#COVID19 Tutegemee nini baada ya Rais Samia kusema 'Gwajiboy oyee Tunachanja, hatuchanji' mbele ya Askofu Gwajima?

#COVID19 Tutegemee nini baada ya Rais Samia kusema 'Gwajiboy oyee Tunachanja, hatuchanji' mbele ya Askofu Gwajima?

Serikali iliyokuwa inapinga chanjo awamu ya tano ina moral authority gani ya kuweza kutoa elimu juu ya chanjo leo hii?Yaani serikali ileile iliyokuwa inashirikiana na Magufuli katika awamu ya tano katika kupinga chanjo leo hii ibadilike kutoa elimu juu ya chanjo? WTF!
Mbona imebadilika na sasa imekubali chanjo na kuzileta? sasa hapo kinashindikana nini kingine?
 
Kwani si uvae barakoa kujikinga na hatua zingine? Je ni haki yako kuingilia uhuru wa afya yangu?
Barakoa sio kinga kamili. Inanizuia mimi kuambukiza kuliko kuambukizwa.

Huu ugonjwa ni kama suala la kuvuta sigara. Uvutaji wa sigara unapigwa marufuku katika public spaces sio kwa sababu utamdhuru mvutaji bali athari kubwa wanayoweza kupata wanaomzunguka kwa kuvuta moshi wa sigara anaoutoa. Ingawa ana haki ya kudharau uwezekano wa yeye kupata cancer lakini hana haki ya kuambukiza wengine.

Ndio maana unaambiwa ukitaka kuvuta sigara, vuta ukiwa mwenyewe au na wavutaji wenzako lakini sio kwenye sehemu inayotumiwa na wasiovuta. Hivyo hivyo na huu ugonjwa. Kama hautaki kuchanja kaa nyumbani au shirikiana na wenye mtazamo kama wako lakini usichanganyane na wale ambao wamechanja au wangependa kuchanja lakini hali yao haiwaruhusu.

Amandla...
 
Mnaoililia chanjo mnajisikiaje huko mlipo? Hahahaha 🤣🤣🤣
 
Mbona imebadilika na sasa imekubali chanjo na kuzileta? sasa hapo kinashindikana nini kingine?
Serikali ya Samia haijaleta chanjo kwa sababu eti ina nia ya kukinga watu dhidi ya Corona na hili linathibitishwa na tabia ya Serikali kutokujali kabisa kanuni za kupambana na Corona kama vile kuzuia mikusanyiko na kadhalika.

Serikali ingekuwa na nia ya kupambana na Corona kupitia chanjo wangetoa elimu juu ya chanjo.

Serikali ya Samia imeleta chanjo kwa sababu zifuatazo:

1.Kukwepa kutengwa kimataifa.

2.Kupata fedha zinazoambatana na masuala ya kupambana na Corona.

3.Kujisafisha kutoka kwenye upuuzi aliofanya Magufuli wa kupinga chanjo katika awamu ya tano.

4.Kuvutia wawekezaji pamoja na watalii kwa kuidanganya dunia kwamba Tanzania inapambana na Corona.
 
Serikali ya Samia haijaleta chanjo kwa sababu eti ina nia ya kukinga watu dhidi ya Corona na hili linathibitishwa na tabia ya Serikali kutokujali kabisa kanuni za kupambana na Corona kama vile kuzuia mikusanyiko na kadhalika.

Serikali ingekuwa na nia ya kupambana na Corona wangetoa elimu juu ya chanjo.

Serikali ya Samia imeleta chanjo kwa sababu zifuatazo:

1.Kukwepa kutengwa kimataifa.

2.Kupata fedha zinazoambatana na masuala ya kupambana na Corona.

3.Kujisafisha kutoka kwenye upuuzi aliofanya Magufuli wa kupinga chanjo katika awamu ya tano.

4.Kuvutia wawekezaji pamoja na watalii kwa kuidanganya dunia kwamba Tanzania inapambana na Corona.
Kama ni hivyo basi hatuwezi kuendelea kumbebesha lawama Magufuli kuwa et ndio kikwazo cha watu wengi kutokuchanja wakati kumbe tatizo ni hii serikali yenyewe ya sasa.
 
