Tusipowakemea hawa wabunge wanaobeza elimu yetu na wasomi wetu, tutazalisha Taifa la hovyo kabisa

Habari wanaBodi...

Nimekua mfatiliaji kidogo wa mijadala ya Bungeni hasa michango inayotolewa na wabunge mashuhuri wawili watatu hivi kuhusu Taifa na maendeleo yake Kiuchumi kisiasa na kiteknolojia.

Lengo la kuandika huu uzi sio kuwataja hao wabunge au kuwadhalilisha Bali ni kuwakosoa ili kujenga Taifa Bora Zaidi.

Mara zote katika michango yao, wabunge Hawa wawili wamekua wakipinga Sana ajenda ya usomi na wasomi wenyewe. Kwa haraka haraka wanaamini kabisa wasomi wetu ambao wapo katika sekta mbalimbali hakuna wanalolifanya kwa Kutumia elimu yao. Yaani kimsingi wanaamini mambo yataenda tu kienyeji bila elimu. Kifupi hawaamini kama elimu Ina msaada wowote katika kukuza chumi za nchi na ustawi wa Wananchi wake.

Hawa watu ukiwafatilia kiundani ni watu waliofanikiwa Kiuchumi kwa njia ambazo wao wanaamini hazikuhitaji elimu, sababu wao wameishia la Saba. Hivyo wanaamini mtu yoyote sio lazima asome ili afanikiwe, kisa tu wao hawajasoma na wametoboa.

Tusipowadhibiti au kupinga hizi kauli zao za kibaguzi dhidi ya wasomi wetu, yamkini watoto au wajukuu zetu huko mbeleni wakipata hizi Hansard hawataona umuhimu wa kusoma, wataamini kama huyu "Joshua" alitoboa(ga) bila kusoma basi kumbe Kuna short cut ya Maisha inawezekana.

TUWAKEMEE MARA MOJA.

Nawasilisha.
kwamba wafungwe mdomo wakose uhuru wa kutoa maoni na mtazamo wao, right?

kwamba hicho ndicho wanachostahili kufanyiwa, baada ya kuwasema ukweli kwamba wasomi kulalamika hawana ajira na wana madigrii mbalimbali ni aibu, na wale wa darasa la saba kule vijijini ndio wameshikilia chumi za vijijini na kata, kwamba wasiseme ukweli huo right?
 
Hili sasa ni tatizo la mfumo sio la wasomi mmoja mmoja. Badala ya kuwafanyia bullying wasomi kama anavyofanya Msukuma bungeni tupige kelele mfumo ufanyiwe mageuzi otherwise mfumo utatuzalishia wasomi hawa hawa tu tulionao.
Tatizo ni la mfumo kweli ila pia linachagizwa na hao hao wasomi ndo maana msukuma anapofanya bullying huwa namuelewa!
Kama profesa alithubutu kusema kaokotwa jalalani akimaanisha Usdm, hapo tatizo ni mfumo au wasomi wenyewe?
 
Habari wanaBodi...

Nimekua mfatiliaji kidogo wa mijadala ya Bungeni hasa michango inayotolewa na wabunge mashuhuri wawili watatu hivi kuhusu Taifa na maendeleo yake Kiuchumi kisiasa na kiteknolojia.

Lengo la kuandika huu uzi sio kuwataja hao wabunge au kuwadhalilisha Bali ni kuwakosoa ili kujenga Taifa Bora Zaidi.

Mara zote katika michango yao, wabunge Hawa wawili wamekua wakipinga Sana ajenda ya usomi na wasomi wenyewe. Kwa haraka haraka wanaamini kabisa wasomi wetu ambao wapo katika sekta mbalimbali hakuna wanalolifanya kwa Kutumia elimu yao. Yaani kimsingi wanaamini mambo yataenda tu kienyeji bila elimu. Kifupi hawaamini kama elimu Ina msaada wowote katika kukuza chumi za nchi na ustawi wa Wananchi wake.

Hawa watu ukiwafatilia kiundani ni watu waliofanikiwa Kiuchumi kwa njia ambazo wao wanaamini hazikuhitaji elimu, sababu wao wameishia la Saba. Hivyo wanaamini mtu yoyote sio lazima asome ili afanikiwe, kisa tu wao hawajasoma na wametoboa.

Tusipowadhibiti au kupinga hizi kauli zao za kibaguzi dhidi ya wasomi wetu, yamkini watoto au wajukuu zetu huko mbeleni wakipata hizi Hansard hawataona umuhimu wa kusoma, wataamini kama huyu "Joshua" alitoboa(ga) bila kusoma basi kumbe Kuna short cut ya Maisha inawezekana.

