#COVID19 Tutegemee nini baada ya Rais Samia kusema 'Gwajiboy oyee Tunachanja, hatuchanji' mbele ya Askofu Gwajima?

#COVID19 Tutegemee nini baada ya Rais Samia kusema 'Gwajiboy oyee Tunachanja, hatuchanji' mbele ya Askofu Gwajima?

Leo wakati Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akielekea Bagamoyo kurecord filamu ya kutangaza utalii wa Tanzania alisimama kwenye jimbo la Kawe ili kusalimia wananchi.

Rais alimsimamisha Mbunge wa Kawe ili kutoa neno lakini kabla ya kumsimamisha aliwauliza wananchi wa Kawe kama watachanja au la kama video inavyoonyesha hapa chini.Katika hali ya kustaajabisha na ya kushangaza wananchi walimwambia Rais bila ya kupepesa macho kuwa hawatachanja kama video hii inavyoonyesha hapa chini.

Nimejiuliza maswali mengi sana.Kwa nini Rais aulize swali hilo kwenye jimbo ambalo mbunge wake hakubaliani na mambo ya chanjo?Ina maana Rais hajui kwamba kazi kubwa ambayo walifanya katika awamu ya tano ya kupinga chanjo ilifanikiwa sana hasa ukizingatia kuwa kazi hiyo ilifanyika katika Taifa lenye umasikini mkubwa sana wa akili?

My take:
Kwa sasa hivi serikali ya CCM inapata shida sana kula matapishi yake yenyewe ambayo waliyatapika katika awamu ya tano.Ni vyema serikali ikiri mbele ya wananchi kuwa Rais Magufuli hakuwa sahihi na alipotosha sana uma ili wananchi waanze upya kuelimishwa juu ya gonjwa la Corona na chanjo.

Kufa kwa covid kwa raha zako.
 
Khaaa!!!Wapi nimesema kuwa kama siyo Magufuli?Umesoma nilichoandika kweli?

Mimi kwenye hoja yangu nimejikita zaidi kwenye ishu ya umasikini wa akili.

Rais yeyote hata kama asingekuwa Magufuli akitamka tu kuwa chanjo ni mbaya basi Watanzania wengi watamwamini sana kwa sababu ni ishu ya kipumbavu.Soma nilichoandika sitaki nirudie tena.
Hicho unachokieleza ndio maana nikauliza kuwa ni sawa na kusema kwamba kama si Magufuli(au rais yeyote) kusemakwamba chanjo ni mbaya je watanzania wengi wangekubali kuchanjwa?

Nauliza hivyo kwa sababu naona anatajwa sana Magufuli kwamba ndio kawapotosha watu.
 
Ndiyo,sababu ni Magufuli.Mfano kama Magufuli angetumia nguvu kubwa kuelimisha watu kuwa chanjo ni nzuri na ni muhimu watu wengi sana leo hii wangekubali kuchanjwa lakini yeye alitumia nguvu nyingi kufundisha kuwa chanjo hazifai
 
Ndiyo,sababu ni Magufuli.Mfano kama Magufuli angetumia nguvu kubwa kuelimisha watu kuwa chanjo ni nzuri na ni muhimu watu wengi sana leo hii wangekubali kuchanjwa lakini yeye alitumia nguvu nyingi kufundisha kuwa chanjo hazifaiView attachment 1921411
Kwahiyo ilitakiwa atumie nguvu nyingi ili ndio watanzania wakubali kuchanjwa?
 
Kwahiyo ilitakiwa atumie nguvu nyingi ili ndio watanzania wakubali kuchanjwa?
Alitakiwa atumie nguvu nyingi kuelimisha.Kazi ya kiongozi ni kuelimisha na wala siyo kupotosha.Magufuli alikuwa anatumia nguvu nyingi kupotosha.

Dada yangu kule kijijini amekataa kuchanjwa, nilipomuuliza kwa nini hataki kuchanja ameniambia kuwa Magufuli alisema kwenye redio kuwa chanjo hazifai.

Mtu kama huyu angeelimishwa na kiongozi huyu wa nchi angekubali kuchanjwa.

Watanzania wengi hawana elimu kwa hiyo kile wanachoambiwa na viongozi wao wanapokea kama kilivyo.Watu hawa wanapaswa kuelimishwa badala ya kupotoshwa.
 
Kuna watu ni wajinga sana, katika nchi yenye watu million 60 , watu hata 50 hawafiki waliokufa na corona for last one year na ushee bila lockdown Wala bila hofu yeyote na Rais aliekuvusha hapo una sema alidanganya wananchi? Chanjo ni hiari na ukiachia hiari unadhani Samia anaweza simamia chochote na kufaulu? Let's not west out time with Samia, hizo pesa za chanjo bora zipelekwe kwenye utoaji wa vitambulisho vya taifa.
 
Kwenye video clip hii hapa chini (wakati Magufuli ndiyo rais), Samia anasikika akiwananga na kuwa ridicule "mabeberu" ambao eti sasa anataka kuwauzia ile "royal movie" yake - IRONICAL!

Producer "beberu" itabidi hii clip aiweke kama trailer halafu tuone kama hiyo movie yake itanoga!!

Siamini Kama ni rais wetu huyuhuyu ambaye Sasa hamutaji Mungu kabisa hata kwa kukosea.
 
Tatizo lilianzia hapo kwenye HIARI
Walitakiwa watangaze tu chanjo zipo watu waende wakachanje
 
Alitakiwa atumie nguvu nyingi kuelimisha.Kazi ya kiongozi ni kuelimisha na wala siyo kupotosha.Magufuli alikuwa anatumia nguvu nyingi kupotosha.

