hapana sio kweli, tusichanganye madesa. jose kongolo na sadam hussein ni watu wawili tofauti.
Najikita kumuelezea zaidi Jose Kongolo.
Jose Kongolo ni mwanamama maarufu wa kicongo na mfanyabiashara anayemiliki mgahawa mkubwa na lounge jijini paris, pia ni mdau mkubwa wa mziki wa rhumba.
jina lake limetajwa sana na wanamuziki wa kicongo wakitamka "JOSÉ KONGOLO FBI MIBEKO LA LOI".
wengi kwa kutokujua wemekuwa wanachanganya jina lake na jina la Kongulu Mobutu "Sadam Hussein", ambaye alikuwa mtoto wa Mobutu Sese Seko.
mgahawa anaoumiliki huyu mama umekuwa ni meeting point ya wacongo wengi ndani ya ufaransa.
kwanini wanamuita FBI mibeko la loi au kwa kiswahili FBI wa Yesu?(wanaojua kikongo vizuri watasaidia kutafsiri). ni kwasababu Jose Kongolo ni born again christian au tuseme mlokole.
licha ya kwamba ni mfanyabiashara, pia ana miliki kanisa lake pale paris. kanisa hili limekuwa msaada mkubwa kwa vijana wa kicongo waliopoteza matumaini ya kimaisha ndani ya ufaransa na nchi nyingine za europe.
yeye huwapokea, huwafanyia counseling, huwapa chakula,maradhi, hawachangia michango mbalimbali ya kibinadamu na baadae huwashawishi waokoke.
baadhi ya wanamuziki wameokoka baada ya kushawishiwa na huyu mama. wengine huwa wanaendelea na career yao ya mziki huku yeye akiendelea kuwapa support.
hapo ndio umaarufu wake unapokuja na ndio maana jina lake linatajwa sana na wanamuziki wa rhumba
kuhusu Kongulu Mobutu "Sadam Hussein".
Kongulu Mobutu almaarufu sadam hussein, huyu sitaki kumuelezea kwasababu hapa JF zipo nyuzi kadhaa ambazo amezungumziwa kiundani. ni wewe tu kuzipitia ili kuongeza knowledge.
nakuwekea link hapa chini:
Mjue Saddam Hussein wa Zaire
Fahamu machache kuhusu special presidential division: Kikosi maalumu kilichomlinda Mobutu Seseseko enzi za utawala wake
katika picha huyu ndio mamaa JOSÉ KONGOLO FBI MIBEKO LA LOI.
View attachment 2280509