Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

rukia na okia ni watu wawili tofauti.

rukia james ni mwanamke na okia james ambaye nilikuwa namzunngumzia mimi ni mwanaume.

ni kweli,rukia james ni moja ya jina ambalo lilikuwa common sana kutajwa na wanamuziki wa rhumba. lakini na jina la okia james(mwanaume), naye alitajwa sana.

maelezo yangu hapo juu kuhusu okia james, yanashabihiana kidogo na maelezo ya mdau hapa chini. nilisema kwa sasa okia james anaonekana mitaa ya mbeya.
Nimekuelewa
 
Hilo lina kweli 100%.

But don't be fooled by their silence, wapo ambao bado wana mzigo wa kutosha ila wameamua kwenda lowkey kuzuga mamlaka. Hawataki tena mambo ya kutajanatajana kwenye mziki.
Watu wanacheza na nyakati wanajiongeza[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji1787]Enzi ya JK watu walikuwa na freedom sana hakukuwa na mambo ya kutafutana majumbani kuulizana hela umepata wapi.
 
Umemsahau Papaa Shabani Ngalawa (R.I.P). Huyu alikua mwalimu mzuri wa tution miaka ya 1995-2001 hizi za shule ya msingi. Miaka ambayo mtaa mzima unakuta waliofaulu la saba ni wawili au hakuna na katika hao waliofaulu wote walisoma tution kwa huyu mwalimu shabani..

Nakumbuka alichukuaga mkopo wa milioni 200 lengo likiwa kujenga shule yake binafsi maeneo ya kibamba. Akaweka rehani nyumba na shamba lake. Mwisho wa siku pesa zote zikaishia kuwatunza akina ally choki na mwinjuma muumini ktk mabendi na nyingine akanunulia toyota baloon. Benki ikaja ikapiga mnada nyumba na shamba wakamfilisi mazima.

Alitajwa sana kwenye nyimbo za Mwinjuma hasa ile ya Kilio cha Yatima. Alikuja kuugua mda mrefu na aliisha akawa kama mtoto. Amefariki akiwa hana hata pa kulala. Sad!
Nmejikuta nacheka tu
 
Haaaahaha kwani huyo Kapuya mwenyewe pamoja na uprofesa ni mtu mwenye akili kweli??? Huyo Kapuya watakua ni wale watu toka sekondari hadi chuo kikuu ni watu wa madesa na connection mwisho wake wanatusua kibahati lakini upstairs ni zero. Simba huzaa Simba hata siku moja hawezi zaa mbuzi.
Naomba kujua Professor Kapuya ni Professor wa nini hapa nchini?
 
1.Fikiri Madinda
2.Pedeshee Mudi Nondo
3.Moris Mariaga
Hapa pedeshee kidogo ni #3,hao 1&2 walikua ni janja janja tu,tuliowahi kuishi nao Sinza_Madukani tunawajua vizuri
Huyo Mudi Nondo BSS aliyoshinda Jumanne Iddi,nafikiri ilikua ndio BSS ya kwanza,siku ya Fainali aligawa pesa hatari,cha kushangaza nyumba aliyopanga ilikatiwa umeme kwa kushinda kulipa bili kwa wakati(enzi hizo hakuna LUKU) [emoji38][emoji38][emoji38]
Fikiri Madinda aliishi kwenye upangaji na nyumba ya kawaida mno tofauti na jina alilokuwa nalo mjini.
Moris Mariaga ni Mkwere mwenye bar zake za kutosha mitaa ya Manzese, Tandale na Sinza...hatari sana
 
Kuna mwamba mwingine alitikisa sana maeneo ya Kariakoo, alikuwa mmoja wa vijana wenye majina makubwa kwenye soko la Kariakoo mle ndani karibu na duka la RTC marehemu Ford,hadi maalimu Gurumo akiwa Sikinde alimwimba.
Baba yake na Shamsa Ford huyo na Wakumojo
 
kuna rhumba moja kali sana ya madilu system inaitwa vice versa.

ktk verse ya kwanza ya track hiyo, madilu anataja jina la Teodoro Obiang Nguema. huyu ni mtoto wa rais wa equatorial guinea, mzee Teodoro Obiang Nguema Mbasogo.

