Arusha ipi wakati wa uchaguzi?
Unawajua waliosimamia matokeo halisi ya uchaguzi yatangazwe pale kwa mkuu wa mkoa?
Arusha hawaishi kwa kutegemea bahasha..mburula nyie.

Kwa taarifa yako maandamano hujumuisha watalii vile vile...

Arusha ni nyumba ya upinzani toka enzi na q.Kaa huko huko bongo uendelee kuishi kwa vibahasha Arusha huijui!!!
 
Last edited by a moderator:
Sawa pasco ila wewe unaonaje mwalimu kuambiwa achangie maabara ni saw a hiyo?mbona sijasikia mjeshi aambiwe kujinunulia kombati kwasababu anavaa mwenyewe na analichakaza mwenyewe,daktali achangie kununua vifaa vya hospital?hapo ndo utaona upole wa mtanzania.Leo nimeona mwigulu anajisifu kachangiwa hela ya fomu ya uraisi kwanini asitumie fursa hiyo kufanya harambee ya kitaifa juu ya Ujenzi wa maabara kuna watanzania watachangia vizuri zaidi ya mwalimu anayeonewa
 
Ili CCM itoke madarakani, CHADEMA jifunzeni kwanza kutoogopa wale jamaa wa FFU.
 
Pasco
Acha kuhadaa watu Pasco unataka kituamhia hapa Lema asinge hamasisha watu kulinda kura kwa nguvu zote nakuwapa ujasiri angepita kuwa mmbunge? tuliona kilichotokea shinyanga mjini kwa Marehemu Shirumbishela alishinda uchaguzi tatizo uwoga wa Raia kura zikaongezwa kama Sita vile bungeni ha ha haaaaaa!Pasco bana!leo umecheka analysisi yako.
 
Last edited by a moderator:
Jackbauer
Mkuu Jakibawa, asante kwa hili, nilikuwa Arusha ipi mbona nimeeleza!, tena ushukuru sana sijayaelezea yaliyotokea Impala wakati wa Kampeni!. Kuhudhuria mikutano ya kampeni hakuna uhusiano wowotw na kuwajua waliosimamia uchaguzi, nimesema nilihudhuria kampeni na sio kuhudhuria uchaguzi!.

Hilo la bahasha, Arusha ndio mwake mwake!, na kwa taarifa kila nikitia timu Arusha siku hizi, huja kuzimwaga hizo bahasha, kuanzia tarehe 20-26 nitakuwa hapo Naura, kuja kuzigawa bahasha nene za nguvu!. Afadhali ya Dar, hata bila bahasha mambo yanakwenda!, kwa Arusha bila bahasha!, hakiendi kitu!.

Pasco wa jf ni Arachuga kwa sana tuu!.

Pasco.
 
Last edited by a moderator:
WILLAFRICA Pasco: Umeteleza kiufikiri kijana jipange upya.

Mara nyingi Pasco hujipambanua kama mwanafikra ila nadhani partiality inamnyina kuwa pragmatic and objective thinker.
 
Pasco

Kusoma post zako niburudani unapima upepo tulisha jua janja yako wewe palilia ugali wako Lowassa akiwa Rais utakuwa Mkuu wa mkoa Arusha lazima uje si nyumbani kwa Lowassa eti kwenu!!
 
Last edited by a moderator:
Mikael P Aweda

Mtu yeyote mwenye Maono na Hekima nilazima atafakari Jambo lolote kabla yakutenda! matokeo yake kwa jamii katika mitazamo yote miwili hasi na chanya.Pengine sijamwelewa mleta mada Mana lema hatumii maarifa au akili badala yake ni nguvu ya mwili "Mfano maandamano kwa watu ili maswahiba wake wafanye maasi yakuiba mali za watu,wengine wafe ili tu yeye apate umaarufu na neema kwa familia yake"Tofauti na hapo anatumia nguvu na sio akili na ndipo watu wakaliba yake au namna yake huona ndio akili halisi.Hata hivyo hakuna mwovu aliye mwoga.Pole mleta mada ni mawazo yako ila umefikiria kidogoooo! Think BIG
 
Last edited by a moderator:
Pasco

Ni kweli ila hapo unajaribu kucheza na maneno kwani naona kabisa unalazimisha hoja yako. Unaposema Lema ni kiazi nikueleweje wakati kabla hajaingia madarakani waliokuwepo ni wabunge wa ccm. Kama kweli maendeleo yalikuwepo ilikuwaje mapato ya halmashauri yawe machache? Unapozungumzia uwezo ni upi labda ni wa kutoa pesa zake mfuko ajenge mabarabara, mahosptal, au awagaie makanisa ili apate uungwaji mkono ama wa darasani? Kama ni hivyo mbona kwenye katiba hii, japo naona hata wewe unajua kabisa ni ushindi wa mezani wameweka kipengele cha mtu kujua tu kusoma na kuandika ambavyo Lema anavyo muda mrefu tu.Kama kweli Lema ni kiazi ni yupi basi bora yeye Lema anayewataka wananchi waandamane kwa amani dhidhi ya watawala kwa kuminya haki, ama ni hao watawala wasomi waliotuingiza kwenye hii mikataba ya kinyonyaji mpaka kufikia tunalipa umeme bei ya juu sana, na unaweza kukatika mara kwa mara na tusiweze kuhoji?