Kama ni hivyo basi hatuwezi kuendelea kumbebesha lawama Magufuli kuwa et ndio kikwazo cha watu wengi kutokuchanja wakati kumbe tatizo ni hii serikali yenyewe ya sasa.
Lawama zote ni lazima azibebe Magufuli kwa sababu serikali iliyopo madarakani sasa hivi imepata mentality,uzoefu,kiburi pamoja na mafunzo ya kupinga chanjo kutoka kwa Magufuli kwa sababu ndiyo iliyokuwa serikali ya Magufuli na huo ndiyo urithi ambao Magufuli aliuacha kwa serikali yake alipokufa.
 
Amri ni kwa watumishi sio waumini hata serikali inaweza sema mtumishi wa umma chanzo lazima hutaki tupishe usituletee ugonjwa,imefanyika hivyo nchi nyingi tuu na ilianza kwa neno hiari.

Kimsingi huna hiari ya kuambukiza wengine nadhani ulimsikia na Spika aliwaambia hivyo hivyo wabunge.

Achaneni na ujinga wa imani za ujinga wa kina Gwajima,mafuta ya mwamposa na ushirikina.
Chuki zako dhidi ya JPM usizilete kwa watu kutaka kulazimisha unavyotaka wewe.

Unadai asiyechanja anakuambukiza una uhakika? Nadharia zilizopo kuhusu chanjo zinakiri kuwa hata aliyechanja anaambukiza sasa kwa nini ushupalie asiyechanja? Pia mmekuwa mnasema aliyechanja hata akipata corona kwake haina makali na hahitaji oksijeni, sasa maana yake kama kufa atakayekufa kwanza ni asiyechanja sasa wewe wasiwasi wako wa nini?

Tafuta njia za waziwazi za kumpinga JPM sio kujifichia katika corona.

Haitakiwi mtu yeyote azungumze lugha ya kulazimishana katika mambo ya binafsi; mtu akitoa maoni humu kuwa mnaolazimisha chanjo muuwawe je utakubaliana na huo uhuru wa maoni? Uhuru wako unaishia pale uhuru wa mwenzio unapoishia.

Kuna watumishi wengi tu hawatachanja lije jua ije mvua.
 
Mama alifanya vizuri kwa sababu kusema tunachanja hatuchanji na wananchi kuitikia tunachanjaaaa
Askofu kaishiwa pozi na hakutaka kuweka comment badala yake kabase kwenye matatizo ya wananchi wake wa kawe

Mama kambana askofu angemuhoji pale direct ingekuwa ni udhalilishaji
Lakini ni kama tu kamtaka askofu aseme tunachanja na ajue huo ndiyo msimamo

Mama hayupo upande wa askofu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Acha uongo wewe, hao wananchi uliowasikia wanasema wanachanja ni wa wapi?
 
Lawama zote ni lazima azibebe Magufuli kwa sababu serikali iliyopo madarakani sasa hivi imepata mentality,uzoefu,kiburi pamoja na mafunzo ya kupinga chanjo kutoka kwa Magufuli kwa sababu ndiyo iliyokuwa serikali ya Magufuli na huo ndiyo urithi ambao Magufuli aliuacha kwa serikali yake alipokufa.
Unajua mwanzo ilikuwa lawama ni kwamba haziletwi chanjo serikali ya Magufuli haikutaka chanjo ila sasa serikali hii imeleta chanjo kitu ambacho ni tofauti na msimamo wa serikali ya Magufuli kwamba chanjo ni mbaya, na si tu kwamba serikali hii imeleta chanjo bali viongozi wake ndio wakwanza kuchanja hadharani kuonesha kwamba chanjo hazina madhara kama ulivyokuwa msimamo wa Magufuli katika serikali yake.

Sasa ukiniambia kuwa serikali hii imepata uzoefu wa kupinga chanjo kutoka kwa Magufuli itabidi nikushangae ni nini unazungumza?
 
Wananch sio wajinga wewe

Nenda makanisani mfano ya katoliki yaliyojaa wasomi wakubwa unakuta ni padri tu ndie kavaa barakoa ina maana waumini wote hawajielewi kasoro huyo padri tu? Wote hawajasoma na wana uelewa mdogo kasoro padri tu?

Ina maana wasomi wote wanaojazana makanisani na misikitini bila barakoa uelewa wao hawana?

