Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Kumbe, lazima azeeke aise maana wakati anaimbwa Ni Miaka ya 2004 huko
Alikuwa naye Ni pedeshee au aliwapa msaaada gani Hawa wanamuziki Hadi aimbwe Sana?
Manka Mushi wala sio 2004 ni kitambo sana miaka ya 1997-2000 huko ndo walikua watuma Salaam wa RFA na Radio One wakati FM Radios ndo zinachipukia Bongo. Lakini pia wameimbwa sana na Kina Muumin Mwinjuma enzi za Mchinga Sound hadi African Revolution, hiyo 2004 unayosema wewe tayari walishakua wakongwe kazini na music wa dance ndo ulikua kwenye turning point na Bongo Flava ndo inaanza anza kushika hatamu
 
Manka Mushi wala sio 2004 ni kitambo sana miaka ya 1997-2000 huko ndo walikua watuma Salaam wa RFA na Radio One wakati FM Radios ndo zinachipukia Bongo. Lakini pia wameimbwa sana na Kina Muumin Mwinjuma enzi za Mchinga Sound hadi African Revolution, hiyo 2004 unayosema wewe tayari walishakua wakongwe kazini na music wa dance ndo ulikua kwenye turning point na Bongo Flava ndo inaanza anza kushika hatamu
upo sahihi kabisa ndg yangu. mimi nilianza kulisikia jina la manka mushi 1997-1998.

kipindi hicho radio fm iliyokuwa imekamata airwaves za bongo ni radio one sterio.
 
mimi kama author wa uzi huu na wadau wenzangu wengine wa masuala ya celebrities and powerful public figures wa bara hili la africa hatumfahamu mtu huyo na wala hatujawahi kusikia jina lake.

umaarufu na upedeshee wake bila shaka unaushia kwenye familia yake na kijijini alichozaliwa. karibu tena ndg.
Pedeshee [emoji3582]

PDG [emoji3581]
 
Nicky Menga Barcelone girlfriend wa zamani wa fally ipupa kipindi hicho fally sio mtu maarufu sana akijitafuta kwenye ramani ya mziki.

pic moja nzuri sana. sijui fally alighafirika nini akamuacha huyu mdada.
 

Attachments

  • 1527b879bf809fae9381a00af34dd77f.mp4
    3.2 MB
Pedeshee [emoji3582]

PDG [emoji3581]
kwa muktadha wa kiswahili kinachotumika kwenye mziki wa dansi, tunandika pedeshee.

kifaransa tunaandika 'président-directeur général' ambapo kifupi chake ndio hiyo PDG ikiwa na maana ya CEO kwa kingereza.

kwa kukusaidia zaidi, CEO kwa kiswahili ni 'Mkurugenzi Mtendaji'.
 
upo sahihi kabisa ndg yangu. mimi nilianza kulisikia jina la manka mushi 1997-1998.

kipindi hicho radio fm iliyokuwa imekamata airwaves za bongo ni radio one sterio.
Leo nlikutana na papa msofe nlikuwa mitaa ya golden folk mikocheni,tukapiga stori 1,2
Wakati natoka naye akawa anatoka akaingia ndani ya kibrevis kimechokchoka,nkamzingua mbn huko humu akacheka akasema ttz yale magari makubw yanachoresha 😄

Ova
 
Leo nlikutana na papa msofe nlikuwa mitaa ya golden folk mikocheni,tukapiga stori 1,2
Wakati natoka naye akawa anatoka akaingia ndani ya kibrevis kimechokchoka,nkamzingua mbn huko humu akacheka akasema ttz yale magari makubw yanachoresha 😄

Ova
Yanachoresha 😅😅😅
 
WAKATI NIPO SINZA NDIYO KAJUMULO KAINGIA MJINI KWA FUJO SANA , SASA ALIKUWA NA WAPAMBE WAKE WANAGAWA T SHIRTS NA MA TRUK SUITS YENYE MAJINA YAKE, MIE NIKAWAAMBIA KAMA MNATAKA NIVAA NGUO ZENYE MAJINA YA KAJUMULO WANALIPE LA HAPANA KABISA KUVAA NGUO ZENYE MAJINA YA WATU MAARUFU WENYE PESA ZA UJANJA UJANJA !!!!!
🤣🤣🤣🤣
 
Awali ya yote nitangulize angalizo kwa vijana ambao maturity stage imewakuta miaka hii ya mitandao ya kijamii. Itabidi msome kimyakimya huku mkiwa mmeshika peni na karatasi kuchukua notes.

