Alafu anatokea mtu anawacheka malawi.Mi nadhani ungeanza na nchi yako kwanza...
Jana nimetoka mizungukoni nimewachukulia wanangu baadhi ya vitu wanapenda kula....nikaachana na daladala nikaingia kwa bajaji...kumbe Kuna zogo kati ya bajaji na daladala...mi nimo ndani wanarushiana maneno,nikamwambia tuondoke,anaondosha bajaji huku anaendelea na kamdomo....wakaanza kimbizia bajaji,dereva bajaji nae akaanza kukimbiza bajaji kama vile anakimbia kwa miguu,yaan ile unakimbia huku na kule ili usikamatwe...Mara ghafla kaparamiana na pikipiki iliyobeba trey za mayai....kibajaji kinataka kulala mi nikaruka...vitu vyangu vilisambaratika ...badala ya kusaidia watu wakaanza kuokota na kubugia bagia,wakaanza kuramba ubuyu....mayai wakazoa mpaka Ute wenye mchanga...bas ikabidi tujiinue sisi wenyewe🙌😔
Uafrika ni laana!!!!