#COVID19 Tutegemee nini baada ya Rais Samia kusema 'Gwajiboy oyee Tunachanja, hatuchanji' mbele ya Askofu Gwajima?

Sasa swali langu lilikuwa kama si Magufuli kupotosha je watanzania wengi wangekubali kuchanjwa? lakini kumbe hata Magufuli asingepotosha bado ingehitajika nguvu kubwa ili kuwashawishi watanzania wengi kukubali kuchanjwa,
Kama Magufuli asingepotosha nguvu ambayo ingetumika isingekuwa kubwa sana ukilinganisha na Magufuli alipopotosha kwa sababu kumbuka kushawishi watu wasahau ule upotoshaji mkubwa wa Magufuli ndipo nguvu kubwa ya kushawishi watu inapohitajika.
Kama siyo Magufuli ni kweli ingekuwa rahisi tu kushawishi watu sasa hivi na kukubali kuchanja.Kumbuka Magufuli alikuwa ni mwanasiasa ambae ni populist.Huwa ni kazi ngumu sana kuneutralize na kufuta anachosema populist kwa sababu populist huwa wana ushawishi na nguvu nyingi sana katika jamii.Wanaomlaumu Magufuli katika hili wapo sahihi.
 
Mleta mada inaonekana ww ndio una umaskini mkubwa wa akili.Kwa umaskini wako mkubwa wa akili unaona Kawe tu ndio wanapinga chanjo.Nenda ulaya,USA,kote kuna ambao hawataki chanjo.Mpaka Rais wa USA alitoa bonus ya uds 200ili wachanjwe.Je nao wanaumasikini wa akili au bogas www ndio maskini mkubwa wa akili.Aidha ukichanjwa bado upo kwenye hatari mkubwa ya kuambukizwa na kuambukiza.Wanaochanjwa waheshimiwe na wasiochanjwa waheshimiwe.Watu msio na ufahamu wa hivi vitu mnyamaze.
 

Mungu ni wa dunia nzima, makao makuu yake hayapo Tanzania
 
Na kwa taarifa yako MagufuliJP was very right. Na ccm wasijaribu kufanya kosa hilo. Sasa hivi mambo mengi sana hayaendi na wanakumbuka MagufuliJP. Ukisema chochote cha kumnanga MagufuliJP you will test the heat [emoji91] of stone. Acha ujinga.

Kwa study iliyo fanyika Israel walio ugua corona wanakuwa na kinga kubwa dhidi ya virusi vya aina zote vya corona. Ambacho ndo hicho MagufuliJP alisema. Tuache usambae ili tupate kinga. Na sisi ukiangalia hatujapata Madhara makubwa kama nchi nyingine. Watu wanakufa sana baada ya kupata chanjo. Tuna madaktari kama 5 wamekufa baada ya chanjo. Nina rafiki zangu wanne wamekufa baada ya chanjo.
 
Duh,wachanje tu!
Magufuli alikuwa sahihi kabisa kwenye hili!
 
Gwajiboy 3 Ndugai na Gwajigirl 0
 
Yaani wabongo bwana!
Uko sahihi nimeona utube maandamano nchi za ulaya wanaopinga chanjo nashangaa hapa wanataka kutufanya tunaokataa kana kwamba hatuna elimu,masikini ,ulaya je?

Na nina mifano ya waliochanja wamekufa ukilinganisha ambao hawajachanja!

Ht tunaopinga chanjo tuheshimiwe!
 
Huyu atafeli mno katika utawala wake wa kurithi.
Analeta mambo ya Meko Meko kuongea ujinga kwenye majukwaa .

Sukuma gang wamemzidi nguvu sasa anapuyanga puyunga tu.

1.Mara tozo ziko palepale
2.Mara Wahisani hawaleti misaada wanataka tufanye BIASHARA...wakati kila siku anaomba misaada ya chanjo ,fedha za maendeleo na mikopo juu anapokea.
3.Kelele za mpangaji hazmzuii mwenye nyumba kulala
4.Mara tupige picha tupeleke meseji kuwa yanayosemwa sio yaliyopo
5.Mara Gwajiboy hoyeeee na kampandisha hadi kwenye gari lake
Ujinga mtupu
Anapuyanga puyanga.
 
Magufuli hajawahi kupotosha,kwenye hili jambo I stand with him!alikuwa sahihi,na ilitusaidia kuondoa hofu na Mungu alituvusha salama bila lockdown wala chanjo!
Unaweza compare na nchi zilizokuwa na lockdown kwa vifo?,hebu muogopeni Mungu.
Hizi chanjo hata mataifa mengine zinapingwa sembuse Tanzania? Acheni kumuonea Magufuli!
Gwajima yuko sahihi,tusiotaka chanjo tuheshimiwe,tuna elimu,tuna uelewa nk na wala sio masikini! Nyie,kachanjeni tu!
 
Viongozi hawawezi toa amri sababu chanjo ni hiari,ila wameshauri usipotoshe!

