Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

nahisi kwa sasa atakuwa anacheza near 50...ameshakuwa kibibi aka juve.


ila mimi watoto wa mzee mengi(ukiondoa marehemu mutie), huwa siwaelewi.

yule kakaake regina jamaa wa kuitwa abdiel nahisi na yeye ni walewale wa upande wa rainbow(sijui kwanini namuwazia hivi,Mungu atanisamehe).

kinachowasadia ni wasiri sana wa mambo yao, hawajichanganyi kwenye mikusanyiko mikubwa ya starehe, halafu hawatumii social media.
Teh teh

Ova
 
Aisee..
Umenikumbusha Kenny Nyembera , wakati ule wa local gym sio mchezo kwa kina Marlon Linje (Mzee ya Gitaa)
Kweli baadae ilikuwa daah.... changamoto za maisha hizi....

Halafu Patrick Nyembera alikuwa multitalent nakumbuka enzi za Don Bosco, Mpira yupo na alikuwa anaupiga mwingi...
UkIja Basketball yupo na mpaka kufika Pazi na michezo mingine mingi tu alikuwa mkali....
Keny nyembera enzi hizo tulikuwa tunapiga naye sana tizi alikuwa na mwili jumba,sema jamaa madawa yalimuaribu sana hapo badaye(am sorry to say this)
Alafu keny alikuwa anatoka na dada mmja enzi hizo alikuwa mke wa mzungu mmja aliyekuwa na biashara kubwa tu bongo,alikuwa kama dada yetu wa mjini(smbdy A.mbonde)
Dem alikuwa akivuta mpunga kwa mme wake anaenda jirusha na k.nyembe kula bata sana
Enzi hizo dem anapush Nissan patrol
Wale wajinga walikuwa maisha sana
Mm mwenyewe nlikula sana hela za yule dada si unajua mambo ya kujiongeza
Ona sasa wanawake walivyokuwa fyatu, dem alipokolea sana kwa k.nyembe si akawa anataka talaka
Akajikanyaga alipoomba talaka kwa mme mzungu yule eti aliomba hela tu nahsi ilikuwa mln 80....yule mzungu faster aka file papers nk ili process ifanyike ,akampatia hela wakaachana
Maaana yule mme wake alijua labda mke atataka mgawanyo wa Mali
Ebwana walipoioata hela wacha wait umbue na k.nyembe
Maana wote walikuwa wanatumia ile kitu...mwisho wa siku waliishi maisha ya kusikitisha sana
Kimbembe sasa tuliyokula hela zake si mizinga tukikutana usipo mpa lawama [emoji1]

Ova
 
hili lina ukweli 100%.
kwanini kwa familia tajiri za kiarabu hali hii haipo?. kwa mfano yusup bakhresa, mtoto wa mzee bakhresa alioa mapema sana na mpaka sasa yupo na mkewe.
Uzi huu umenifanya nmkumbuke dada yetu Amina mongi (RIP)
Na imani angekuwepo mpaka leo angekuwa mtu fulani
Nakumbuka dstv inaingiaingia bongo
Na muktichoice wao ndy walikuwa wa kwanzakwqnza kuipigia promo
Nmepiga naye sana nyagi kinywaji chake....

Ova
 
Aisee ktk jamii ambazo hua wanawahi kuoa hua Ni waarabu na hii Ni Hadi kwa familia zao za matajiri,kijana hata wa early 20's unakuta ameoa afu fresh tu Maisha yanaendelea, nadhani labda Ni mambo ya tamaduni mkuu.
Yap waarabu wahindi kuoa ni mapema sana naona hawajamezwa sana na tamaduni za magh
 
Awali ya yote nitangulize angalizo kwa vijana ambao maturity stage imewakuta miaka hii ya mitandao ya kijamii. Itabidi msome kimyakimya huku mkiwa mmeshika peni na karatasi kuchukua notes.

Huu uzi ni wa sisi ma-seniors, maudhui yake yatagusa zaidi vijana wenzangu ambao maturity liwakuta kuanzia late 90s to early 2000s.

