Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
kwamba wafungwe mdomo wakose uhuru wa kutoa maoni na mtazamo wao, right?Habari wanaBodi...
Nimekua mfatiliaji kidogo wa mijadala ya Bungeni hasa michango inayotolewa na wabunge mashuhuri wawili watatu hivi kuhusu Taifa na maendeleo yake Kiuchumi kisiasa na kiteknolojia.
Lengo la kuandika huu uzi sio kuwataja hao wabunge au kuwadhalilisha Bali ni kuwakosoa ili kujenga Taifa Bora Zaidi.
Mara zote katika michango yao, wabunge Hawa wawili wamekua wakipinga Sana ajenda ya usomi na wasomi wenyewe. Kwa haraka haraka wanaamini kabisa wasomi wetu ambao wapo katika sekta mbalimbali hakuna wanalolifanya kwa Kutumia elimu yao. Yaani kimsingi wanaamini mambo yataenda tu kienyeji bila elimu. Kifupi hawaamini kama elimu Ina msaada wowote katika kukuza chumi za nchi na ustawi wa Wananchi wake.
Hawa watu ukiwafatilia kiundani ni watu waliofanikiwa Kiuchumi kwa njia ambazo wao wanaamini hazikuhitaji elimu, sababu wao wameishia la Saba. Hivyo wanaamini mtu yoyote sio lazima asome ili afanikiwe, kisa tu wao hawajasoma na wametoboa.
Tusipowadhibiti au kupinga hizi kauli zao za kibaguzi dhidi ya wasomi wetu, yamkini watoto au wajukuu zetu huko mbeleni wakipata hizi Hansard hawataona umuhimu wa kusoma, wataamini kama huyu "Joshua" alitoboa(ga) bila kusoma basi kumbe Kuna short cut ya Maisha inawezekana.
TUWAKEMEE MARA MOJA.
Nawasilisha.
kwamba hicho ndicho wanachostahili kufanyiwa, baada ya kuwasema ukweli kwamba wasomi kulalamika hawana ajira na wana madigrii mbalimbali ni aibu, na wale wa darasa la saba kule vijijini ndio wameshikilia chumi za vijijini na kata, kwamba wasiseme ukweli huo right?