Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Waziri wa Elimu ndugu Mkenda katika hotuba yake ya uzinduzi wa Mtaala mpya wa elimu ametoa kali ya mwaka pale aliposema kuwa Yeye na timu ya wataalam walipata ugumu kuonana na Rais ili wampatie briefing ya yaliyomo kwenye mtaala mpya. Nimezalisha maswali kadhaa ya tafakuri hapa....
Karibuni tujadili
- Waziri ambaye ameteuliwa na kuapa mbele ya Rais, na ambaye ni mjumbe wa Baraza La Mawaziri ambalo maamuzi yake hayahojiwi na chombo chochote nchini, ana hadhi kiwango gani ndani ya serikali?
- Waziri na Rais wanawasiliana ama kuonana vipi ilihali Rais ndiye amewateua kama wasaidizi muhimu kusimamia sekta zote nchini?
- Wasaidizi wa rais wana mamlaka gani kumzuia Waziri kuonana na rais pale anapoomba kufanya hivyo?
- Ikulu yetu ina utaratibu gani wa kumsaidia rais kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuonana ama kujadiliana ama kuwasiliana kwa karibu na wasaidizi wake muhimu na wakuu wa sekta zote nchini? yaani Mawaziri na manaibu wao..
- Kauli ya Waziri Mkenda inatuma ujumbe gani kwetu sisi wapigakura ambao hapo Oktoba tutatumia vichinjio vyetu kuchagua viongozi wa nchi?
Karibuni tujadili