Wananchi wanajielewa sana kuliko viongozi

Unapoona kiongozi wa dini yeye peke yake ndie kavaa barakoa waumini hawajavaa ujue kuwa waumini wana imani kwa Mungu kuliko kiongozi wao!!!! Kiongozi anaamini kuwa akiwa kanisani kwenye nyumba ya Mungu MUNGU ANAWEZA MTUPIA CORONA WAKATI WAUMINI HAWAAMINI HILO
Yale yale ya mwendazake subiri ipite na wewe kushoto mbona hukwenda kumsaidia na kumwomba Mungu wake amwokoe ?kumbuka ni Mungu huyu huyu ameruhusu ELIMU NA MAARIFA VITAMALAKI,ILI WATU WASIFE HOVYO ni suala la muda tu wewe utapatika unamsikiliza huyo UNO Gwajima hamna kitu pale hakawii kuyaruka aliyoyasema.
 
Tumemsikia rais Samia akitamka, Gwajima hoyee…Gwajiboy hoyeee..!

Gwajima anajulikana kwa kukinzana na serikali ya Samia kuhusu chanjo ya korona na amekuwa akitoa kauli tata na hata kuwakeji viongozi wa serikali akiwepo waziri wa afya, spika na wengine.

Sasa rais anapomshabikia Gwajima haoni kwamba anapeleka ujumbe wenye utata kwa wananchi kuhusu chanjo na namna Gwajima anavyo behave?

Je rais anamuunga mkono Gwajima katika suala lipi hasa kwa hiyo hoyeeeeee….?!
 
Kwani hiyo hoyee , aliitoa katika munasaba gani?
 
Yale yale ya mwendazake subiri ipite na wewe kushoto mbona hukwenda kumsaidia na kumwomba Mungu wake amwokoe ?kumbuka ni Mungu huyu huyu ameruhusu ELIMU NA MAARIFA VITAMALAKI,ILI WATU WASIFE HOVYO ni suala la muda tu wewe utapatika unamsikiliza huyo UNO Gwajima hamna kitu pale hakawii kuyaruka aliyoyasema.
Nauliza Logic ya mapadre kuvaa barakoa wakati Kuna wasomi kibao kanisani kwao waliowazidi Elimu na exposure well travelled around the world kuliko wao kutovaa barakoa

Kuna tatizo mahali

Padre unaona na kibarakoa chake waumini wasomi na wenye exposure kubwa wanamuona Kama kituko tu
 
Tumemsikia rais Samia akitamka, Gwajima hoyee…Gwajiboy hoyeee..!

Gwajima anajulikana kwa kukinzana na serikali ya Samia kuhusu chanjo ya korona na amekuwa akitoa kauli tata na hata kuwakeji viongozi wa serikali akiwepo waziri wa afya, spika na wengine.

Sasa rais anapomshabikia Gwajima haoni kwamba anapeleka ujumbe wenye utata kwa wananchi kuhusu chanjo na namna Gwajima anavyo behave?
Je rais anamuunga mkono Gwajima katika suala lipi hasa kwa hiyo hoyeeeeee….?!
Awali Gwajima ni mbunge wa Kawe....mh.Rais alikuwa anampelekea heshima yake kama mwakilishi wao.....

Pili ,Mh.Rais ni "mwanademokrasia sana"....hwenda asifike "levels" za akina Hichilema et al ila kwa mazingira yetu Afrika anaendeleza kuonyesha UNAFUU NA UKOMAVU juu ya HOJA KINZANI.....

Mwenyezi Mungu amlinde na kumpa afya njema mh.Rais Samia Suluhu Hassan ,aaamin aaaamin🙏

#SiempreJMT
#KaziIendelee
 
Mapema Leo wakati Rais Samia yupo Tegeta jimbo la Kawe kwa Mchungaji Gwajima akiongea na wananchi na wakazi wa Kawe waliojitokeza kumsikiliza ameongea mengi lakini kati ya hayo ni pale aliposema "Gwajiboy oyeee, tunachanja, hatuchanji? Haya mheshimiwa gwajima endelea"

Kwa kauli hii Spika na Waziri wa Afya wako na hali gani kwa sasa?

Je, tuendelee kutegemea hatua zozote kutoka kwenye chama (CCM) dhidi ya Gwajiboy?
Na wananchi wanasema hatutakiiiii....
 
Hyo moja kwa moja mama Yuko pamoja na gwajima akubali akatae Mana kwa Hilo la chanjo kiukweli gwajima ameeleweka vizuri zaidi kwa uzito was hoja zake.
 
Anamuunga mkono ktk swala zima la kukataa chanjo,japo hawez kusema Waz kuwa chanjo si nzuri ila anasema ukihitaji ku chanjwa sawa na ukikataa sawa hakuna mtu anayekulazmisha
 
Back
Top Bottom