sahivi na ignore tu, bora lawama halafu kitu kingine nilichokuja gundua watu hawajui kuwa sio wao pekee wanaoomba michango hiyo. Mwingine unamwambia saivi nimebanwa sitoweza shiriki lakini nakuuna mkono kwa hichi kidogo anaona kama unamkataa kumbe sio. Mwezi huu ofisini nimechangia hela kwa ajili ya sherehe ya kustaafu mtumishi mwenzetu, wiki iliyopita binamu yangu mwanae anamaliza darasa la 7 nikaona isiwe kesi nikatuma hela, ofisini kuna wadada wa 4 wanaolewa mwezi wa 10 na wa 11, mmojawao hapo npo nae kitengo/ofisi moja hivyo hata sapoti kwake inakuwa kubwa, kuna mtumishi mwenzngu mwingine yupo makao makuu naye anaoa, kuna dada nimesoma nae primary nimemchangia leo, kuna kaka nimesoma nae advance jana kanikumbushia mchango wake , kuna dada nilisoma nae chuo naye anataka mchango wa ndoa yake pamoja na zawadi kama darasa. Juzi mpwa wangu mwanae anamaliza la 7 , kanipa taarifa sijataka hata kumjibu.Hao wote jumla wanafika 10 au 9, michango yao ni 100k au 70k , hamna hamna hapo nikisema nishiriki kote 700k lazima initoke .
Bado kuna misiba kama miwili ya staff&schoolmate kufiwa na wazazi nimechanga
Bado kuna wale wanaojipost wame engage naogopa hata kuwapa hongera nisije ombwa mchango