Tusizuge wana Yanga SC wengi ( 99% ) hawana Furaha na Matokeo ya Marudiano leo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Wana Yanga SC wote walijaa hadi Pomoni kwa Mkapa wakijua kuwa kama Ugenini mlishinda Goli 2 basi leo kwa Mkapa Wanaijeria wangekufa / wangefungwa Goli nyingi kuanzia 3 kwenda mbele matokeo yake imeisha Suluhu ( 0 - 0 )

Najua mnashangilia Shingo upande tu huku mkiwa Wanafiki kwani matokeo mliyoyapata hamkuyatarajia kamwe na ndiyo maana Mashabiki wote wa Yanga SC waliokuwa Uwanjani wanamlaumu mno Kocha Mkuu wenu Nabi kwa Kubeti Kupanga Wachezaji wasio Wazoefu katika Mechi muhimu kama hii ya Leo tena ikichezewa Nyumbani nchini Tanzania.
 
Asante kwa taarifa!
 
Furaha mkiwa nayo nyie Wana Simba, inatosha.
Jibu la kikatili sana Apostle!

Baidhawee, sisi tulijua tumeshafuzu kuingia nusu fainali. Haikuwepo haja ya kutumia nguvu kubwa kuwachosha wachezaji. Everything was planned.

Naomba kukabidhi maiki kwa jamaa zetu waliokufa kiume. Hivi nani aliwaambia kifo kina jinsia?

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Esperance kashinda moja ugenini kufika kwake kalinda ushindi wa goli moja akadroo.Mamelod kashinda nne ugenini kufika kwake kalinda ushindi wake akapata ushindi mwembamba wa goli mbili moja.

Hao sio kwamba walishindwa kufunguka bali waliiona mechi washa zimaliza na walinde walichokuwa nacho na kuepusha majeruhi kwa wachezaji wao.
 
Acha mihemko,, mipango ya kocha huwezi kuielewa wewe. Kikosi Bado kina majukumu mengi, hakukuwa na haja wa kutumia nguvu kubwa mwisho watengeneze na injury zisizo za msingi. League Bado tuna michezo migumu ugenini ambayo yote ni muhimu sana, sasa ya nini kuchoka kwenye shughuli iliyokwishatamatika? Bado kuna michuano ya Azam.

kichwa panzi huwezi kuelewa
 
Ukifurahia wewe pompoma inatosha
 
Itakuwa Scars huyo
 
Na ndio jibu sahihi. Unaanzaje kuhamanika na udhuni ya majirani kama wewe unafuraha? πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Ila tuwapongeze,wametoka kiume
 
Bila shaka hasira za huyu mleta mada ni kuchaniwa mkeka [emoji28][emoji28][emoji28].

Muhimu kwa Yanga ilikua ni kucheza kwa kumuheshimu mpinzani, kulinda Ushindi, na kufuzu nusu fainali
 
Mkuu hii comment muwekee lamination halafu akabandike ukutani kwake, ajue mpira ni mipango sio kutumia nguvu nyingi za kutaka sifa wakati hazitafutwi alama tatu pale bali ni aggregate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…