Wasanii wa DRC kumbe hauwafahamu, wengi ni choka mbaya na wanaishi kwa kuungaunga sana.
Ambao huwa wanakwenda Europe huwa hata huko wanaishi kwa kuungaunga sana, wakipata pesa huwa cha kwanza ni shopping za nguo na vipodozi. In short huwa hawana maisha ya kueleweka ila wapo exceptional wachache wenye mafanikio.
nimewahi kufanya kazi na wacongo wakati fulani nikiwa najishughulisha na masuala ya entertainment. naijua vizuri sana hii jamii.
wasanii wa congo wanaenda kwa category, bila shaka utakuwa unawazungumzia wale wachanga ambao bado hawajatoka kimziki.
ni kweli hilo kundi wengi wao wanaishi kiujanjaujanja. hata hapa tz tunao wengi tu.
baadhi yao wanafanya kazi kama hair dressers kwenye saloon za kike mitaa ya kinondoni, usiku wanaenda kutumbuiza kwenye bar, kiingilio bia.
katika hili kundi, wengine wamejishikiza kwa mijimama ya mjini yenye hela, wakilelewa kama watoto, wao kazi yao ni kuchakata K tu.
hawa ndio wale kila pesa wanayopata, inaishia kununua mavazi na vipodozi. wanaamini utanashati ni great factor ya kuwanasa wanawake wenye fedha.
category ya wanamuziki wa kicongo ambao wapo vizuri kifedha ni akina koffi olomide, felix wazekwa, werrason, jb mpiana, fally, ferre gola, bwana mdogo innoss'b nk.
hili kundi ndio linaenjoy mikataba minono ya kibiashara, fedha na zawadi kutoka kwa matajiri na wanasiasa mbalimbali wa congo wanazotoa kama tip kwa msanii baada ya majina yao kuimbwa sana kwenye nyimbo.
kundi hili la wasanii ni matajiri sana. sidhani kama kuna mwanamuziki nchini anafikia utajiri wa hawa wanamuziki.hata huyu star wetu nasibu abdul ambaye kwa hapa kwetu anaonekana tajiri, hafiki kwenye level ya utajiri alionao fally ipupa. hawa wacongo wanamiliki majumba kinshasa, paris na brussels.
halafu wakifanya show ulaya, arena huwa zinajaa kwasababu ya support wanayopewa na diaspora community kubwa ya wenzao wanaoishi huko. pia support nyingine inatoka kwa waafrika wanaotoka ktk mataifa yanayozungumza kifaransa.
mcheki koffi olomide hapa akiwa anaendesha moja gari zake za kifahari. ila sijajua kati ya hii na ile ya diamond, ipi ni toleo la nyuma. wataalam wa magari watatusaidia.