Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Hivi yule jamaa FM academia walikuwa wakimuimba wanamuita Askofu wa kwanza. Alikuwa ni nani na kwa nn alijiita askofu? alikuwa ni askofu kweli au alikuwa na uhusiano gani na kanisa
Askofu wa kwanza ni jamaa ambaye alikuwa anafanyakazi BARAZA LA MAASKOFU Kurasini Daaah yeye ni mwendo wa HEINEKEN na kutunza Waimbaji
 
Kuna mwamba mwingine alitikisa sana maeneo ya Kariakoo, alikuwa mmoja wa vijana wenye majina makubwa kwenye soko la Kariakoo mle ndani karibu na duka la RTC marehemu Ford,hadi maalimu Gurumo akiwa Sikinde alimwimba.
Marhum Ford huyu alikuwa anapenda Starehe enzi za Late 70es to Early 80... Mtoto wake wa kumzaa anaitwa WABOGOJO kwenye video za Mr.Nice alikuwa anajikunja kunja alikuwa Monaco hivi karibuni yaani maisha yapo njema... Marhum Ford ameacha Ghorofa moja jembamba la Floor 2, ukiwa unatokea Mabatini Police kuelekea Afrika sana lipo kulia kwenye corner kabla ya Soko
 
Nimekulia Sinza ile ya akina Remi ndio wanatamba na Volkswagen imeandikwa.''mambo kwa soksi'' tulikuwa tunajua karibu vijana wote, hivi sasa Sinza imebadirika ni Sinza ya magorofa,mahoteli,vijana wote wa zamani ama wamerudisha namba kwa Sir God ama wamehamia sehemu nyingine nje ya mji,nyumba nyingi tulizokuwa tunapanga chumba kimoja kimoja zimebomolewa na kujengwa mahekalu, nakumbuka pale sinza madukani kulikuwa na mbabe wa kikurya Lucky baba yake alikuwa usalama wa Taifa,namkubuka bibi Uliye alikuwa na mabinti kama 10 hatari sana, nakumbuka akina Banza stone wakiwa wadogo wakicheza disco mtaani, nakumbuka Vatican City ikiwa hotel kumbwa Sinza na Simba walikuwa wakiweka kambi hapo, namkumbuka Fred Mwalasha akiwa ametoka Ulaya na mke wa kizungu ikawa yeye ni bangi na bangi na yeye hadi mwanamke wa kizungu akamkimbia, siku hizi sinza yamejaa madangulo na wazee wale waliokuwa na nyumba ambazo tulikuwa tumepanga nao hatunao duniani ila zile nyumba walizoacha watoto wao wameziuza kwa matajiri na kwenda kunywea pombe na kula sembe. Sinza ya sasa si ile tuliyokuwa tunaitimba, ama kweli siku hazigandi.
Mkuu Fred Mwalasha wa TOT ambaye ni Marhum?
 
Hapo samora nimeshatengeneza o level academic certificate 2 za marafiki kwenda Malaysia na India kusoma.
Kwao mambo safi ila vyeti hawana.
Kuna mzee mmoja niliwaunga nao wakapata vyeti kwa 30,000 kila kimoja.
Yule mzee yupo hadi leo pale anashinda bookshop.
Magu alipoingia aliwashughulikia sana,ingawa baadhi yao walimshinda! Enzi za Jakaya watu walikua wanapiga sana pesa,Mtaa wa Samora ndiyo kulikua na kila aina ya mihuri! Kuna msela mmoja alipewa pesa za kampuni x,akaweke kwenye account,bwana wewe jamaa akaenda kutengeneza fake slip ya bank,akapiga mpunga akawapelekea slip fake,ilikua jumamosi,jumatatu wanaenda kucheki mpunga,haupo,na jamaa kesharuka zake mbele! Wahindi walilia kama watoto! Zilikua 40M za Mauzo! Watu wahuni sana jamani
 