Dada yangu kule kijijini amekataa kuchanjwa, nilipomuuliza kwa nini hataki kuchanja ameniambia kuwa Magufuli alisema kwenye redio kuwa chanjo hazifai.

Mtu kama huyu angeelimishwa na kiongozi huyu wa nchi angekubali kuchanjwa.

Watanzania wengi hawana elimu kwa hiyo kile wanachoambiwa na viongozi wao wanapokea kama kilivyo.Watu hawa wanapaswa kuelimishwa badala ya kupotoshwa.
Kaelimishe wewe na uwajibu maswali yao yote

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
President Samia leo huku kwetu kawe ulikutana na wananchi na kuwaeleza faida za kuchanja chanjo ya covid 19.Wale uliwaoona wakimshangilia Kakobe ni wafuasi wake na sio wananchi wa kawe.Aliwatoa maeneo mbalimbali ya Dar na mpaka mikoani.Leo waziri wako wa mambo ya ndani anaweweseka eti hatuwezi kuingilia imani za watu.Askofu hatuhumiwi kwa kuwaambia wafuasi wake wasichanje,bali anatuhumiwa kwa kumkashifu Rais na taasisi zake.Hilo ni kosa kubwa na kama ataachwa hivi hivi basi tunapoelekea pabaya.Ndio maana tunasisitiza siasa na dini haziendani.
 
Alitakiwa atumie nguvu nyingi kuelimisha.Kazi ya kiongozi ni kuelimisha na wala siyo kupotosha.Magufuli alikuwa anatumia nguvu nyingi kupotosha.

Dada yangu kule kijijini amekataa kuchanjwa, nilipomuuliza kwa nini hataki kuchanja ameniambia kuwa Magufuli alisema kwenye redio kuwa chanjo hazifai.

Mtu kama huyu angeelimishwa na kiongozi huyu wa nchi angekubali kuchanjwa.

Watanzania wengi hawana elimu kwa hiyo kile wanachoambiwa na viongozi wao wanapokea kama kilivyo.Watu hawa wanapaswa kuelimishwa badala ya kupotoshwa.
Sasa swali langu lilikuwa kama si Magufuli kupotosha je watanzania wengi wangekubali kuchanjwa? lakini kumbe hata Magufuli asingepotosha bado ingehitajika nguvu kubwa ili kuwashawishi watanzania wengi kukubali kuchanjwa, sasa nachokiona sasa hivi sioni nguvu kubwa kutumika kuwashawishi watu kuchanjwa bali naona watu wanatumia muda mwingi kumlaumu Magufuli kuwa ndio sababu ya watu kukataa kuchanjwa kana kwamba imetumika kila jitihada vya kutosha kuwashawishi na kuwaelimisha ikashindikana au kwamba kama si Magufuli basi ingekuwa rahisi tu kwamba watanzania wengi wangekubali kuchanjwa wenyewe tu.
 
Chanjo haikataliwi Tanzania pekee, USA, Canada, UK na nchi nyingine nyingi tu watu wanakataa kuchanjwa. Why watu wanashupaza shingo ili tu wengi wachanjwe wakati hata hiyo bajeti ya chanjo hawaifahamu?
 
Ndio mie nashangaa kwamba pamoja na huko kwengine nako wapo watu wanakataa chanjo wengine hadi wamefukuzwa kazi zao kwa kugoma kuchanjwa ila et Bongo chanzo cha watu kutochanjwa ni Magufuli tu.
 
Nimejiuliza maswali mengi sana.Kwa nini Rais aulize swali hilo kwenye jimbo ambalo mbunge wake hakubaliani na mambo ya chanjo?Ina maana Rais hajui kwamba kazi kubwa ambayo walifanya katika awamu ya tano ya kupinga chanjo ilifanikiwa sana hasa ukizingatia kuwa kazi hiyo ilifanyika katika Taifa lenye umasikini mkubwa sana wa akili?
Kuamua kutochanjwa siyo kuwa na umaskini mkubwa wa akili. Jifunze kuheshimiana na watu wenye mitazamo tofauti na wa kwako.
Shilingi ina pande mbili, mtu anayeona upande mmoja tu asiangalie upande ule wa pili huyo ndiye tunaweza kusema ana umaskini mkubwa wa akili.
 
Wananch sio wajinga wewe

Nenda makanisani mfano ya katoliki yaliyojaa wasomi wakubwa unakuta ni padri tu ndie kavaa barakoa ina maana waumini wote hawajielewi kasoro huyo padri tu? Wote hawajasoma na wana uelewa mdogo kasoro padri tu?

Ina maana wasomi wote wanaojazana makanisani na misikitini bila barakoa uelewa wao hawana?

Wananchi wanajielewa sana kuliko viongozi

Unapoona kiongozi wa dini yeye peke yake ndie kavaa barakoa waumini hawajavaa ujue kuwa waumini wana imani kwa Mungu kuliko kiongozi wao!!!! Kiongozi anaamini kuwa akiwa kanisani kwenye nyumba ya Mungu MUNGU ANAWEZA MTUPIA CORONA WAKATI WAUMINI HAWAAMINI HILO
Huwa nawashangaa Sana Mapadre halafu ukienda Hospitali ya Cardinal Rugambwa pale Ukonga wamejazana kibao wakiwa na changamoto za upumuaji.
 
Apo kwa magufuli hakua sahihi huo moto ni hatar hawato weza kuuzima wakomae apo apo kwenye chanjo wataweza kuwaita kwenye kamat
 
Back
Top Bottom