Tusipotoshane, ajira ina nafuu na uhakika zaidi kuliko kujiajiri

Kuna kujiajiri na kujiajiri kubangaiza maisha, means kujiajiri definition au maana yake sio kuuza duka tu.
Na watu wengi ndipo wanapojichanganya kwenye hiyo definition wakisikia neno "kujiajiri" ikiwemo wewe.

Mtu anayeuza duka anabangaiza maisha lakini bado amejiajiri.

CEO au mtu anayemiliki biashara kubwa au company kadhaa ambapo kwa mwezi anaingiza sio chini ya 100 to 200 million kama faida na anawalipa wafanyakazi wake mishahara ya laki mpaka million kadhaa na mwenyewe anajilipa million kadhaa. naye amejiajiri vilevile.
Au mfanya biashara wa kiwango cha kati ambaye anaingiza 3 to 5 million kwa mwezi naye amejiajiri vilevile.

So hapo wote wamejiajiri ila ukubwa wako wa mawazo na uwezo wako wa akili ndio utadetermine umejiajiri kivipi na hiyo ndio maana kuna course za uchumi na biashara (MBA) nk.. au hizi courses zisingekuwepo.

Pia ni ngumu kumkuta mtu aliyesoma akiuza duka (kubangaiza maisha) bali kama anafanya biashara basi ni something reliable au labda awe msomi uchwara.
Sababu kwa akili ya mtu aliyesoma akaelimika kuuza kaduka bado ni hatua ya chini sana kuweza kuwa something realiable bali lazima atataka kuboresha na kupanda juu zaidi kwenye chochote kile.

Na usidiscourage kujiajiri au kungekuwa hakuna sekta binafsi ambazo wao ndio watakuajiri ili wakulipe hizo million mbili.
Sababu Company binafsi zote zimeanzishwa na watu walio na uthubutu, sio waoga wa maisha na wenye akili ili watengeneze ajira nyingi zaidi kwa wengine. au kama kila mtu anakimbia moto then nani atazima moto?

Na usitegemee 2 million serikalini easily na kwa mwingine million mbili anaona ni pesa ya kawaida sana hivyo atataka kutafuta zaidi na zaidi na sio kustick kwenye one point then ukistaafu urudi tena chini. angalia wastaafu wanavyohangaika sasa hivi.
Na Fun fact hakuna tajiri yoyote duniani aliyeajiriwa pia kusema matajiri wanasomesha watoto wao ili waajiriwe sio kweli kabisa, labda tajiri mbadilisha mboga.
bali matajiri watasomesha watoto wao ili waje kuwarithisha na kuendeleza utajiri wao sasa tuone wewe uje kuwarithisha wanao hiyo ajira.


Kwangu mimi kuajiriwa ni uoga wa maisha considering sipendi kuwa chini ya kima yoyote hivyo nitapita njia zangu mwenyewe. and actually that's what a man supposed to be fearless, brave, strong physically and mentally. and not to be a scared little girl.

So hapo hakuna ambaye yuko sahihi zaidi ya mwingine bali kila mtu anakuwa na preference zake na sio universal truth.
Kikubwa kinachowatofautisha hao wawili ni ukubwa wa mawazo, ambitions na akili ya mtu husika.
 
Kinachomatter sio wangapi au kina nani wanafanya nini, kinachomatter ni wewe mwenyewe.
 

Huo ndio ukweli mtupu, ndio maana CCM walikuwa tayari kutoa roho za Watanzania wasio na hatia ili waendelee kuajiriwa na kututawala milele na kuwa na uhakika wa kujichotea pesa za serikali!
 
Unasema?! Hivi nyie watu mnaishi wapi? Tokeni ndani ya maboksi hayo. Mshahara wa 6m kila mwezi ni hela ya kubeza biashara? Be serious man! Nilitaka nipite kimya ila uzalendo umenishinda.
Hahahahahah mzee utakuwa unamiliki sheli 😅
 
kuajiriwa ni utumwa boss ana kuamusha saa kumi na moja asubuhi na mvua au baridi wai kazini yeye anakura tunda lake chumbani taratibu ana amka saa tatu anakufokea kwanini kazi umefanya vibaya matusi kama yote yaani mwajiri wako ana kwendesha wewe na familia yako yote mpaka maamuzi yenu kwenye familia yenu hamuwezi kuamua mpaka mumwambie yeye
 
Kinachomatter sio wangapi au kina nani wanafanya nini, kinachomatter ni wewe mwenyewe.
Kwangu binafsi kwa nchi yetu hii naona hakuna wa kumdharau mwenzie! Labda kwa first world countries ndiyo tunaweza sema kujiajiri ndiyo bora kuliko kuajiriwa kwa mifano!