Marhum Ford huyu alikuwa anapenda Starehe enzi za Late 70es to Early 80... Mtoto wake wa kumzaa anaitwa WABOGOJO kwenye video za Mr.Nice alikuwa anajikunja kunja alikuwa Monaco hivi karibuni yaani maisha yapo njema... Marhum Ford ameacha Ghorofa moja jembamba la Floor 2, ukiwa unatokea Mabatini Police kuelekea Afrika sana lipo kulia kwenye corner kabla ya Soko
Shamsa Ford
 
Hapo samora nimeshatengeneza o level academic certificate 2 za marafiki kwenda Malaysia na India kusoma.
Kwao mambo safi ila vyeti hawana.
Kuna mzee mmoja niliwaunga nao wakapata vyeti kwa 30,000 kila kimoja.
Yule mzee yupo hadi leo pale anashinda bookshop.
Waliweza kwenda huko India?
 
Walienda.
Tumrpotezana.
Mmoja Malaysia mwingine India.
Sasa sijajua huko ikawaje lakini wa Malaysia alinicheki tena rafikiye alikuwa anataka cheti.
Ha ha ha ha! Hii story ni noma sana! Kuna msela ali disco chuo, tulikua nae mwaka mmoja! Basi siku moja akaniambia anaomba photo ya vyeti vyangu, kuna mchongo sehemu! Basi bwana nikatoa copy nikampa! Kumbe kaenda kwa wajanja wa town,wakabadili jina langu kwenye vile vyeti,wakaweka jina la jamaa,wakapiga muhuri wa moto na mambo kibao!

Siku moja jamaa namuona kwenye taasisi moja hivi private ni mtu mnene na anacheyo pale,basi jamaa nikamvutia sharubu,tukapanga tukutane sehemu,nikaenda kweli,tukapiga story na akaniambia ukweli wote kabisa,basi nikakaa zangu tu kimya,ni mwana sana hua tunatona pesa ndogo ndogo kwenye hizo shida na raha,jamaa ana pesa kunizidi hadi mimi
 
Hapo samora nimeshatengeneza o level academic certificate 2 za marafiki kwenda Malaysia na India kusoma.
Kwao mambo safi ila vyeti hawana.
Kuna mzee mmoja niliwaunga nao wakapata vyeti kwa 30,000 kila kimoja.
Yule mzee yupo hadi leo pale anashinda bookshop.
30,000 mwaka gani huu?? Jamaa yangu walimpiga 300,000 gamba la chuo
 
Dar ya Zamani ilikuwa ndogo ila mishe kibao,wajanja walikuwa wanapiga pesa Sana,serikali ilikuwa na mifumo dhaifu Sana.Wakati huo sera za uchumi wa serikali kuhodhi Mali zinakufa tunaingia uchumi wa soko huria watu walizipiga Sana.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
nakumbuka mwaka 2000 mpaka kuja 2005 kulikuwa na mabroo wanasukuma magari makubwa ya kutembelea ila kazi walizokuwa wanafanya hazieleweki kwa usahihi.

kuna broo mmoja ambaye kwa sasa ni marehemu(alijiua kwa kujipiga risasi na bastola), yeye alikuwa na kijiofisi chake cha ujanjaujanja kule nyuma ilipokuwa club billicanas


ndani ya kile kiofisi kulikuwa na meza moja, kiti chake cha kukalia, viti viwili vya wageni na desktop computer moja ndani ikiwa na OS ya window xp(ma IT technician wa zamani wanakumbuka).

huyu broo alikuwa anabadili gari za kutembelea mpaka mimi mwenyewe nikawa nashangaa, halafu gari zake zote kali zikiwa ktk condition nzuri unaweza dhani zimetoka moja kwa moja showroom.

wiki hii atakuja na pajero, baada ya wiki kadhaa utamuona na rav4, mara utamuona ana drive lexus nk. halafu yeye mwenyewe mda wote ni msafi. that was his lifestyle routine.

