Tutamkumbuka kwa lipi Ummy Mwalimu?

Kuiboresha NHIF na msd toka zilipokuwa Hadi hapa zilipo sasa , soma pamoja na taarifa ya mkaguzi mkuu WA Sirikali
 
Ummy kashindwa kuidhibiti NHIF, NHIF watu wanaiba sana mpaka hpspitali hazilipwi. Aga Khan wamefunga, Hospitali zingine mfano Tiba, sasa hivi hawapokei bima za NHIF.

NHIF kuna pesa nyingi sana lakini kuna madudu ya kufa mtu, kama haijapewa kampuni binafsi kuiendesha, itawaondosha wengi sana.

Madudu NHIF na Madudu MADAWA ni ya kufa mtu.
 
Hivi kabudi si ndio Allenda kunywa nyungu Madagascar au sikumbuki πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£
Ndio. Alitumwa na magufuli kwenda kuileta Tanzania. Alishiriki ushirikina. Magufuli bana, mwanasayansi gani unaamini ushirikina hata kikombe cha loliondo alienda kunywa
 
Zile pingili zake shingoni
 
Kiutendaji ni kama Rais wetu tu
 
Kuna kitu hufahamu kuhusu NHIF, na watu wengi wamekaririshwa. Ngoja nikupe shule kidogo.

NHIF ni suala mtambuka kwa 100%, japokuwa inafanya kazi chini ya wizara ya afya lakini uratibu wake uko chini ya Rais na baraza la mawaziri kwa sababu uendeshaji wake unahitaji pesa nyingi kutoka wizara ya fedha na utumishi. Waziri wa Afya hawezi kutunga sheria wala sera za uendeshaji wake, hawezi kuteua wala kutengua mtendaji yoyote wa NHIF.
Suala la NHIF ni sawa sawa na suala la bodi ya mikopo (HESLB), Mifuko ya Pension, TANROAD, EWURA, REA. Waziri hawezi chochote linapokuja suala la kisera au sheria za uendeshaji wake. Ukiona kikotoo cha wastaafu kinawapunja wastaafu usikimbilie kumlaumu waziri husika maana hata yeye hana mamlaka ya kubadili chochote zaidi ya kupambana kusimamia utekelezaji wake.
 
Angeidhibiti vipi bila kuwa dikiteta? Wakati wa Magufuli NHIF haikuwa na upuuzi huu wa sasa hivi kwa sababu ya usimamizi wa wakati ule.
 
Kila kitu Tanzania hii kipo chini ya Rais, hilo unalosema wala siyo ajabu.
 
Amesimamia mageuzi mapya katika sekta ya Afya kwa awamu ya 4 na 5! Ujenzi wa vituo vya afya,hospitali za wilaya,ununuzi wa vifaa mbali mbali vya Matibabu,uboreshaji wa majengo,nk
Kwa kweli alijitahidi,mnyonge mnyongeni lakini yake mpe!
Nadhani Mama ameamua kumpumzisha kama Prof.Kabudi na Lukuvi,huenda atamrusha kama ataendelea mpaka 2030!
 
Huko ulimwengu gani mkuu, ni nchi gani imetawaliwa na uingereza barani africa na mawaziri wake hawatokani na bunge?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…