Darasani kwa Dr
Yahya Msangi
Notice: jifanye yako ule block fasta
BANDARI YA BAGAMOYO HAIFAI HATA IKITIWA TUI LA NAZI NA KINA "MADE IN CHINA"
Awali ya yote nimshukuru Allah kwa kuniponya maradhi na kuniwezesha kufunga mwezi mtukufu. Niwashukuru wote mlioniombea.
Wakati nikiwa naumwa nilijitahidi kupitia hoja mitandaoni kila nilipoweza. Haswa za kuhusu report ya CAG na Bandari ya Bagamoyo. Léo nitajikita kwenye bandari kwa kuwa ni suala linaonyesha ni jinsi gani baadhi ya viongozi wetu walivyo wanafiki kwa kuwa wamepigwa mhuri mgongoni wa "MADE IN CHINA"!
Kabla ya kueleza ni kwa nini bandari ya Bagamoyo haifai hata ikipuliziwa pafyumu na kina Lusinde na wenzake waliosimama kumtetea spika eti watu "hawakumuelewa" nianze kwa kuwakumbusha (mnaosahau haraka) mauzauza ya hii bandari.
Uzauza namba 1:
Ndugai alitoa taarifa bungeni mara tu alipofanya ziara na ujumbe wake (ingefaa muwajue waliokuwa msafara wa Ndugai Kabla hamjawasifu). Katika taarifa île pale bungeni (Kabla Magufuli hajaeleza masharti ya hovyo ndani ya mkataba) Ndugai alitamka kuwa walikutana kwa bahati mbaya na viongozi wa China...! Fikiria mwenyewe hivi: Spika wetu na ujumbe wake walikutana kwa 'bahati mbaya' na viongozi wa taasisi iliyotupa masharti ya kihayawani? Spika alidai ilikuwa bahati mbaya kwa kuwa safari yao ilihusu mkutano wa kuanzisha utaratibu wa kidijitali (digitalization of parliament aka BUNGE DIGITAL).
Hivi inawezekanaje spika na ujumbe wake wakutane kwa 'bahati mbaya' na waliotoa masharti ya kuhujumu nchi? Spika alidai walifanyiwa presentation "nzuri mno"! Hivi hiyo presentation "nzuri mno" nayo iliandaliwa kwa bahati mbaya? Haikueleza masharti ya kuhujumu nchi? Spika na ujumbe wake hawakupewa nakala ya mkataba? Pale bungeni spika alisherehesha hoja yake kwa kudai katika kampuni inayotaka kutujengea bandari wamebaki wazee wachache mno wanaoipenda Tanzania! Éti tukubali haraka mradi kabla hawajafa au kustaafu! Spika akaendelea kusherehesha hoja yake kwa kudai wachina wanatucheka sana na wanaweza kwenda kuwekeza kwingine! Hakika ukishapigwa muhuri kama ng'ombe mnadani unaweza kutetea hoja yako kipumbavu mno!
Uzauza Namba 2:
Katika kujieleza na kupigia chapuo mradi wa wachina Spika hakujua anatupa habari nyingine ya kusikitisha na kustua. Kwa kuwa watanzania wengi sio wachambuzi hakuna aliyeona hatari iliyopo! Wachina ndio walijenga ukumbi wa Umoja wa Afrika (AU) na ndio walifunga vifaa vya digital pale Addis Ababa. Siku moja kwa bahati mbaya usiku wa manane mtaalam mmoja mzalendo akahisi kuna mawasiliano yanaendelea ! Katika kuchunguza akakuta ni mawasiliano kati ya wataalamu wa kichina na wenzao walioko China! Ndipo uchunguzi ulipofanyika ikagundulika wachina walikuwa wananasa mawasiliano na taarifa zoote ya AU! Ikumbukwe mawasiliano mengine ni siri n'a yanahusisha wakuu wa Nchi! Kashfa hii inafahamika vizuri na nchi zote na hâta Tanzania ! Sasa Spika WETU alienda China kuonyesha digitalization ya bunge letu! Kuna kinachozungumzwa au kujadiliwa bungeni kwetu mchina asijue?Je hawa wanaotetea mradi wa mchina sio kwamba wanajua aliyewapiga mhuri mgongoni anawasikiliza?