Bongo kuna walioajiriwa na wanawazidi baadhi ya waliojiajiri na kuna waliojiajiri wanawazidi baadhi ya walioajiriwa! Na wengi waliojiajiri na wakafanikiwa walianza na kuajiriwa!
 
Una point , ila umeangalia sana upande mmoja.

Mifano uliyotoa iko sawa, ila pia ni kwa upande mmoja.

Naona pia hujui tofauti kati ya biashara na mjasiriamali.

Ni kweli kufanikiwa kama mfanyabiashara inahitaji hayo uliyosema.

Ila kufanikiwa kama mjasiriamali inahitaj zaid na zaid ya hayo, ila ukishafanikiwa unakuwa mtu mkubwa.

Ambao nina uhakika ww unawafanyia kazi hao (wajasiriamali/wafanyabiashara) unaowabeza.

Na kwa kukuelewesha zaidi.
Wewe ni mfanyakazi wa mjasiriamali/mfanyabiashara aliyefanikiwa.

Sasa naomba usidharau biashara au mjasiriamali yoyote. Ni mwanzo tu.

Na pia Kwasababu, kama hawez kukulipa ujira wewe basi anaweza mlipa ujira mtu mwingine (hata kama elfu 50). na ndio mzunguko wa maisha Papaa.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Upeo wako mdogo sana! Wewe jifariji tu utakapokuja kugundua kuwa ajira pia ni biashara utakuwa umechelewa sana na hauta recover forever!

Kwenye hiyo ajira yako biashara unayofanya ni kuuza muda wako na Uhuru wako!

Kwanza kwa leo milioni 2 kwa mwezi tena gross ni nini? Kuna watu wanaingiza hiyo pesa kwa siku au week kwenye biashara zao.

Ulipoanza shule ulikuwa unaamka saa 11 alfajiri kuwahi namba shule! Leo unakaa Gongolamboto bado unaamka saa 10 alfajiri kuwahi kibaruani kwa boss wako kwa kupewa milioni 2 gross kwa mwezi!

Hao wanaopata elfu 20 kwa siku wamejenga nyumba zao!

Wewe ukikatwa kodi na makato mengine unajidanganya eti napata net ya 1.5 milioni kwa mwezi! Siyo net hiyo, Wewe ni zuzu huelewi tu!
Ebu toa nauli ulizotumia kwa mwezi, chakula ulichokula kazini huko mchana na gharama zingine utajikuta una negative balance!
 
Hizi story ukiwaambia watu waliopo Vodacom,Tigo,TCC,mgodini,Bandari,nmb,nssf,wataona una kichaa!!kama kuwa mtumwa ndio unapata overtime zaidi ya milioni mbili kwa wiki!basi huo utumwa mzuri.
 
Mkuu mbona unaongelea mshahara wa mamilioni wakati kuna watu wanafanya kazi wanalipwa laki 1 na 30 tu
 
Hizi story ukiwaambia watu waliopo Vodacom,Tigo,TCC,mgodini,Bandari,nmb,nssf,wataona una kichaa!!kama kuwa mtumwa ndio unapata overtime zaidi ya milioni mbili kwa wiki!basi huo utumwa mzuri.
Hao washikaji wanatumbua hela....ni balaaa
 
Mkuu mbona mbaobgelea mshahara wa mamilioni wakati I na watu wanafanya kazi wanalipwa laki 1 na 30 tu
Mbona wengine wanaongelea faida za mamilioni na wakati kuna wafanyabiashara wanaingiza vilaki tu na ni wengi mno kuliko hao wanaoingiza mamilioni! Tunapolinganisha haya mambo tunatakiwa kuwagroup watu kwa kuangalia uwiano wa vitu kama kipato, umri, idadi, consistency, nk siyo tunalinganisha tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…