TUWAKEMEE MARA MOJA.

Nawasilisha.
Wabunge hao wana kila sababu ya kuwatukana wasomi uchwara wa nchi hii, ukiwemo na wewe uliandika uzi huu! na mimi nasema watukanwe tu mpaka pale akili zitakapowakaa sawa maana hamna namna nyingine! mfano wewe kilichochokushinda kutaja majina ya hao wabunge tuseme ni uoga au ndio ukanjanja wenyewe wa wasomi wetu. bila majina ya wahusika, hiki ulichoandika ni majungu na umbea dhidi ya waheshimiwa wawakilishi wetu.
 
Mkuu kwa hiyo form six na Darasa la Saba Wana upeo wa kufanana?
Unazungumzia upeo ? Form six anaelimu gani zaidi ya kukalilishwa theory afaulu mitihani elimu ya mtaani ni kubwa kuliko hiyo mnayopew huko shuleni huwezi kumfananisha graduate yupo mtaani miaka nane anasubiri ajira na kijana wa darasa la saba ambaye yupo na fremu ya biashara na mtaji wa mil 50-100 na ametoa na ajira
 
Nakunaliana na hoja yako, haiwezekani wasomi wote wakadeliver sawa.... Watakaofeli, basi ni kuwaadress hao particularly.... Lakini Hawa jamaa wanaponda wasomi kiujumla.... Hiyo ndio hoja yangu... Na angalia nilivyomalizia mwishoni
Anza kumpa ukweli yule Muhadhiri mwandamizi aliyedai UDSM ni jalalani.
Msomi wa kiwango chake anaongea utopolo hadharani wasomi wote mlikaa kimya.
Huyu profesa wa jalalani na mwenzake profesa Mchembe waliwaongoza watanzania kutumia mitishamba wakati janga serious la Corona kwa nia ya kumfurahisha aliyewateua.
Wasomi wa aina hiyo ni kituko, kama hawata jirekebisha watapuuzwa tu.
 
Acha ukweli usemwe. Inakuwaje mtu Anakuwa professor Hana Tija Kwa Taifa

Hata kingereza Hajui.

Mfano Ndalichako waziri...Alifanya nini Kwenye Taifa hili kama waziri wa Elimu

Wako wengi tu. Hawana impact Kwa jamii
Kwa kuwa hawana impact ndiyo tudharau elimu?
 
Tatizo kubwa linalokabili taifa letu hili ni impactfulness ya elimu kutoonekana kwa miaka ya hivi karibuni.

Zamani kulikuwa na equilibrium kwa kiasi flani baina ya wasiosoma na waliosoma ila wepesi wa maisha ulikuwa zaidi kwa waliokwenda shule maana fursa zao zilikuwa wazi nikimaanisha soko la ajira.

Ilikuwa ni rahisi mtu kubadilisha maisha ya familia masikini aliyetokea. Mfano kwetu tu mzee wangu utotoni walikuwa wakiishi maisha duni wazazi ni wakulima walilala kwenye nyumba ya udongo ila baada ya kumaliza shule tu alichukuliwa na serikali na kula shavu dodo chap akawajengea wazazi nyumba za tofali ya baba na mama yake. Somesha wadogo zake kibao tu. Elimu yake ilikuwa na tija kubwa tu sababu ilikuwa baada ya shule tu unapata ajira nzuri na kulipwa fedha ya kutosha kubadili maisha haraka na kuhodhi mali.

Sasa leo hii hali imekuwa kinyume na tafsiri ya mafanikio ni kumiliki mali na fedha regardless una elimu au hauna. Wasomi wengi waliohitimu ngazi za juu za elimu hawana mali wala fedha ila wale ambao hawakufuata mfumo wa shule wengi wana mali na fedha tayari wakati aliyehitimu hana kazi na hata akipata ni ya kipato duni.
 
Habari wanaBodi...

Nimekua mfatiliaji kidogo wa mijadala ya Bungeni hasa michango inayotolewa na wabunge mashuhuri wawili watatu hivi kuhusu Taifa na maendeleo yake Kiuchumi kisiasa na kiteknolojia.

Lengo la kuandika huu uzi sio kuwataja hao wabunge au kuwadhalilisha Bali ni kuwakosoa ili kujenga Taifa Bora Zaidi.

Mara zote katika michango yao, wabunge Hawa wawili wamekua wakipinga Sana ajenda ya usomi na wasomi wenyewe. Kwa haraka haraka wanaamini kabisa wasomi wetu ambao wapo katika sekta mbalimbali hakuna wanalolifanya kwa Kutumia elimu yao. Yaani kimsingi wanaamini mambo yataenda tu kienyeji bila elimu. Kifupi hawaamini kama elimu Ina msaada wowote katika kukuza chumi za nchi na ustawi wa Wananchi wake.

