Tuwaepuke wanasiasa wanataka kutuletea ukabila kupitia uChifu

Hawa wameibuka kutoka wapi?
Na je wana impact gani katika maisha yetu kwa ujumla?
Sijawahi kusikia Chifu anatoa neno lolote kwenye jumuiya yetu
Hata kusifu au kukemea kitu ila ghafla tunasikia chifu wa huku na kupewa uchifu sijui nini
Mkuu hii ndio asili ya Africa ndiko babu zetu walipotoka kabla ya kutekwa akili na mzungu aliedhulumu haki yako..
 
Kila jambo huwa na kiasi, linapozidi huweza kubadili maana au kuharibu kabisa. Mfano, pete, ikizidi itakuwa Bangili.

Utamaduni ni jambo tofauti kabisa na uchifu. Uchifu unaweza kuwepo ndani ya utamaduni. Hapa ipo siku tutachanganyiwa mambo
 
Mkuu hii ndio asili ya Africa ndiko babu zetu walipotoka kabla ya kutekwa akili na mzungu aliedhulumu haki yako..
Hakuna kitu kama asili ya Afrika.

Kwanza neno lenyewe tu ni la Kiingereza CHIEF.

Chiefs ni watu waliosimikwa na mkoloni kwa ajili ya utawala wa kikoloni. Divide and rule tactics.

Waafrika walikuwa na viongozi wao lakini sio CHIFU. Hii CHIEF ni ya mzungu.

Na samia kaja na wachawi wake anaiwaita ati MACHIFU.
 
Ukiongelea uchifu unaongelea asili yetu..tamadunj..mila na miiko bila kusahau imani..wewe mlokole na mfia dini ambaye uliondolewa akili na utu wako kisa dini za wazungu na waarabu..ili wakutawale kuanzia akili na mali..unaona upuuzi kuenzi mila zako.

Bure kabisa..wewe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwanza uelewe kwamba CHEIF ni neno la kizungu.

Pili MACHIFU ni viongozi wa kiafrika waliowekwa na wazungu kwa ajili ya kazi za kikoloni.

Afrika haijawahi kuwa na CHEIF. Hii CHIEF ni invention ya mkoloni.

Hawa wa sasa hivi wanaoitwa MACHIFU ni wachawi wa samia.

Hakuna kitu kama CHEIF. Haya ni machawi tu yaliyotafuta chaka zuri la kujifichia.
 
Mkuu hii ndio asili ya Africa ndiko babu zetu walipotoka kabla ya kutekwa akili na mzungu aliedhulumu haki yako..

Sawa ni asili yetu lakini swali bado liko palepale mbona hatuwasikii kwenye jamii ?
Naomba unielewe hoja yangu
Kwanini hawana nguvu kwenye jamii yetu au ndio wamekuwa wale wa kuabudu mizimu tu
 
Kuna baadhi ya makabila mengi tu hapa Tanzania wakati wa ukoloni yalikuwa na machief (waliowekwa na wakoloni sehemu za pwani waliwata maakida, maliwali nak). Lakini baada ya uhuru Nyerere aka-mute haya mambo ya uchief (whether wa asili au wa kupewa na wakoloni). Sasa kama tukianza kuupa heshima sana hawa machief na kuufufua uchief kutoka makabulini ulikozikwa miaka 60 iliyopita tutaamsha dude moja baya saya huko mbeleni la ukabila na umajimbo.
 
CCM ni wakala wa shetani.
Hilo anayepinga na apinge,lakini ukweli unajulikana.
 
Huu uchifu wa sasa wa Samia, sio uchifu haswa. Ni vikundi vya wachawi wanaomsimika Hangaya kwa kumpa mamlaka na utii. Ni power transfer ama alama ya utii katika mamlaka za wachawi.
...Duh!....hizi ni siasa tu wakuu zisiwatishe... Tanzania yetu haiwezi kurudishwa kwenye Uchifu.
 
Nyerere aliwadanganya na kuwabrainwash msahau mila na tamaduni zenu ili awatawale bila usumbufu. Pia alipiga marufuku upinzani wa siasa kwa sababu hiyo hiyo. Mmefikia sehemu mnazikana na kuzikashifu jadi na tamaduni zenu.
 
Kama wameweka tegemeo lao kwa uganga, uchawi, ulozi, mizimu, matunguli na mauchafu kama hayo.........usitegemee jambo la kinyume chake. Kukimbiza tu moto unaoitwa mwenge ni ibada kamili ya kishetani, itakuwa kwenda kuzindikwa mauchawi na hao wanaoitwa machifu...........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…