Nyinyi waandishi kwa sehemu kubwa ndio tatizo la nchi hii, huwa nakuangalia unayemtetea hapa nachoka kabisa. Sikatai ndio demokrasia lakini kumbuka ni vizuri ukawa upande sahihi na sio kumshabikia ambaye kwenye jamii amechafuka. Nadhani hiki kinachoendelea huku mitandaoni dhidi yenu toka kwa akina Chabruma kinadhibitisha hilo. Ni nani anayetaka Tz ijayo kuuongozwa na watoa rushwa? Kwanini nyinyi kama waandishi wa habari wangalau mkikutano huko msiweke utaratibu wa kuita think tank wa nchi hii ili waendeshe mijadala ya wazi, watoe mawazo ya kuendeleza nchi na kutoa utambuzi kwa umma juu ya viongozi wazuri na sio watoa rushwa? Au ndugu yangu wewe hukuwa unaona kinyaa watu kukata mauno siku ile bungeni watu wakishangilia ushindi wa mezani kwa rasimu ya hila itakayoendeleza tatizo letu la msingi la uongozi mbovu? Au wewe unaamini kwamba wakulima, wafugaji, nyinyi waandishi wa habari mtapa haki zenu toka kwenye katiba ijayo kwa viongozi walioamua kujitengezea katiba ya kuwafanya mungu watu? Pasco una watu tunaokuheshimu na tutaendelea kukuheshimu japo tatakupuuza kuwa sehemu ya kushabikia viongozi wenye doa. Au na wewe ndugu yetu umekulia kwenye hiki kizazi cha propaganda za amani, wakati wanaosema mjali amani wanaficha mikataba, wanachakachua kura, wanatumia dola kubaki madarakani lakini sio uwezo wa hoja na mawazo chanya ila kuongoza kwa mazoea baada ya kukamata mrija katika shamba la bibi?
 
Last edited by a moderator:

Ajabu unaweza kukuta hata hao watu wanaojifanya wamemchangia Mwigulu ni yeye mwenyewe kawapa hela.
 
Ajabu unaweza kukuta hata hao watu wanaojifanya wamemchangia Mwigulu ni yeye mwenyewe kawapa hela.
Ni kweli unachosema ila concept ya kuchangisha ingewekwa katika mambo ya maendeleo ningekubali zaidi,mfano mwigulu angefanya harambee jimboni kwawadau wa maendeleo kumchangia maabara badala kumminya mtumishi
 
Arusha inahitaji kutumia busara kuhakikisha Lema haendelei kuwa Mbunge, wakiendekeza matakwa ya "machalii" Mji utaendelea kudorora kama tuonavyo sasa, Lema hana akili ya ziada...zaidi ya kusisitiza vijana "acheni uoga" hakuna mbinu mbadala alizowasaidia wajikomboe.

Amewatumia vijana kumpigania tofauti zake na Meya, leo hii waliokufa wameshasahaulika yeye na huyo Meya bado wanakula maisha.....mnawajaza vijana ujasiri wa kijinga kwa manufaa binafsi.

Kama serikali ya Uganda wangemdhibiti Kibwetere mapema asingefikia kuangamiza roho za watu kama vile.....Lema ni Kibwetere.
 
Pasco

Unapoongelea ukiazi wa baadhi ya wabunge wa CDM... kama waTz wangekuwa wanachagua watu kwa uwezo wao (kiuelewa na kitaaluma) nafikiri wabunge wengi wa chama tawala wasingekuwa wabunge leo hii, mf jah people, Kibajaj, etc.

Sidhani kama swala la kutokuwa kiazi ni factor kubwa kwenye kuchaguliwa kwa nchi hii. Ingekuwa hivyo tusingeshuhusia mipasho na vitorondo vikichezwa kwenye bunge letu, tungeshuhudia watu wakitofautiana kwa hoja tu.
Arusha ni sehemu ambayo, hata kiazi kikiweje ilimradi ni cha CDM kina nafasi kubwa zaidi ya kupita vinginevyo CCM wachakachue kura, Chalinze ni sehemu ambayo hata kiazi kikiwaje ilimradi ni cha CCm kitapita tu hata kama upinzani ungekuwa madarakani
 
Last edited by a moderator:
tindo

Pasco ameamua kujivua ufahamu. japo kuna wakati anataka kuonyesha kwamba yeye hayupo upande wowote ila ukisoma between the lines unaelewa anachokishabikia. Kilichobaki kwa sasa aachane na habari ya kujaribu kufanya critical analysis, aweke mambo hadharani tu
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…