Tutamkumbuka kwa lipi Ummy Mwalimu?

Tutamkumbuka kwa lipi Ummy Mwalimu?

Ummy kashindwa kuidhibiti NHIF, NHIF watu wanaiba sana mpaka hpspitali hazilipwi. Aga Khan wamefunga, Hospitali zingine mfano Tiba, sasa hivi hawapokei bima za NHIF.

NHIF kuna pesa nyingi sana lakini kuna madudu ya kufa mtu, kama haijapewa kampuni binafsi kuiendesha, itawaondosha wengi sana.

Madudu NHIF na Madudu MADAWA ni ya kufa mtu.
Kwa mara ya kwanza leo naona point, hongera sana
 
Amesimamia mageuzi mapya katika sekta ya Afya kwa awamu ya 4 na 5! Ujenzi wa vituo vya afya,hospitali za wilaya,ununuzi wa vifaa mbali mbali vya Matibabu,uboreshaji wa majengo,nk
Kwa kweli alijitahidi,mnyonge mnyongeni lakini yake mpe!
Nadhani Mama ameamua kumpumzisha kama Prof.Kabudi na Lukuvi,huenda atamrusha kama ataendelea mpaka 2030!
Kutenguliwa siyo kupumzishwa, ni kufedheheshwa tu.

Ni bora Rais avunje baraza la mawaziri na kuliunda upya hapo ukiachwa kuna heshima ya kusema umrpumzishwa, lakini kutenguliwa ni kuvunjiana heshima tu, kwa mimi ukiniteuwa tena sikubali uteuzi nabaki na ubunge wangu kuwakilisha wananchi, lakini kwakuwa maccm yanawakilisha matumbo yao wacha waendelee kudhalilishwa tu.
 
Nchi inahitaji kufanyiwa overhaul kwa kuiondowa ccm imeshafeli waje kuongoza watu wapya.

Chini ya ccm maigizo yataendelea tu, sasa jiulize waziri wa hovyo kama Mwigulu mbona haguswi?
Wakushika nchi Sasa ndo wananjaa zaidi Hadi washibe ni miaka ya xxm. unaoonekana ni mbadala hauaminiki
 
Uteuzi uliofanywa na Mhe. Rais SSH tatehe 14 Agosti 2024 umemtema nje bi Ummy Mwalimu kutoka Wizara ya Afya.

Kutokana na unyeti wa Wizara ya Afya, umuhimu wake ni mkubwa kwenye jamii. Pamoja na kusimamia sera ya Afya nchini lakini ndiyo wizara inayosimamia taaluma ya wahudumu wa Afya.

Je tuna lipi la kumkumbuka dada Ummy kama mchango wake kwenye kuimarisha ama kuidhoofiaha sekta ya afya nchini

Pia soma: Ummy Mwalimu atenguliwa Uwaziri wa Afya
Namkumbuka aliingia kudeki sakafu somewhere kulikuwa kuchafu🤣
 
Kutenguliwa siyo kupumzishwa, ni kufedheheshwa tu.

Ni bora Rais avunje baraza la mawaziri na kuliunda upya hapo ukiachwa kuna heshima ya kusema umrpumzishwa, lakini kutenguliwa ni kuvunjiana heshima tu, kwa mimi ukiniteuwa tena sikubali uteuzi nabaki na ubunge wangu kuwakilisha wananchi, lakini kwakuwa maccm yanawakilisha matumbo yao wacha waendelee kudhalilishwa tu.
Mkuu hayo ni mabadiliko ya kawaida!
 
Wakati wa mwenbda zake ndiyo ilikuwa inapigwa juu kwa juu. Ni heri ujikalie kimya tu. Ingekuwa ya maana isingefumuliwa.
SIyo kweli; enzi zile NIHF ilikuwa inaheshimika na hospitali zote. Leo hii ukiwa na kadi ya NIHF utakwama karibu hospitali zote isipokuwa labda za serikali tu.
 
Dorothy Gwajima angerudishwa Wizara ya Afya, yaani ingekuwa mtu sahihi sanaaa nionavyo..!!
Dorothy hafai kuwa waziri wa afya
Madakari hawafai kuwa mawaziri kwenye hii wizara maana wizara ina kada nyingi sana ila wakiwa wao ndio maboss wanajipakulia nyama zote.hawawajibishajibishani,daktari mwenzao anaweza hata kufanya ugaidi na bado wakamtetea,akifanya kosa mtu wa kada nyingine utaona media za dunia nzima wameitwa kupewa taarifa
 
Back
Top Bottom