Mzee masharubu alikuwa anaitwa
Alikuwa anauziaga pale mbuyuni primary shule na alikuwa anaishi pale St Peters kulikuwa na kijumba
Na jioni alikuwa anaondoka na familia yake kwenda coco kuuza mihogo
Kuna siku nlikaa sehemu napiga vyombo wakaja jamaa wa media sjui clouds wale kuna mmja namjua na wakawa wanazungumzia mambo ya mihogo,ndy nkawambia nyie mnajua historia ya mihogo coco lakini
Ova
ilikuwa ni siku ya jumamosi mwaka 1997 nikiwa kidato cha pili ktk secondary fulani maarufu jijini dar.
tulikuwa tunaishi mitaa ya chang'ombe maduka mawili, jirani na uwanja wa TCC club(siku hizi panaitwa gwambina lounge).
mida ya saa moja jioni, mimi,mshua, bmkubwa na ndugu wengine wawili wa familia tukaingia kwenye landrover defender la pale home. mshua akiwa kwenye usukani tukaanza safari ya kuelekea oysterbay kwenye harusi ya ndugu yetu.
sikumbuki jina la ukumbi,ila ninachojua ulikuwa mkono wa kushoto, kilomita chache mbele baada ya kushuka kilima nyege.
kipindi hicho mziki wa hip-hop hapa tz ndio ulikuwa unaanza kukamata akili za marika mbalimbali ya vijana, mimi nikiwemo.
moja ya kundi lililokuwa linatamba sana ni kundi la Kwanza Unit. asilimia kubwa ya waasisi wa hili kundi walikuwa ni watoto wa kishua, halafu base yao muda mwingi ilikuwa mitaa ya Oystebay.
baadhi ya video zao zilikuwa zinarushwa sana ITV(enzi zetu za analogia, enzi za mikanda ya VHS).
katika kundi hili mwanahiphop ambaye nyota yake ilikuwa tayari imeshaanza kuchomoza alikuwa ni marehemu Robert Mwingira aka D. Rob. ofcourse nilikuwa namu admire sana, jamaa alikuwa na style ya pekee ya kunata na beat.
sasa tukiwa pale ukumbini, mshua akanitambulisha kwa baadhi ya ndugu waliohudhuria ile sherehe ya harusi.
moja ya ndg. wa familia ambao mshua alinitambulisha ni marehemu D. Rob. akaniambia Baba yake yeye na Baba yake Robert ni ndugu, wote ni wangoni wenye asili ya huko Mbinga, Ruvuma.
nikawa so excited kukutana na mtu ambaye namu-admire, jamaa alikuwa so charming, mda wote ana furaha halafu mnyamwezi ile mbaya, ana kipini puani kama 2pac, kavaa mavazi kama wanayovaa vijana weusi wa mitaa ya queen's bridge, si unajua tena mapigo ya watoto wa kishua wa miaka ile.
those days Baba yake D. Rob(marehemu mzee mwingira) alikuwa ni ofisa mkubwa serikalini, makazi yao yalikuwa ni mitaa ya Oystebay.
nikiwa pale ukumbini nikawa najiweka karibu na D.Rob ili nipiginae story. halafu washkaji zake kama wanne hivi waliokuja pale ukumbini, walikuwa na swagger kama yeye, kuanzia mavazi mpaka uzungumzaji.
jamaa walikuwa wanaongea kingereza chenye lafudhi ya wamarekani weusi. nikawa naenjoy tu kuwasikiliza, utoto bhana, acha tu[emoji16]
siku hiyo D. Rob alikuwa kagandana na binti fulani wa kizungu, baadae nikaja kuambiwa ni mchumba wake.
inasemakana huyu binti wa kizungu alikuwa ni mtoto wa balozi(sijui wa canada, sina uhakika). wahenga wenzangu ambao walikuwa karibu na circle ya D. Rob mnaweza kujazia nyama kuhusu huyu manzi wa kizungu.