Mwaka 2002 mpaka 2012, mziki wa dansi ulikuwa upo kwenye prime time.

Kwa uchache tu, band zilizotamba ni FM Academia, Akudo Impact, Twanga Pepeta na Diamond Musica. Zingine zilikuwa zinaibuka na kupotea ndani ya muda mfupi.

Umaarufu wa hizi band ulienda sambamba na trend ya wanamuziki kutaja majina ya baadhi ya watu kwenye mashairi yao.

Majina ya hawa watu yalivuma na kuwa maarufu kuliko sura zao kwasababu miaka ile kulikuwa hakuna social platform za ku-share picha na video kama ilivyo hivi sasa.

Kutokana na kujichanganya kwangu ukijumlisha na ujanja wangu wa kimjini mjini wa miaka ile, nilifanikiwa kufahamiana na baadhi mapedeshee au wazee wa mujini ambao majina yao yalikuwa yanatajwa kwenye mziki wa dansi.

Nitataja ninaowakumbuka na wewe ongeza wa kwako.

Naandika majina yao kama yalivyokuwa yanatamkwa kwa mbwembwe na wanamuziki.

Kwa mfano kama mtu alikuwa anaitwa John, wanamuziki walikuwa wanatamka papaa John Young Millionaire Muzee ya ma-Range Rover[emoji3][emoji3].

Haya twende kazi:
Pedeshee Mychoice na kati ya Mbeya
:
huyu sijui alikuwa anapiga mishe gani huko Mbeya, watu wa Mbeya mtatusaidia.

Braza K na kati ya Tunduma:
Watu wa Tunduma mtatusaidia kutujuza kuhusu huyu jamaa, alivuma sana.

Mamaa Rukia Soloon:
Huyu bibie namfahamu, ana saloon yake ya kike mitaa ya Mikocheni barabara ya Rose Garden. Those days she was very pretty, kwa sasa utu uzima umemchukua.

Mamaa Dotnata Decoration:
Bila shaka wengi mnamkumbuka, aliwahi kuwa muigizaji maarufu kupitia ITV, baadae akaingia kwenye ujasiriamali wa kutoa huduma za decoration and catering. shughuli hizi zilimpatia mafanikio sana. sijui kwa sasa yupo wapi huyu mama. FM Academia waliwahi kumtungia wimbo wenye jina lake.

Mamaa Juddy Moshi:
Alikuwa mmiliki wa band ya Daimond Musica kwa financial support ya mshua mmoja ambaye alikuwa ni MD wa Yellow Pages, watu wa zamani wanaelewa. Juddy alikuwa mrembo si kitoto, kwa sasa umri wake umesonga mbele.

Pedeshee Akayesu Ndama Mutoto ya Ng'ombe:
Sina haja ya kumuelezea, ni mtu maarufu wa misimu yote. Wajanja wa mujini watamuelezea zaidi. Jina lake lilitajwa sana kwenye nyimbo za dansi zilizovuma.

Young Millionaire Bill gate Muzamir Katunzi:
Christian Bella aliwahi kutunga mpaka wimbo wenye jina hilohilo la Muzamir Katunzi. I don't know him personally, but it's told he was financially successful.

Papaa Msofe Chuma cha Reli hakishiki Kutu.
Sina haja ya kuandika mengi kuhusu umaarufu wa Papaa Msofe. Itoshe tu kusema jina lake liliimbwa sana halafu ni wachache waliokuwa wanajua sura yake. Walianza kuiona kwenye media alipokuwa anahudhuria viunga vya mahakama kujibu kesi yake.

