Tutajie orodha ya kozi ambazo hazitoi ajira ili tupate kuzifahamu

Tutajie orodha ya kozi ambazo hazitoi ajira ili tupate kuzifahamu

unasoma theology ili ukaajiriwe?. utasota sana mtaani na cheti chako.

jizime data, ingia mtaani, anza kuhubiri huku ukitumia maarifa uliyopata kwenye masomo yako ya theology. wafanyie watu miujiza ya uongo na ukweli.

mahubiri yako yaegemee kuhusu mahusiano ya ndoa, uchumba na upatikanaji wa kipato cha mtu mmoja mmoja. hili ndio eneo ambalo utawapata wajinga wengi wa kukupa sadaka.

siku za kwanza baadhi ya watu watakuona chizi, watakudharau. ila miaka miwili au mitatu baadae utakuwa unamiliki kanisa lako. utajiri utakuwa unacheza kwenye mlango wako.
Mambo ya nguvu za kiume pia
 
Bachelor of Science in Mathematics

Akili zangu zote zimemwagikia hapo, nimebaki mweupe, mwenye stress, halafu waajili wanasema ndo kozi gani hiyo.

Mtaani nako wananichanganya tuu, maana kila mtu anauliza, "kwani hujapata kazi tuu, mbona ulikuaga na akili sana"
Nenda vyuoni mkuu hasa private probably ukaonwaaaa
 
Shahada ya kwanza
😂😂😂😂😂Kuna siku nilikuwa dodoma kwenye daladala Kaka mnamnyatia nyatia dada,anamuuliza uliza maswali,akaulizwa anasoma chuo gani nasikia binti anajibu anasoma mipango,Kaka kauliza unasoma kozi gani?dada kamjibu anasoma GPA.🙄🙄.....ndio wewe Sasa😂
 
Zama hizi nani akuajiri na hizo kozi?

Kwa mfano, hiyo degree ya procurement hakunaga muajiri bonafsi atakuchukua, subiri serikalini au taasisi za umma, nako ni kwa uchache mnoo tena kimchongo mnoo, na saturation point ilishafikiiwa na vyuo vinazidi kumwaga mamia ya wahitimu mtaani.

Business administration ndio haiwekani tena kuajirika.

Entrepreneurship nani akuajiri?
Ahahaha umesema ukweli mtupu procument na hzo ba Ni upuuzi sna hata uwe na ile ya bodi yao Bado msoto Ni mkali mno dada angu anayo hyo procument ila mkp sas hajapata Kaz

Account no koz Kali sna alfu ajira zake zipo kila siku
 
Nakushauri umshauri, ahame hiyo kozi. Japo saizi nasikia wana electives za ualimu ili wafae kuajiriwa kama walimu. Hiyo kozi ni majanga.

Ama kama nyumbani sio haba, na kichwani zinachaji haswa, akamalize na GPA kali halafu aunge master's.

Mkanye asidanganyike na stori za Dr. Sunzu. Huyu tuliwahi bishana juu ya tija ya hiyo kozi kwenye kipindi chake nikiwa mwaka wa tatu. Ni mtu smart ila kama H.O.D anashindwa kukudisappoint kwa kusema ukweli.

Akitaka ushauri wa kweli amtafute mtu anaitwa Dr. Mwaihuti, Stephen Mwaihuti.
Aisee Bora hat unasema ukweli mnk Kuna watu wabishi sna wanakumbia hyo kozi Ni dili San kwa Sasa watu wa hesabu wnapata kz mapema mno sas njoo mtaani utaonekana mjinga sna na hata ualimu uwezi kuwa dah mbaya San

Mm Ni mesoma account nimeshafanya kazi karibia kampuni tano HV na Wala Sina CPA
 
Bachelor of Science in Mathematics

Akili zangu zote zimemwagikia hapo, nimebaki mweupe, mwenye stress, halafu waajili wanasema ndo kozi gani hiyo.

Mtaani nako wananichanganya tuu, maana kila mtu anauliza, "kwani hujapata kazi tuu, mbona ulikuaga na akili sana"
Unanikumbusha UDSM enzi hizo chini ya Prof. Masenge
 
Dah aisee pole Bora ungepga ata bachelor ya statistics sema unaweza namba sana piga MASTERS YA STATITICS AU ENGINEERING
Mkuu hakuna stress mbaya kama kusoma hali ya kuwa huna pesa!! Maisha ya masters ili uyafurahie atleast uwe umeajiriwa,yaani unasoma huku pesa inaingia. Inatia sonona pale mbapo umesota mtaani na bachelor yako hujui mustakabali wa kazi, majukumu yanakuandama halafu uendelee tena kukaa darasani, ngumu sana!!!

Upo zako mabibo hostel unawaona wenzako wanaokuja kuchukua masters na Phd wote wanapaki ndinga zao nje ya block , wewe unakanyaga kwa miguu mpk soli inaisha. Kula yako inategemea boom la HESLB au viskolaship unavyokuwa funded nusu.
 
Back
Top Bottom