Huu uzi ni wa sisi ma-seniors, maudhui yake yatagusa zaidi vijana wenzangu ambao maturity stage iliwakuta kuanzia late 90s to early 2000s.

Mwaka 2002 mpaka 2012 mziki wa dansi ulikuwa upo kwenye prime time.

Kwa uchache tu, band zilizotamba ni FM Academia, Akudo Impact, Twanga Pepeta na Diamond Musica. Band nyingine zilikuwa zinaibuka na kupotea ndani ya muda mfupi.

Umaarufu wa hizi band ulienda sambamba na trend ya wanamuziki kutaja majina ya baadhi ya watu kwenye mashairi yao.

Majina ya hawa watu yalivuma na kuwa maarufu kuliko sura zao kwasababu miaka ile kulikuwa hakuna social platform za ku-share picha na video kama ilivyo hivi sasa.

Kutokana na kujichanganya kwangu ukijumlisha na ujanja wangu wa kimjini mjini wa miaka ile, nilifanikiwa kufahamiana na baadhi mapedeshee au wazee wa mujini ambao majina yao yalikuwa yanatajwa kwenye mziki wa dansi.

Nitataja ninaowakumbuka na wewe ongeza wa kwako.

Naandika majina yao kama yalivyokuwa yanatamkwa kwa mbwembwe na wanamuziki.

Kwa mfano kama mtu alikuwa anaitwa John, wanamuziki walikuwa wanatamka papaa John Young Millionaire Muzee ya ma-Range Rover[emoji3][emoji3].

Haya twende kazi:
Pedeshee Mychoice na kati ya Mbeya
:
huyu sijui alikuwa anapiga mishe gani huko Mbeya, watu wa Mbeya mtatusaidia.

Braza K na kati ya Tunduma:
Watu wa Tunduma mtatusaidia kutujuza kuhusu huyu jamaa, alivuma sana.

Mamaa Rukia Soloon:
Huyu bibie namfahamu, ana saloon yake ya kike mitaa ya Mikocheni barabara ya Rose Garden. Those days she was very pretty, kwa sasa utu uzima umemchukua.

Mamaa Dotnata Decoration:
Bila shaka wengi mnamkumbuka, aliwahi kuwa muigizaji maarufu kupitia ITV, baadae akaingia kwenye ujasiriamali wa kutoa huduma za decoration and catering. shughuli hizi zilimpatia mafanikio sana. sijui kwa sasa yupo wapi huyu mama. FM Academia waliwahi kumtungia wimbo wenye jina lake.

Mamaa Juddy Moshi:
Alikuwa mmiliki wa band ya Daimond Musica kwa financial support ya mshua mmoja ambaye alikuwa ni MD wa Yellow Pages, watu wa zamani wanaelewa. Juddy alikuwa mrembo si kitoto, kwa sasa umri wake umesonga mbele.

Pedeshee Akayesu Ndama Mutoto ya Ng'ombe:
Sina haja ya kumuelezea, ni mtu maarufu wa misimu yote. Wajanja wa mujini watamuelezea zaidi. Jina lake lilitajwa sana kwenye nyimbo za dansi zilizovuma.

Young Millionaire Bill gate Muzamir Katunzi:
Christian Bella aliwahi kutunga mpaka wimbo wenye jina hilohilo la Muzamir Katunzi. I don't know him personally, but it's told he was financially successful.

Papaa Msofe Chuma cha Reli hakishiki Kutu.
Sina haja ya kuandika mengi kuhusu umaarufu wa Papaa Msofe. Itoshe tu kusema jina lake liliimbwa sana halafu ni wachache waliokuwa wanajua sura yake. Walianza kuiona kwenye media alipokuwa anahudhuria viunga vya mahakama kujibu kesi yake.

