Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

nakumbuka mwaka 2000 mpaka kuja 2005 kulikuwa na mabroo wanasukuma magari makubwa ya kutembelea ila kazi walizokuwa wanafanya hazieleweki kwa usahihi.

kuna broo mmoja ambaye kwa sasa ni marehemu(alikufa kwa kujipiga rasasi), yeye alikuwa na kijiofisi chake cha ujanjaujanja kule nyuma ilipokuwa club billicanas

ndani ya kile kiofisi kulikuwa na meza moja, kiti chake cha kukalia, viti viwili vya wageni na desktop computer moja ndani ikiwa na OS ya window xp(ma IT technician wa zamani wanakumbuka).

huyu broo alikuwa anabadili gari za kutembelea mpaka mimi mwenyewe nikawa nashangaa, halafu gari zake zote kali.

wiki hii atakuja na pajero, baada ya wiki kadhaa utamuona na rav4, mara utamuona ana drive lexus nk. na gari zake zote zilikuwa kwenye condition nzuri. halafu yeye mwenyewe mda wote ni msafi. that was his lifestyle routine.

sijui ni akili ya utoto/ujana au nini,nikawa inspired na ile lifestyle yake, nikaamua kutafuta mbinu ya kumzoea maana jamaa alikuwa sio mtu wa mastori. akishuka tu kwenye gari, anazama ofisini.

pale ofisini kulikuwa na mpambe wake mmoja(siku hizi wanaitwa machawa) ambaye alikuwa anashinda mda mwingi.huyu mpambe na yeye kwa sasa ni marehemu.

nikamzoea huyu mpambe wake, halafu kila nikipata chance namuuliza kuhusu michongo anayopiga boss wake ili kama inawezekana aniajiri katika team yake.

yule mpambe akawa anacheka kwa dharau halafu ananiuliza "utaweza?". mimi kwa kujiamini nikawa namjibu ndio nitaweza. basi akaniambia ondoa shaka nitazungumza na broo ili tuone tunafanye.

baada ya kama mwez hivi.,yule mpambe akaniambia tayari alishaongea na broo, twende ofisini nikakutambulishe.

tukafika, nikamsalimia, akaniambia dogo nimepata salamu zako, unataka nikupe kazi, nikamjibu ndio broo. akaniuliza swali lilelile nililoulizwa na mpambe wake, "utaweza?".

nikamjibu ndio nitaweza bro, halafu nikamuuliza kwani unataka kunipa kazi broo. akanitazama kwa makini kama sikunde tano hivi, halafu akanijibu "kazi ya kusambaza unga".

roho yangu ikafanya paaa, wakati nikiwa kwenye mshtuko, yule broo akaendelea kuniambia anataka anipe kazi ya kusambaza unga ndani ya vitongoji vya jiji la dar, halafu niki improve atakuwa ananituma mikoani then niki improve zaidi atakuwa ananituma nje ya nchi.

those days nilikuwa bado chalii halafu mtoto wa kota, bado nipo home kwa baba na mama, sikuwa na knowledge kubwa kuhusu maisha.

lakini pia sikuwahi kuuona unga kwa macho wala kuuza, zaidi tu ya kusikia habari za madhara yake kwenye vyombo vya habari, kusikia mikasa mbalimbali ambayo wauza unga wanapitia na kuwaona mateja wakibembea ktk vichochoro vya kitaani kwetu.

hii ajira ambayo huyu broo alitaka kunipa kwa kweli ilinishtua sana,ni kitu kigeni kwangu. nikiwa kwenye mshtuko,akaniambia nenda kajifikirie,ukiwa tayari utanijulisha, ila usimwambie mtu, iwe siri yako.

ni kweli sikumshirikisha mtu, ila niliapa kutotafuta tena mazoea na yule bro. kila nikimuona ana park gari lake mimi namkwepa asinione.

yule mpambe wake kila mara alikuwa ananikumbusha kama bado najifikiria au vp. akawa ananiambia broo anasubiri jibu lako.

all in all, yule bro alikuwa ni ZUNGU LA UNGA wa level ya juu kabisa. may his soul continue to rest in peace.

sijataja jina lake kwa makusudi ili niwaachie
lesson wajanja wa zamani waunge dot vizuri. bila shaka watamjua.
Utaweza kazi??

Huu mkasa unanikumbusha miaka ya 2008 baada yakumaliza chuo,nipo zangu kitaa sina mbele wala nyuma,nipo zangu pande za Bahari Beach,natembea kwa mguu kurudi home kunduchi mtongani, Harrier old model,hiyo inapaki kwa mbele yangu,kioo kikashushwa,kucheki ni mwana mmoja tumesoma nae chuo,vipi kaka wapi,naenda home,kwa mguu,ndiyo kaka sina nauli,twende nikusogeze,ndani ya gari maongezi ya jamaa kwenye simu ni USD 500 kwenda mbele,kaka nashuka hapa,twende tu hadi town Kwan una shughuli gani home sasa hivi?? Au chukua hii 50,000 utanicheki uje nilipo!