Hawa watu ukiwafatilia kiundani ni watu waliofanikiwa Kiuchumi kwa njia ambazo wao wanaamini hazikuhitaji elimu, sababu wao wameishia la Saba. Hivyo wanaamini mtu yoyote sio lazima asome ili afanikiwe, kisa tu wao hawajasoma na wametoboa.

Tusipowadhibiti au kupinga hizi kauli zao za kibaguzi dhidi ya wasomi wetu, yamkini watoto au wajukuu zetu huko mbeleni wakipata hizi Hansard hawataona umuhimu wa kusoma, wataamini kama huyu "Joshua" alitoboa(ga) bila kusoma basi kumbe Kuna short cut ya Maisha inawezekana.

TUWAKEMEE MARA MOJA.

Nawasilisha.
Kwanza kabisa, ili tuwe pamoja, elimu ni nini?
 
Tafsiri ya Elimu ni pana sana.

Shida sio wasomi wa Tanzania bali shida ni mfumo mbovu wa elimu unaozalisha wahitimu fake, HILI WOTE TUNAPASWA KULIPIGIA KELELE MAANA ELIMU BORA NDIO KITU PEKEE KINACHOWEZA KUTULETEA MAGEUZI YA KIUCHUMI NA KISIASA.

Elimu ndio imeleta mageuzi maeneo mengi duniani hapa, hivyo shida sio Elimu Bali shida ni mfumo mbovu wa elimu unaotoa wahitimu fake.
 
Kuanzia zama za magufuli wasomi wamedhalaulika sana, ukosefu wa ajira na mambo waliyokua wanayafanya wanasiasa wasomi mfano Pro. Kabudi imesababisha wasomi wote waonekana hamnazo.
Sasa hata sasa kuna unafuu gani?! Kama ajira zilizopo au zinazozalishwa na wawekezaji wenu wa ki Asian mishahara ni ya laki 3 utafanya maendeleo gani kumzidi hustler std 7?

Kiuhalisia tu mtu ni la saba ila toka mmeachana shule 15 years ago kakomaa na kujijenga na biashara mnakutana yeye anasukuma VX-R wewe na Masters yako upo kwa bolt bodaboda utakuwa na hoja gani ya msingi ya kutetea usomi wako?

Mkikaa sehemu ya kupata ikija bill ni zaidi ya mshahara wako mwenzio anagusa Lipa namba tu bila kupepesa macho.

Umasikini unaumiza sana na uko evident zaidi kwa wahitimu hata ukijificha kwenye kichaka cha PhD na ndio maana watumishi wengi wa umma wa sasa ni wezi na wakiiba mabilioni wanakimbilia kuwekeza kwenye biashara za hao hao std 7.
 
Habari wanaBodi...

Nimekua mfatiliaji kidogo wa mijadala ya Bungeni hasa michango inayotolewa na wabunge mashuhuri wawili watatu hivi kuhusu Taifa na maendeleo yake Kiuchumi kisiasa na kiteknolojia.

Lengo la kuandika huu uzi sio kuwataja hao wabunge au kuwadhalilisha Bali ni kuwakosoa ili kujenga Taifa Bora Zaidi.

Mara zote katika michango yao, wabunge Hawa wawili wamekua wakipinga Sana ajenda ya usomi na wasomi wenyewe. Kwa haraka haraka wanaamini kabisa wasomi wetu ambao wapo katika sekta mbalimbali hakuna wanalolifanya kwa Kutumia elimu yao. Yaani kimsingi wanaamini mambo yataenda tu kienyeji bila elimu. Kifupi hawaamini kama elimu Ina msaada wowote katika kukuza chumi za nchi na ustawi wa Wananchi wake.

Hawa watu ukiwafatilia kiundani ni watu waliofanikiwa Kiuchumi kwa njia ambazo wao wanaamini hazikuhitaji elimu, sababu wao wameishia la Saba. Hivyo wanaamini mtu yoyote sio lazima asome ili afanikiwe, kisa tu wao hawajasoma na wametoboa.

Tusipowadhibiti au kupinga hizi kauli zao za kibaguzi dhidi ya wasomi wetu, yamkini watoto au wajukuu zetu huko mbeleni wakipata hizi Hansard hawataona umuhimu wa kusoma, wataamini kama huyu "Joshua" alitoboa(ga) bila kusoma basi kumbe Kuna short cut ya Maisha inawezekana.

TUWAKEMEE MARA MOJA.