Papaa Martin Kasianju.
Ni marehemu kwa sasa, huyu mshua ndio alikuwa mmiliki wa Band ya FM Academia. Nilikuwa namfahamu personally. licha ya kwamba alikuwa ni mjasiriamali na muajirwa Serikalini, pia alikuwa ni Senior Officer wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Andrew Traders na Kariakoo Big Supply: Jamaa alikuwa ni mfanyabiashara wa kuuza tairi za gari Mtaa wa Agrey Kariakoo huku akipiga michongo yake ya "general supply". Watu wa mujini wa zamani wanaelewa vizuri maana ya kampuni kusajiliwa kwa jina la general supply. Katika biashara ya kuuza tairi, alishirikiana na kaka yake, ila yeye akawa maarufu zaidi na akaaminika na wadau.

Kinje Mutoto wa Mujini:
Najua wengi mnamfahamu na zile deal zake alizokuwa anapiga. sina haja ya kumuelezea zaidi.

Pedeshee David Kabunga:
Sifahamu alikuwa ni nani, jina lake lilikuwa linatajwa sana.

Papaa Ally Kileo:
He was a prominent lawyer in town, jina lake lilikuwa linatajwa sana kwenye nyimbo za dansi.

Papaa Mutarika Mzee wa Mambo mengi:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa zamani watajazia nyama kumuelezea.

Chef Justice Rugaibura:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa miaka ile watajazia nyama kumuelezea.

Chief Kiumbe le Big Boss:
Anafahamika vizuri, jina lake lilitajwa na kuimbwa sana na wanamuziki wa band. wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Papaa Amos Makalla mzee wa Mvomero, Babaa na Gabriele:
Kwa sasa ni RC wa Dar, jina lake lilianza kuvuma kitambo sana kabla hata hajaingia kwenye siasa.

Fikiri Madinda Mukuu wa kazi: Anafahamika vizuri, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Pedeshee Abdul Mkeketa:
Huyu wakati fulani aliwahi kuwa mbunge ktk Mkoa wa Morogoro, sikumbuki ni jimbo gani. kwa sasa ni marehemu.

Charles Mutawali Muzee ya Magari.
Binafsi simfahamu, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea.

Saidi Mukuu wa lumumba:
Jamaa alikuwa dalali wa kuuza magari pande za Lumumba.

Meddy Kitendawili....?
Ben Mulokozi....?
Salim Chicago Matelefone...?
Kizaizai....?
Omary Tolu...?
Abduli Tolu...?
Joshua Limited...?
Muddy Nyamalonda mzee wa Pamba...?
China wa China...?
Shaibu Mapajero....?
Moris Mariaga Rais wa Sinza...?
Nteze wa Nteze....?
John Nzenze....?
Papaa Madenge....?
Muddy Nyambi....?
Jimmy Chokolete....?


Note of Appreciation
.
sikufikiria kama huu uzi ungepata wafuatiliaji wengi kiasi hiki. niwashukuru wote mnaoufatilia na mnaochangia maoni yenu. asanteni sana wadau.[emoji1431][emoji1431][emoji1431][emoji1431]

Tukapate lunch tukape lunch oooh oooh kwa Mama Sakina uohh kwa Mama Sakina uoooh, mama Sakina mama wa Vingunguti
 
Uzi huu umenifanya nmkumbuke dada yetu Amina mongi (RIP)
Na imani angekuwepo mpaka leo angekuwa mtu fulani
Nakumbuka dstv inaingiaingia bongo
Na muktichoice wao ndy walikuwa wa kwanzakwqnza kuipigia promo
Nmepiga naye sana nyagi kinywaji chake....

Ova
umenirudisha mbali sana bro kuhusu dada amina mongi. may her soul continues to rest in peace. ardhi imemeza watu hii, dah!!.

miaka fulani ya katikati mwa 2000, niliwahi kufanya kazi kwa ukaribu sana na kaka yake azizi mongi. sijui yupo wapi kwa sasa huyu braza.

NB:
ila mrangi nimekuvulia kofia aisee, wewe ni encyclopedia inayotembea.

upo deep and well informed kuhusu matukio, lifestyle na watu maarufu waliotingisha jiji la dar mwishoni mwa miaka ya 90, miaka ya 2000 mpaka 2012.

nakushauri utunge kitabu ili upige pesa. kama utahitaji udhamini, nitasaidia kukupa connection.
 
umenirudisha mbali sana bro kuhusu dada amina mongi. may her soul continues to rest in peace. ardhi imemeza watu hii, dah!!.

miaka fulani ya katikati mwa 2000, niliwahi kufanya kazi kwa ukaribu sana na kaka yake azizi mongi. sijui yupo wapi kwa sasa huyu braza.