Baada kama ya siku mbili, hivi nikamcheki,jamaa akajibu kindly text,kaka Mimi flan,ohhh sasa mbona hukunipigia siku ile? Kaka mambo yalikua mengi, okay chukua bajaji ndoo Bahari Beach Mtaa x,bajaji wanapajua!

Kweli huyu hadi huo mtaa,fika pale ule Mtaa upo kimya,hakuna vurugu kabisa,nikaenda hadi kwenye ile nyumba,nikamkuta msanii wa bongo flavor jina lake x, ni jina maarufu sana Mkoa flani hivi,basi tukawa tunapiga story pale, jamaa anakula zile sigara kubwa za watu wenye pesa,pembeni ana warembo 2,wakiwa nusu naked,pombe mezani zote za bei ya juu!

Basi sababu kipindi kile sikua nakunywa,tukawa tunapiga tu story na jamaa yangu,jamaa akasema nataka nikupe deal la pesa,kwa shauku ya haraka sana nikasema na Mimi si nitakua na maisha kama ya huyu jamaa,nikasema poa! Lakini akauliza tena swali,utaweza? Nikasema kwani kazi gani ambayo kidume kama Mimi nishindwe kuifanya??

Jamaa akasema utaweza kusukuma powder,sikuelewa hii Kodi,nikasema ndiyo naweza,wale wadada wakacheka sana,mwishowe wakasema unaweza uza unga?? Aiseeee! Nilishituka,jamaa akasema huwezi,ushafeli tayari,basi jamaa akasema hii ni Siri,wewe ni mtu wa kwanza kujua nafanya kazi gani,so ukimwambia mtu mwingine,kazi nnazofanya,nitakupoteza,wale warembo,wakawa wanampapasa tu jamaa mgooni!

But miaka ya 2013 hivi walishikwa huko mikoa ya kusini na jamaa mmoja alikua Master sana kwenye michongo hiyo,jamaa hadi leo yupo nyuma ya nondo,kuna demu mmoja siku moja nilikutana nae pande za fish fish masaki,alinipa full details nilibaki mdomo wazi tu aiseeee!
 
Yes sema gharama ya kutajwa na bendi mara nyingi inakuja hapo unapolazimika kutunza fedha kwa sababu unayoiona kwamba usipomtunza anayekupaisha utakuwa unamchosha bure...wale mapedeshee wanaotajwa na kutunza wanatoa zaidi ya millioni hata tatu kwa siku kwa ajili ya kutunza inabidi uwe mzuri hasaa kifedha...DRC congo huko ndio watu wanatunza hadi millioni 20 kwa siku na ukiona mtu katajwa kwenye wimbo ukue katoa si chini ya millioni 5 atajwe
Yeah huko DRC wanaita mabanga
 
Utaweza kazi??

Huu mkasa unanikumbusha miaka ya 2008 baada yakumaliza chuo,nipo zangu kitaa sina mbele wala nyuma,nipo zangu pande za Bahari Beach,natembea kwa mguu kurudi home kunduchi mtongani, Harrier old model,hiyo inapaki kwa mbele yangu,kioo kikashushwa,kucheki ni mwana mmoja tumesoma nae chuo,vipi kaka wapi,naenda home,kwa mguu,ndiyo kaka sina nauli,twende nikusogeze,ndani ya gari maongezi ya jamaa kwenye simu ni USD 500 kwenda mbele,kaka nashuka hapa,twende tu hadi town Kwan una shughuli gani home sasa hivi?? Au chukua hii 50,000 utanicheki uje nilipo!

Baada kama ya siku mbili, hivi nikamcheki,jamaa akajibu kindly text,kaka Mimi flan,ohhh sasa mbona hukunipigia siku ile? Kaka mambo yalikua mengi, okay chukua bajaji ndoo Bahari Beach Mtaa x,bajaji wanapajua!

Kweli huyu hadi huo mtaa,fika pale ule Mtaa upo kimya,hakuna vurugu kabisa,nikaenda hadi kwenye ile nyumba,nikamkuta msanii wa bongo flavor jina lake x, ni jina maarufu sana Mkoa flani hivi,basi tukawa tunapiga story pale, jamaa anakula zile sigara kubwa za watu wenye pesa,pembeni ana warembo 2,wakiwa nusu naked,pombe mezani zote za bei ya juu!

Basi sababu kipindi kile sikua nakunywa,tukawa tunapiga tu story na jamaa yangu,jamaa akasema nataka nikupe deal la pesa,kwa shauku ya haraka sana nikasema na Mimi si nitakua na maisha kama ya huyu jamaa,nikasema poa! Lakini akauliza tena swali,utaweza? Nikasema kwani kazi gani ambayo kidume kama Mimi nishindwe kuifanya??