Teodoro au maarufu teddynguema kama anavyofahamika kwenye social media, kwa sasa ni makamu wa rais wa taifa hilo.

maisha anayoishi huyu teddy yanaakisi kwa kiwango kikubwa maisha halisi ya kipedeshee, ana pesa nyingi sana za kula bata.

anasafari maeneo mbalimbali duniani ktk kujipa raha na huwa hafichi kitu, picha zake za kula bata huwa anaziweka kwenye kurasa zake za social media.

baba yake yupo ktk orodha ya marais ambao wapo madarakani kwa mda mrefu duniani. yeye na baba yake wanaitawala equatorial guinea kwa mkono wa chuma kweli kweli.

Vice versa | Boomplay Music



View attachment 2279163View attachment 2279164View attachment 2279165View attachment 2279168
Jamaa nasikia Hana mke yupo single tu
 
Nilisikia huyu mwamba mali zake zimekamatwa na serikali ya Marekani pamoja na Ufaransa na pia ni kama yupo kizuizini huko Ufaransa,huyu mwamba ndiye amasemekana alinunua ile glove maarufu yenye vimulimuli vya dhahabu aliyokuwa anaivaa Wacko Jacko.
Ufaransa na Marekani walisanda, aliwafungulia kesi ya Madai ya kumdhalilisha kwa kukamata Mali zake akatoa ushahidi ulionyooka...wakarudisha Mali zake zote na kesi akaifuta
 
Shaban Ngalawa nilisomava tuition kwake wiki moja tu.

Pale mitaa ya kimara resort (vidudu)na tulikuwa tunafanya mitihani kwake enzi hizo.

Alikuwa mfupi hivi anapiga panki kifuani anaacha vishikizo viwili juu wazi na cheni inabembea na bonge la mustache.
Dah umenikumbusha zamani Sana, Enzi Hizo nikiwa darasa la 7 mwaka 1997 pale Ubungo NHC kila Jumamosi lazima tupande UDA kwenda Kimara Resort opposite na Ile Sheli kupiga paper zake za kila wiki ili tutusue paper za NECTA

ANDREW SEKIDEA ambaye alikuwa Twanga Pepeta ndiyo alimuunganisha kwa kina Choki, kuna kipindi alikuwa Tour Guide huko Arusha sijui ikawaje, sikuwahi jua kuwa alishafarikigi
 
Yupo hai ni dereva wizara ya kilimo. Zamani alikua dereva Tamisemi.
Sasa hivi Fikiri Madinda ni Dereva wa Serikali na anaishi Dodoma na ni mwenyeji wa Dodoma ni Mrangi lakini Mama yake NI Mgogo. Fikiri Madinda kwa Sasa ni Dereva wa Naibu Waziri wa Wizara Mojawapo Serikalini lakini Siyo Kilimo.

Aliyekuja kuwa Naibu Waziri wa Kilimo wa Kwanza baada ya Bashe kupandishwa cheo na kuwa Waziri kamili wa Kilimo ndiyo huyo anayemuendesha kwa Sasa hata baada ya huyo Naibu Waziri kuhamishwa Wizara alihama na Dereva Fikiri Madinda kutoka Wizara ya Kilimo na kwenda nae Wizara mpya aliyoteuliwa
 
Sasa hivi Fikiri Madinda ni Dereva wa Serikali na anaishi Dodoma na ni mwenyeji wa Dodoma ni Mrangi lakini Mama yake NI Mgogo. Fikiri Madinda kwa Sasa ni Dereva wa Naibu Waziri wa Wizara Mojawapo Serikalini lakini Siyo Kilimo.

Aliyekuja kuwa Naibu Waziri wa Kilimo wa Kwanza baada ya Bashe kupandishwa cheo na kuwa Waziri kamili wa Kilimo ndiyo huyo anayemuendesha kwa Sasa hata baada ya huyo Naibu Waziri kuhamishwa Wizara alihama na Dereva Fikiri Madinda kutoka Wizara ya Kilimo na kwenda nae Wizara mpya aliyoteuliwa
Mkuu wizara moja wapo ni ipi hiyo wakati anajulikana yuko Tamisemi. Unaficha ficha nini sasa, ama unaona ni jambo la siri saaana.
 
Back
Top Bottom