Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Kabudi na Lukuvi wameshushwa cheo yaani "Demotion" period.
Sawa wazee Kabudi na Lukuvi wamepewa nafasi mpya Ikulu ya kuwa washauri wa raisi.
Lakini kwa Kabudi ni kwamba ameondolewa pale Wizara ya katiba na sheria ili kufanya marekebisho ya sheria zote ambazo alizisimamia ziliporekebishwa wakati raisi akiwa John Magufuli.
Hii inamaanisha kwamba shinikizo la kutoka nje ni kwamba Kabudi ni "hardliner" na "ally" wa zamani wa JPM hivyo ni lazima aondoke hapo ili sheria hizo ziweze kufanyiwa mabadiliko.
Lengo kuu likiwa ni sheria kama madini ambazo zimekuwa "complex" kwa sasa na zahitaji watu wa nje ya wizara kusaidia kuzitafsiri na kuzibadili na uwepo wa Kabudi itakuwa ni kikwazo.
Kwa Lukuvi jambo la msingi ni kumdhibiti kada huyu mkongwe na anaeaminika ndani ya CCM na njia pekee ni kumweka karibu na raisi Samia ili iwe rahisi kufahamu nyendo zake.
Umri wa Lukuvi, uzoefu, na umahiri wa kazi unampa faida zaidi endapo angeendelea kuwa waziri kule Ardhi ambako angekuwa huru zaidi khas katika kipindi hiki hadi uchaguzi wa 2025.
Mtu ambae hatakuwa na wasiwasi sana ni Profesa Kitila Mkumbo ambae ameonekana kuwa si tishio na aweza tu kuendelea na u-backbencher bungeni.
Ila kwa Lukuvi na Kabudi ni wazi kuwa hii ni kushushwa cheo yaani "demotion" na kukaa ofisini kusoma gazeti tokea asubuhi hadi wamaliza kazi.
Kutokana na uzoefu wa kuwa karibu na watu waloshushwa cheo lakini bado waonekana ni tishio, uingiapo ofisini saa mbili au tatu asubuhi, kwanza ni kupata kikombe cha chai, kisha kama kuna kabrasha lolote basi laweza kukuchukua hadi saa tano walisoma tu na kama kuna cha kushughulikia basi waongea na katibu muktasi na atashughulikia hiki na kile.
Tatizo ni pale uingiapo ofisini asubuhi na kukuta hamna kabrasha siku hiyo isipokuwa magazeti yote upendayo kuanzia Daily News, Guardian, na Citizen ambayo kwa Kabudi ni cha mtoto, kisha kama wapenda ya kiswahili Nipashe na Habari leo hayakosi.
Mchana saa saba watoka kwa ruhusa au kujulisha wapi waendaa kwa "lunch" na saa nane lazima urudi na ujulishe, ni hatari sana.
Hali ni hiyohiyo kwa mzee Lukuvi na hali hii huweza kukufanya kukumbuka mambo mengi sana mazuri ambayo huenda wayakosa kwa kuendelea kuwepo hapo ofisini.
Wazee wengi ambao nimewahi kuwaona wengine waliishia kuacha kazi kwa kuchanganyikiwa na wengine kuanza hadi kutembea tu mabarabarani na kuishia kumaliza soli za viatu.
Lakini kwa Mzee Kabudi ni kheri akafikiria kuomba kurudi UDSM ili aendelee na kazi yake ya uhadhiri ambayo angalau itampa ukurasa mpya wa maisha nje ya baraza la mawaziri.
Kwa kuwa mzee Lukuvi ni "too late" kurudi kuwa mwalimu lakini aweza kuomba tu kuendelea kuwa mbunge wa kawaida kama Profesa Mkumbo, isipokuwa kama analazimishwa kuwa msomaji magazeti Ikulu.
Ni aibu na udhalilishaji kwa mtu mzima kushushwa cheo halafu wapelekwa sehemu kusoma magazeti na kunywa chai.
Mimi ni mmoja wa watanzania ambao tunafuatilia kwa makini mambo ambayo yanaendelea nchini ambayo sasa yamekosa dhamana ya wananchi walo wengi na ambao wanashindwa kuelewa nini lengo kuu.