Jamaa akasema utaweza kusukuma powder,sikuelewa hii Kodi,nikasema ndiyo naweza,wale wadada wakacheka sana,mwishowe wakasema unaweza uza unga?? Aiseeee! Nilishituka,jamaa akasema huwezi,ushafeli tayari,basi jamaa akasema hii ni Siri,wewe ni mtu wa kwanza kujua nafanya kazi gani,so ukimwambia mtu mwingine,kazi nnazofanya,nitakupoteza,wale warembo,wakawa wanampapasa tu jamaa mgooni!

But miaka ya 2013 hivi walishikwa huko mikoa ya kusini na jamaa mmoja alikua Master sana kwenye michongo hiyo,jamaa hadi leo yupo nyuma ya nondo,kuna demu mmoja siku moja nilikutana nae pande za fish fish masaki,alinipa full details nilibaki mdomo wazi tu aiseeee!
Maisha ni fumbo.. Ukiona umeingia utu uzima bill cash cash na vyombo vya dola. mshukuru Mwenyezi Mungu. Maisha ya kitaa ni changamoto. Wengi tunateswa na tamaa. biashara ya unga imewaumiza wengi.

talk of unga, hivi akina Shamimu Mwasha bado wapo nyuma ya nondo? jamani tupambane lakini tuwe na staha ya kutafuta pesa. Mimi Yule binti nilikuwa namuona Ana uwezo wa kutafuta bila kugombana na dola…
 
kuna kipindi fulani wakati mziki wa dansi upo kwenye chati, nilijenga ukaribu na baadhi ya wanamuziki wa kicongo hapa nchini. wapo ambao bado ni rafiki zangu mpaka sasa.

mwanamuziki ambaye alikuwa anataja jina langu siku hiyo alikuwa ni rafiki yangu sana, alikuwa ananitaja kama sehemu tu ya kudumisha urafiki wetu, ndio maana akaona hakuna haja ya mimi niwe nanyanyuka kila mara kwenda stejini kumtunza.

kuhusu villapark ni kweli haipo tena, kama kumbukumbu zangu zipo sawa, mara ya mwisho kwa hii lounge kuwa active ni 2019 au mwanzoni mwa 2020.

hii lounge licha ya kwamba haipo tena, imebeba kumbukukumbu nzuri kuhusu mimi na misele yangu ya jiji la mwanza. kila nikifika mwanza, picha ya kwanza inayonijia kichwani ni villapark.

sitosahau rosti ya sato na sato wa kuoka kwenye foil niliokuwa nakula pale, it was superb.

View attachment 2288603View attachment 2288605View attachment 2288604View attachment 2288606View attachment 2288608
View attachment 2288640View attachment 2288641View attachment 2288642View attachment 2288644
Jamaa ameshaifungua tena villa yake
 
Marhum Ford huyu alikuwa anapenda Starehe enzi za Late 70es to Early 80... Mtoto wake wa kumzaa anaitwa WABOGOJO kwenye video za Mr.Nice alikuwa anajikunja kunja alikuwa Monaco hivi karibuni yaani maisha yapo njema... Marhum Ford ameacha Ghorofa moja jembamba la Floor 2, ukiwa unatokea Mabatini Police kuelekea Afrika sana lipo kulia kwenye corner kabla ya Soko
Kwahiyo alikua mzee wa twn,nyumba bado ipo au wameuza watoto
 
Maisha ni fumbo.. Ukiona umeingia utu uzima bill cash cash na vyombo vya dola. mshukuru Mwenyezi Mungu. Maisha ya kitaa ni changamoto. Wengi tunateswa na tamaa. biashara ya unga imewaumiza wengi.

talk of unga, hivi akina Shamimu Mwasha bado wapo nyuma ya nondo? jamani tupambane lakini tuwe na staha ya kutafuta pesa. Mimi Yule binti nilikuwa namuona Ana uwezo wa kutafuta bila kugombana na dola…
Bado wapo nyuma ya nondo mkuu! Maisha ni changamoto sana
 
Chief kiumbe yupo wapi siku hizi?

Na yule mcomoro Said Comorien naye alirudi kwao nini siwasikii kabisa.
 
Haruna Fagason..huyu mwamba kila nyimbo aliyoimba gwiji na nguli wa muziki wa dansi Tanzania, Tx Moshi William lazima amtaje. Kwasisi wapenzi kindakindaki wa Msondo tunalitambua hili jina
 
Walienda.
Tumrpotezana.
Mmoja Malaysia mwingine India.
Sasa sijajua huko ikawaje lakini wa Malaysia alinicheki tena rafikiye alikuwa anataka cheti.
Mimi kuna mtu aliwahi kuomba vyeti vyangu vya form 4, lakini cheti kina picha sikuweza kukubali,
Kuanzia 2008 vyeti vina picha
 
Back
Top Bottom