sijui ni akili ya utoto/ujana au nini,nikawa inspired na ile lifestyle yake, nikaamua kutafuta mbinu ya kumzoea maana jamaa alikuwa sio mtu wa mastori. akishuka tu kwenye gari, anazama ofisini.

pale ofisini kulikuwa na mpambe wake mmoja(siku hizi wanaitwa machawa) ambaye alikuwa anashinda mda mwingi.huyu mpambe na yeye kwa sasa ni marehemu.

nikamzoea huyu mpambe wake, halafu kila nikipata chance namuuliza kuhusu michongo anayopiga boss wake ili kama inawezekana aniajiri katika team yake.

yule mpambe akawa anacheka kwa dharau halafu ananiuliza "utaweza?". mimi kwa kujiamini nikawa namjibu ndio nitaweza. basi akaniambia ondoa shaka nitazungumza na broo ili tuone tunafanye.

baada ya kama mwez hivi,yule mpambe akaniambia tayari alishaongea na broo, twende ofisini nikakutambulishe.

tukafika, nikamsalimia, akaniambia dogo nimepata salamu zako, unataka nikupe kazi, nikamjibu ndio broo. akaniuliza swali lilelile nililoulizwa na mpambe wake, "utaweza?".

nikamjibu ndio nitaweza bro, halafu nikamuuliza kwani unataka kunipa kazi gani broo?. akanitazama kwa makini kama sikunde tano hivi, halafu akanijibu "kazi ya kusambaza unga".

roho yangu ikafanya paaa, wakati nikiwa kwenye mshtuko, yule broo akaendelea kuniambia anataka anipe kazi ya kusambaza unga ndani ya vitongoji vya jiji la dar, halafu niki improve atakuwa ananituma mikoani then niki improve zaidi atakuwa ananituma nje ya nchi.

those days nilikuwa bado chalii halafu mtoto wa kota, bado nipo home kwa baba na mama, sikuwa na knowledge kubwa kuhusu maisha.

lakini pia sikuwahi kuuona unga kwa macho wala kuuza, zaidi tu ya kusikia habari za madhara yake kwenye vyombo vya habari, kusikia mikasa mbalimbali ambayo wauza unga wanapitia na kuwaona mateja wakibembea ktk vichochoro vya kitaani kwetu.

hii ajira ambayo huyu broo alitaka kunipa kwa kweli ilinishtua sana,ni kitu kigeni kwangu. nikiwa kwenye mshtuko,akaniambia nenda kajifikirie,ukiwa tayari utanijulisha, ila usimwambie mtu, iwe siri yako.

ni kweli sikumshirikisha mtu, ila niliapa kutotafuta tena mazoea na yule bro. kila nikimuona ana park gari lake mimi namkwepa asinione.

yule mpambe wake kila mara alikuwa ananikumbusha kama bado najifikiria au vp. akawa ananiambia broo anasubiri jibu lako.

all in all, yule bro alikuwa ni ZUNGU LA UNGA wa level ya juu kabisa. may his soul continue to rest in peace.

sijataja jina lake kwa makusudi ili niwaachie
lesson wajanja wa zamani waunge dot vizuri. bila shaka watamjua.
 
Nimesoma Comments Baadhi sijamaliza Zote.. Sijaona Akitajwa OKIA JAMES hasa kwenye Nyimbo za FM Academia na Kwa Christian Bella nadhani... Huyu Vipi??
okia james alikuwa mfanyakazi wa bandari enzi za JK. alipoingia jiwe na ile operation yake ya kusafisha bandarini, operation ikamkumba na okia.

huyu alikuwa ni mtu wa karibu na mmiliki wa FM academia, mzee martin kasianjo(RIP).

inasemekana kwa sasa yupo kwao mbeya.ila financially bado yupo vizuri.

wajuzi watafunguka zaidi.
 
Back
Top Bottom