Uzauza namba 3:
Nilimsikiliza Spika akirejea hoja yake baada ya kifo cha Magufuli. Spika hakusema chochote kuhusu kurekebisha masharti! Hawa kina Kibajaji wanaodai watu hawakumuelewa Spika sio miongoni mwa waliopigwa mhuri mgongoni kwa bahati mbaya kule China? Au tu unafiki wao? Maana Magufuli alipoeleza ubaya wa masharti hatukumsikia Kibajaji na wenzie wakimwambia masharti yarekebishwe! Kibajaji ni mmoja wa aliyesifu hatua thabiti ya Magufuli kupinga bandari! Léo mnapataje Akili ya kumsifu msaliti sampuli hii? Kibajaji kacheza na akili za wasiofikiri! Kakemea kumdhalilisha Marehemu na hapohapo kamsaliti kwenye hoja ya bandari. Anayethamini kazi ya Magufuli hawezi kutetea bandari ya mchina! Hivi masharti aliyaweka Kibajaji au Spika? Sio wachina? Utasemaje yaondolewe wakati hukuyaweka wewe na tukikutizama una mhuri wa made in China mgongoni? Pindi Serikali itakapofungua majadiliano mapya na mchina uwezekano za kina MADE IN CHINA kuwasaidia wachina utakuwepo! Tutajikuta hatujadiliani na wachina peke yao! Nyuma yao kina MADE IN CHINA watakuwepo! Tutafungua kitu kwa kiingereza inaitwa "Pandora's Box"! Litatoka jini kwenye box! Serikali ikatae katakata kuanza majadiliano mapya. Hao wachina waende watakapo! Acha watucheke kwa kukataa wasituibie!
Uzauza Namba 4:
Mradi huu awali ulikuwa ufadhiliwe na hao wachina na Serikali ya Oman. Lakini kina MADE IN CHINA wetu hawatuambii ni kwa nini na lini Serikali ya Oman ilijitoa? Je Oman waliona huu utapeli? Waliondolewa? Watanzania wanapaswa kujua Oman ilijiondoa au iliondolewa? Kisa? Au humo ndani bado Oman Fund wamo?
Uzauza Namba 5:
Toka tupate uhuru sikuwahi kuona Spika sampuli hii! Spika ambaye ameonyesha waziwazi kuhalalisha marupurupu ya wanaompigia kura. Spika huyu ukimsikiliza wakati bunge linavunjwa au uchaguzi wa spika unafanyika utasikia akiwakumbusha wabunge namna anavyoboreshaga maslahi yao! Ni spika ambaye ANATAFUTA uspika kwa "kuwahonga" wapiga kura kwa ahadi za kuwaongezea maslahi. Huyu ni spika ambaye hachelei kutafuta fursa. Mfano ni juzi akitetea upya hoja ya Bandari. Alimaliza kwa kudai eti Serikali ijenge miundombinu halafu usafirishaji waachiwe hâta wabunge wawekeze! Akatolea mfano wa barabara. Serikali inajenga watu binafsi ndio wanafanya biashara. Hivi kwa nini asidai na serikali ijenge viwanja vya ndege, magereza, mashule, mabwawa, mahospitali n.k. halafu iwaache wabunge au raia wafanyie biashara? Kwa nini achague SGR? Tuna spika mwekezaji? Hivi bunge letu likawa ni la wawekezaji watupu tutasalimika? Hivi kwa tamaa anayoonyesha spika huyu mwaka 2025 au hâta 2030 hawezi kutia nia? Na kwa kuwa anaboresha maslahi ya wabunge wengi wakiwa wajumbe wa vikao hawezi kupita? Bandari haitajengwa? Nadhani ni wakati sasa wa kumtizama spika huyu kwa jicho kali!
Sasa baada ya haya mauzauza tujiulize hivi ni kweli tunahitaji bandari mpya? Kina MADE IN CHINA hawatuelezi kama tunahitaji bandari! Walau Magufuli alisema hatuihitaji kwa kuwa itaua bandari aliyoanzisha baba wa taifa. Hivi hili kina Lusinde hawakulisikia?
Ukweli ni kwamba hatuihitaji bandari mpya! Tizama wenye bandari eneo letu: Kenya, Msumbiji, South Africa na Namibia. Wana bandari ngapi? Walau Tanzania inazo Dar, Tanga na Mtwara. Zinatosha mnoo! Bahari ya Hindi sio njia kuu ya meli za mizigo au abiria. Kina Ndugai wanakosea kufananisha Singapore na Tanzania. Singapore iko eneo lenye njia kuu za Meli. Na hâta hivyo ina bandari moja yenye terminals kama 5 hivi! Ndugai ama haijui Singapore au anasherehesha hoja yake ya MADE IN CHINA!
Hakuna comparative advantage na majirani zetu wa Indian Ocean kwa kujenga bandari mpya. Tanzania inatakiwa iboreshe tu Bandari zake haswa kwa kujenga miundombinu kama alichofanya Magufuli. Ijenge SGR, barabara, bandari za Nchi kavu, iikarabati TAZARA, iongeze terminals n'a container handling equipment, n.k.
Bandari mpya tuwaachie kina MADE IN CHINA wabwabwaje wao na wachina wao. Kina Lusinde wajue watanzania sio wapumbavu. Wamemwelewa Spika na wamewaelewa mnaomtetea! Wamewaelewa wasaliti hâta wanaojifanya kumsifu marehemu!