Nawasilisha.
Nakubaliana na Kishimba.

Tuwafundishe watoto kuhusu wealth generation mapema na utaftaji wa fedha. Watakuwa wakijua dhamira yao kuwa duniani hapa maisha ni fedha hivyo matumizi ya muda ni muhimu sana katika uzalishaji mali.

Sio kukazania usomi usio na tija maana hatuna shule za kuzalisha wasomi wa aina hio hapa nchini na kama zipo huenda hata hazifiki 1% ya shule zote. Mtoto aliyeishia form 4 mwenye mafanikio ya kiuchumi na umiliki wa mali anaheshimiwa sana kuliko PhD holder ambaye ni jobless anayetambia usomi na cheti cha chuo kikuu.
 
Kila mtu ana elimu tunatofautiana viwango tu, impact ya elimu inaweza isionekane kwasababu mbalimbali mf. Mtaji, mfumo wa uongozi, sheria, mazingira nk
Elimu ni baadhi bidhaa yenye gharama na thamani kubwa kutokana na umuhimu wake.
Baadhi ya wasomi hutumia elimu kuendana na matakwa ya watawala.
 
Tafsiri ya Elimu ni pana sana.

Shida sio wasomi wa Tanzania bali shida ni mfumo mbovu wa elimu unaozalisha wahitimu fake, HILI WOTE TUNAPASWA KULIPIGIA KELELE MAANA ELIMU BORA NDIO KITU PEKEE KINACHOWEZA KUTULETEA MAGEUZI YA KIUCHUMI NA KISIASA.

Elimu ndio imeleta mageuzi maeneo mengi duniani hapa, hivyo shida sio Elimu Bali shida ni mfumo mbovu wa elimu unaotoa wahitimu fake.
Waliotengeneza na wanaotengeza mifumo ya elimu ni akina Profesa Ndalichako, Profesa Mkenda, Dr Msonde nk.
Hutawakuta akini Kishimba huko.
Hivyo mabingwa wenye taaluma zao ndiyo waotukwamisha.
Lawama zote wanazopewa ni haki yso.
 
Habari wanaBodi...

Nimekua mfatiliaji kidogo wa mijadala ya Bungeni hasa michango inayotolewa na wabunge mashuhuri wawili watatu hivi kuhusu Taifa na maendeleo yake Kiuchumi kisiasa na kiteknolojia.

Lengo la kuandika huu uzi sio kuwataja hao wabunge au kuwadhalilisha Bali ni kuwakosoa ili kujenga Taifa Bora Zaidi.

Mara zote katika michango yao, wabunge Hawa wawili wamekua wakipinga Sana ajenda ya usomi na wasomi wenyewe. Kwa haraka haraka wanaamini kabisa wasomi wetu ambao wapo katika sekta mbalimbali hakuna wanalolifanya kwa Kutumia elimu yao. Yaani kimsingi wanaamini mambo yataenda tu kienyeji bila elimu. Kifupi hawaamini kama elimu Ina msaada wowote katika kukuza chumi za nchi na ustawi wa Wananchi wake.

Hawa watu ukiwafatilia kiundani ni watu waliofanikiwa Kiuchumi kwa njia ambazo wao wanaamini hazikuhitaji elimu, sababu wao wameishia la Saba. Hivyo wanaamini mtu yoyote sio lazima asome ili afanikiwe, kisa tu wao hawajasoma na wametoboa.

Tusipowadhibiti au kupinga hizi kauli zao za kibaguzi dhidi ya wasomi wetu, yamkini watoto au wajukuu zetu huko mbeleni wakipata hizi Hansard hawataona umuhimu wa kusoma, wataamini kama huyu "Joshua" alitoboa(ga) bila kusoma basi kumbe Kuna short cut ya Maisha inawezekana.

TUWAKEMEE MARA MOJA.

Nawasilisha.
Huko bungeni kumejaa Hao "wasomi" Na, PHD zao! Spika ni msomi, tena Dokta! Hawapo serious bro, pale bungeni watu wanafanya maigizo na vituko tu! Kule kumejaa akili za kina baba levo na mwijaku!
 
Acha ukweli usemwe. Inakuwaje mtu Anakuwa professor Hana Tija Kwa Taifa

Hata kingereza Hajui.

Mfano Ndalichako waziri...Alifanya nini Kwenye Taifa hili kama waziri wa Elimu

Wako wengi tu. Hawana impact Kwa jamii
Ona huyu kenge sasa mtu hadi anakuwa professor unajua anatakiwa afanye nini ili aupate huo uprof au unajua wanapewa km zawadi tu..

Acha kuropoka mambo usiyoyajua.
 
Back
Top Bottom