NB:
ila mrangi nimekuvulia kofia aisee, wewe ni encyclopedia inayotembea.

upo deep and well informed kuhusu matukio, lifestyle na watu maarufu waliotingisha jiji la dar mwishoni mwa miaka ya 90, miaka ya 2000 mpaka 2012.

nakushauri utunge kitabu ili upige pesa. kama utahitaji udhamini, nitasaidia kukupa connection.
Aziz namjua alikuwaga na ofisi ktk frame za konondoni bakwata Enzi zile
Jamaa alikuwa amesoma sana na mpaka ubongo wake ulikuwa kama umemwagika,nshamtumia sana kwa kunifanyia dili fulani fulani za mjini
Tulikuwa leo tunaelewana,mara kesho nkienda muona ananichenjia basi dah
Tafranii, sijui yuko wapi sahvi aziz

Yah amina mongi alikuwa vzr sana

Ova
 
Aziz namjua alikuwaga na ofisi ktk frame za konondoni bakwata Enzi zile
Jamaa alikuwa amesoma sana na mpaka ubongo wake ulikuwa kama umemwagika,nshamtumia sana kwa kunifanyia dili fulani fulani za mjini
Tulikuwa leo tunaelewana,mara kesho nkienda muona ananichenjia basi dah
Tafranii, sijui yuko wapi sahvi aziz

Yah amina mongi alikuwa vzr sana

Ova
the guy was naturally genius ila ukimuona unaweza dhani dishi limeyumba.
 
Haruna Fagason..huyu mwamba kila nyimbo aliyoimba gwiji na nguli wa muziki wa dansi Tanzania, Tx Moshi William lazima amtaje. Kwasisi wapenzi kindakindaki wa Msondo tunalitambua hili jina
ni kweli, hili jina nimelisikia mara nyingi. marehemu moshi william alikuwa analitaja sana.

alikuwa ni nani huyo mtu na yupo wapi hivi sasa?.
 
Nasikia sunda ni mwenye mount meru hotel Arusha
Sahihi kabisa mkuu,ana shares(partnership) na wakina Sullivan.Kuna kipindi hao Sullivan walitaka kuuza shares zao zote waondoke Ila sijui iliishia wapi.

R.Mengi aliwahi kutaka kuinunua Mount Meru hotel, wenyewe wakawa wanataka Tsh.bil 45 wkt Mengi anasema awape Tsh.33bil

Naona walishindwana,Mengi akaachana na biashara hio.
 
Uzi huu umenifanya nmkumbuke dada yetu Amina mongi (RIP)
Na imani angekuwepo mpaka leo angekuwa mtu fulani
Nakumbuka dstv inaingiaingia bongo
Na muktichoice wao ndy walikuwa wa kwanzakwqnza kuipigia promo
Nmepiga naye sana nyagi kinywaji chake....

Ova
Amina Mongi alikuwa na kampuni ya masuala ya urembo inaitwa faces international ndiyo iliyomtoa Miriam Odemba (Miriam mtoto wa Keko ghafla akawa maarufu na safari za China, usiniulize akienda kufanya nini).

Mkitaja wanamuziki msisahau wacheza densi kama King Jobiso, Small Jobiso na wengineo.

Ila Wabongo, nakumbuka kulikuwa na jamaa mmoja nimemsahau yeye alikuwa naye anawatuza sana Wanamuziki. Enzi simu ndiyo zinaanzaanza kabla ya kampuni ya Vodacom, jamaa alikuwa anapenda kuning'iniza simu yake kwenye suruali na maji ya Kilimanjaro anatembea nayo (enzi hizo ujiko).
 
Back
Top Bottom