Chanjo haizuii maambukizi!
Ukichanja lzm ufuate tahadhari zote!
Sasa chanjo ya nini?
 
Na kwa taarifa yako MagufuliJP was very right. Na ccm wasijaribu kufanya kosa hilo.
Magufuli alikuwa very right kwa sababu gani?Hoja yako ni ipi?
Sasa hivi mambo mengi sana hayaendi na wanakumbuka MagufuliJP. Ukisema chochote cha kumnanga MagufuliJP you will test the heat [emoji91] of stone. Acha ujinga.
Kwa ushahidi wa ile ripoti ya CAG ambayo ilikuwa ni chafu sana, Magufuli alikuwa ni kiongozi populist ambae alikuwa ni mwizi,fisadi na mzembe wa mali za uma aliekuwa anajificha kwenye chaka la siasa za propaganda ili kulaghai wajinga.
Kwa study iliyo fanyika Israel walio ugua corona wanakuwa na kinga kubwa dhidi ya virusi vya aina zote vya corona. Ambacho ndo hicho MagufuliJP alisema. Tuache usambae ili tupate kinga.
Ukisema kuwa tuache usambae ili tupate kinga maana yake ni kwamba unawatoa sadaka wazee pamoja na watu wenye magonjwa sugu kitu ambacho hakikubaliki hata kidogo.
Na sisi ukiangalia hatujapata Madhara makubwa kama nchi nyingine.
Umejuaje kuwa hatupati madhara kama nchi nyingine wakati hakuna takwimu zinazotolewa?Umefanya tafiti gani ya nchi nzima hadi ukajua kuwa hatujapata madhara kama nchi nyingine?Yaani umetumia kigezo gani kujua kuwa hatujapata madhara kama nchi nyingine?
Watu wanakufa sana baada ya kupata chanjo. Tuna madaktari kama 5 wamekufa baada ya chanjo. Nina rafiki zangu wanne wamekufa baada ya chanjo.
Watu kufa baada ya kupata chanjo ni jambo la kawaida kabisa na ni jambo lililothibitishwa kisayansi kwa sababu hizi chanjo zina efficacy.Kama efficacy ya chanjo ni asilimia 70 lazima kuna watu wengi tu watakufa baada ya kupata chanjo.Unaelewa maana halisi ya efficacy katika chanjo?
 
Viongozi hawawezi toa amri sababu chanjo ni hiari,ila wameshauri usipotoshe!

Chanjo haizuii maambukizi!
Ukichanja lzm ufuate tahadhari zote!
Sasa chanjo ya nini?
Amri ni kwa watumishi sio waumini hata serikali inaweza sema mtumishi wa umma chanzo lazima hutaki tupishe usituletee ugonjwa,imefanyika hivyo nchi nyingi tuu na ilianza kwa neno hiari.

Kimsingi huna hiari ya kuambukiza wengine nadhani ulimsikia na Spika aliwaambia hivyo hivyo wabunge.

Achaneni na ujinga wa imani za ujinga wa kina Gwajima,mafuta ya mwamposa na ushirikina.
 
Magufuli hajawahi kupotosha,kwenye hili jambo I stand with him!alikuwa sahihi,na ilitusaidia kuondoa hofu na Mungu alituvusha salama bila lockdown wala chanjo!
Unaweza compare na nchi zilizokuwa na lockdown kwa vifo?,
Mungu ametuvusha salama kivipi?Una takwimu za watu waliokufa kwa Corona Tanzania?Unavyosema kwamba madhara tuliyopata huwezi kulinganisha na madhara waliopata watu waliokuwa na lockdown kwani unayajua madhara ambayo Tanzania imepata?Una data/takwimu?Unatumia kigezo gani kujua kuwa Tanzania haijapata madhara makubwa?Umefanya tafiti nchi nzima ukajua kuwa waliokufa kwa Corona siyo wengi?Hoja yangu hapa ni kwamba umetumia kigezo gani kufikia conclusion uliofikia kuwa Tanzania haikupata madhara makubwa wakati hadi kutoa takwimu ilipigwa marufuku?
hebu muogopeni Mungu.
Hizi chanjo hata mataifa mengine zinapingwa sembuse Tanzania?
Chanjo kupingwa katika mataifa mengine haihalalishi kuwa chanjo kupingwa Tanzania ni sahihi.Kwani nchi nyingine hazina wajinga?Hizo nchi nyingine wanaishi miungu ambayo haiwezi kuwa wajinga?Si wanaishi tu binadamu kama Tanzania?
Acheni kumuonea Magufuli!
Gwajima yuko sahihi,tusiotaka chanjo tuheshimiwe,tuna elimu,tuna uelewa nk na wala sio masikini! Nyie,kachanjeni tu!
Gwajima hayupo sahihi kwa sababu ni mbumbumbu peke yake ndiye anaweza kupingana na sayansi.Wewe unazikataa chanjo kwa kigezo kipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…