Papaa Martin Kasianju.
Ni marehemu kwa sasa, huyu mshua ndio alikuwa mmiliki wa Band ya FM Academia. Nilikuwa namfahamu personally. licha ya kwamba alikuwa ni mjasiriamali na muajirwa Serikalini, pia alikuwa ni Senior Officer wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Andrew Traders na Kariakoo Big Supply: Jamaa alikuwa ni mfanyabiashara wa kuuza tairi za gari Mtaa wa Agrey Kariakoo huku akipiga michongo yake ya "general supply". Watu wa mujini wa zamani wanaelewa vizuri maana ya kampuni kusajiliwa kwa jina la general supply. Katika biashara ya kuuza tairi, alishirikiana na kaka yake, ila yeye akawa maarufu zaidi na akaaminika na wadau.

Kinje Mutoto wa Mujini:
Najua wengi mnamfahamu na zile deal zake alizokuwa anapiga. sina haja ya kumuelezea zaidi.

Pedeshee David Kabunga:
Sifahamu alikuwa ni nani, jina lake lilikuwa linatajwa sana.

Papaa Ally Kileo:
He was a prominent lawyer in town, jina lake lilikuwa linatajwa sana kwenye nyimbo za dansi.

Papaa Mutarika Mzee wa Mambo mengi:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa zamani watajazia nyama kumuelezea.

Chef Justice Rugaibura:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa miaka ile watajazia nyama kumuelezea.

Chief Kiumbe le Big Boss:
Anafahamika vizuri, jina lake lilitajwa na kuimbwa sana na wanamuziki wa band. wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Papaa Amos Makalla mzee wa Mvomero, Babaa na Gabriele:
Kwa sasa ni RC wa Dar, jina lake lilianza kuvuma kitambo sana kabla hata hajaingia kwenye siasa.

Fikiri Madinda Mukuu wa kazi: Anafahamika vizuri, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Pedeshee Abdul Mkeketa:
Huyu wakati fulani aliwahi kuwa mbunge ktk Mkoa wa Morogoro, sikumbuki ni jimbo gani. kwa sasa ni marehemu.

Charles Mutawali Muzee ya Magari.
Binafsi simfahamu, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea.

Saidi Mukuu wa lumumba:
Jamaa alikuwa dalali wa kuuza magari pande za Lumumba.

Meddy Kitendawili....?
Ben Mulokozi....?
Salim Chicago Matelefone...?
Kizaizai....?
Omary Tolu...?
Abduli Tolu...?
Joshua Limited...?
Muddy Nyamalonda mzee wa Pamba...?
China wa China...?
Shaibu Mapajero....?
Moris Mariaga Rais wa Sinza...?
Nteze wa Nteze....?
John Nzenze....?
Papaa Madenge....?
Muddy Nyambi....?
Jimmy Chokolete....?


Note of Appreciation
.
wakati naandika huu uzi sikufikiria kama ungepata wafuatiliaji wengi kiasi hiki. niwashukuru wote mnaoufatilia na mnaochangia maoni yenu. asanteni sana wadau.[emoji1431][emoji1431][emoji1431][emoji1431]
Kuna huyu alikua anaitwa Jack Pemba
 
mwaka 1996 kundi la wenge musica BCBG chini uongozi na usimamizi wa Werrason na JB mpiana liliachia album kali sana kwa jina pentagone.

nadhani baada ya hapo kundi lilisambaratika na kuzalisha mkundi mengine yaliyoshindana kimuziki.

ndani ya album hiyo kuna track inaitwa coco madimba.
coco madimba sio neno la kilingala bali ni jina la mtu,mdau wa muziki au tuseme sponsor mwenye fedha zake ambaye aliwalipa wanamuziki hao ili wamuimbe.

jina lake limesikika kwenye nyimbo nyingi za kundi hilo zilitoka miaka ya 90.

licha ya kwamba coco madimba ndio muhusika mkuu wa huu wimbo, ndani yake yametajwa majina ya wadau wengine wa muziki wa kikongo.

nakuwekea hapa kipande kifupu cha video ili uweze kuwafahamu.
 

Attachments

  • TikTok_7350817590849146118.mp4
    1.6 MB
Back
Top Bottom