Vijana wa kiafrika hasa afrika mashariki ni wajinga wajinga sana! Kutwa kufuatilia ujinga... sasa nagundua mleta mada aliuliza makusudi ili tuone kiasi gani wasomi hewa wanazalishwa... mtu hasomi wala kufuatilia mambo yeye anakurupuka tu, kuna mtu ana shahada ya sayansi kwenye mahesabu, mwingine takwimu. Wanadai kazi hakuna. Daaahhh! Afrika [emoji17][emoji17][emoji17]
Kuna comment umeweka pale juu nikakuterm conscious, mapungufu machache nikayaelewa kibinaadam.
Hiki ulichoandika hapa ni kama mtu mwingine kabisa.
Ungesoma comments zangu zote, am sure hiki usingekiandika.
Chini kabisa nitakuwekea sifa ya umri wa kuingia jeshi, jambo uliloshauri pale juu. Ila hapa nitakwambia machache nikiwa moja ya vijana uliotuona "wajinga".
Kwanza kabisa, nina uhakika, ukipewa wewe fani hizi ziwe kichwani mwako na vyeti vyake, ukatafute hizo unazoziita kazi, hata kusurvive hutaweza.
Pili kwa kutambua ukubwa wa tatizo kwenye fani husika, chuo kimemodify hii program, yakwanza imechanganywa na moduli za ualimu ili graduate wake waqualify tamisemi, nyingine imefanywa kua Bachelor of Science in Mathematics and Computer Science. Hiyo kwa uchache.
Ulishauri kufundisha. Nilisema pale juu, nilipewa mpaka nyumba na masister wa kikatoliki pale morogoro. Kwa muongozo wa tamisemi mratibu elimu alinikataa mimi kua mwalimu.
Umeshauri jeshi.
Soma hapa kigezo cha umri kwa elimu husika.
Kwa vijana wenye elimu ya darasa la saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18.
Vijana wenye elimu kidato cha nne umri usiwe zaidi ya miaka 20.
Vijana wenye elimu ya kidato cha sita umri usiwe zaidi ya miaka 22.
Vijana wenye elimu ya stashahada umri usiwe zaidi ya miaka 25.
Vijana wenye elimu ya shahada umri usiwe zaidi ya miaka 26
Vijana wenye elimu ya shahada ya uzamili umri usiwe zaidi ya miaka 30
Vijana wenye elimu ya shahada ya uzamivu umri usiwe zaidi ya miaka 35.
Hata nikapewe hiyo masters sasahivi, jeshi singii. Labda nipate phd.
Mwisho nitasema kama kijana mjinga wa afrika mashariki, ninayefatilia ujinga..
Kama kweli unayo kazi unayofanya, kama kweli ulipata hiyo kazi kwa kuitafuta mwenyewe kwa uwezo wako, kama kweli unafatilia mambo ya msingi yanayoendelea kwenye hili taifa, hautarudia kucomment vitu kama nilivyokuquote hapa.