Tuwaepuke wanasiasa wanataka kutuletea ukabila kupitia uChifu

Na hio ni sababu nyingine kuwa Samia haifai Tanganyika....yupo pale kuvuruga tu

Tanganyika (Tanzania bara) imetekwa, inaongozwa na raia wa kigeni (raia kutoka Zanzibar)
Kama ni ugenini basi ondoeni majeshi yenu ya vamizi. Mnasubiri nini?
 
Acha matusi mkuu....changia kistaarabu tu.

Hili suala linatumika kama mtaji wa kisiasa ila litavuruga taifa letu.
Nisameheni jamani nimechukizwa sana na haya maujinga ya kibibi cha kiarabu.
 
Afrika imekuwa na utaratibu huu wa utawala tangu enzi na enzi. Hizi tawala zilizoletwa na wakoloni hapa Afrika zina miongo michache tu iliyopita. Tusizidharau hizi taratibu zetu za jadi, kwa sababu ya taratibu za kigeni.
Asante sana...
 
[emoji817][emoji817][emoji817]
 
Taifa lisilo na utamaduni wake halisi ni taifa mfu!
 
Mama yenu content hana sasa atafanya nini kupata attention?

Preparation is everything, she wasn't well prepared.
 
CCM ni wakala wa shetani.
Hilo anayepinga na apinge,lakini ukweli unajulikana.
We watu wanazungusha kibatari nchi nzima kwa magharama kibao wakimini eti kibatari hicho kinamulika mpaka nje ya mipaka ya nchi kilete tumaini pale ambako hakuna tumaini, upendo pale penye chuki.....


Kwanini wasiwe wachawi?
 
Kwani kwasbb ni utaratibu wa tangu enzi km unavyosema ndo unaondoa ukweli kuwa ni ,uchawi,ushirikina,mizimu?
Hii haiondoi ukweli huu,haijalishi uliwekwa na kufuatwa na nani!
Haufai kenye nchi,tunamhitaji Mungu muumba wa mbingu na nchi sio machifu
Mkumbushe na kale kamshumaa wanakokazungusha nchi nzima wakikaabudu...
 
Hawa wameibuka kutoka wapi?
Na je wana impact gani katika maisha yetu kwa ujumla?
Sijawahi kusikia Chifu anatoa neno lolote kwenye jumuiya yetu
Hata kusifu au kukemea kitu ila ghafla tunasikia chifu wa huku na kupewa uchifu sijui nini
Kwenye uongozi wa nchi Kuna mengi Sana, tusije tukajiona tunajua sana. Mpaka rais kuamua kufanya alichofanya basi ujue kuna kitu kinawekwa sawa.
Uongozi sio rahisi tumtie Moyo mama atufikishe kwenye maendeleo
 
Kikubwa wakubwa wasijewaza kuwapa mavieite na watumishi kadhaaa, tutapigwa kama nchi. Wawakoge tu hivyooo maisha yaendeleee. Ila kwetu hatuna chief. Labda tuanzishe, na mwenye fursa ni mimi walau.
 

Afrika ilikuwa na viongozi wake wa kimila, waite jina unalopenda machifu, watwala, warola, musimba, ghokoi, thyaaa, thunaaa lolote upendalo ila viongozi walikuwepo.

Tz ya leo Katika vijiji vyote nje ya mfumo rasmi kuna wazee wa kijiji wanaoheshimika ambao hata serikali haiwatambui lakini jamii husika inawatambua na kuwaheshimu, nenda katika mabaraza ya vijiji utakutana nao, na hata madiwani sijui makatibu kata mpaka mabalozi sijui wenyeviti huwa wanawaona hawa wazee kwa ajili ya baraka zao ndipo wapiganie kuiwakilisha serikali humo kijijini.

Serikali imeona kuendelea kujifanya kuwa hawa wazee hawapo wakati jamii inawatambua na kuwaheshimu si busara ikaamua iwatambue. Hakuna tatizo katika hilo labda kama upo hapa TZ kwa ajili ya kupinga, na kama ni hivyo hata ungekuwa ni mkutano wa wachungaji na mashekhe ungepinga.
 
Zamani kwetu vijijini tukisikia anakuja waziri, achilia mbali rais, siku hiyo hakuna kusoma. Barabara zinafagiliwa na wanafunzi tunapangwa barabarani kumsubiri kuanzia asubuhi hadi atakapopita. Baadae tabia hii ilipigwa marufuku.
Nimeona sasa hivi kama vile inajirudia! Kukiwa na ndege inaleta watalii, wanakusanywa wamasai kiwanja ndege wawaimbie, tazama Tz Safari Channel kama huamini. Kwa makabila yenye tamaduni fulani nayo yanarundikana mahali kwa madhumuni ya kumvisha kiongozi vipande fulani vya ngozi, kumkabidhi rungu au mkuki...nk na kumzawadia jina na cheo cha uchifu. Sasa hivi imefikia mahali inachekesha, rais SSH, pamoja kuwa ni mwanamke kapewa uchifu na jina ambalo wala halitumii!! Kama sio kujipendekeza, Afrika mwanamke kufanywa Chifu wapi na wapi!
Ukifuatilia kwa undani inaweza gundua ni suala zima la kujipendekeza viongozi mbalimbali. Wanamuona rais kama mpenda sifa fulani nao wanajua ndo pakupitia kwa maslahi binafsi. Lakini pia, Inaelekea kwa sasa, tamaduni za kale zinafufuliwa ili zisaidie kuuwa vyama pinzani - atakapotembelea eneo hilo, kabila au jamii husika inahusishwa kumpamba mkuu huyo kwa mapambio ya kisiasa na inaelekea wanafanikiwa! - hatua 1 mbele, 1 nyuma, hatusongi mbele
 
Chifu ni neno lenye asili ya kiswahili???
 
Uchifu ni usultani. Tofauti ni majina tu.
 
Kikubwa wakubwa wasijewaza kuwapa mavieite na watumishi kadhaaa, tutapigwa kama nchi. Wawakoge tu hivyooo maisha yaendeleee. Ila kwetu hatuna chief. Labda tuanzishe, na mwenye fursa ni mimi walau.
Uchief unajua ni jina tu. Kwenu lazima kuna wale wazee wanaoaminika na kuheshimika ambao wanapelekewa suala lolote la kijamii kabla ya kufikishwa serikalini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…