Tuwasaidie wanawake wanaotembeza matunda na watoto mgongoni

Tuwasaidie wanawake wanaotembeza matunda na watoto mgongoni

Nilikuwa na house girl mshamba mbutika kamaliza gongo la mboto mwisho wa lami. Anavaa vitenge mpaka kwenye unyayo..
Baada ya mwezi akaanza kunawiri
Baada ya mwezi mwingine akapata simati foni. Shida ilianzia hapo
Jamani kama kuna binti ambaye nilimuasa kuhusu maisha yule anaongoza..
Lakini sasa hivi analea mimba aliyojaribu kuitoa mara tano ikishindikana.. Kapanga chumba cha giza kula yake ya kubahatisha.. Kakonda kabaki kichwa
Nawaza sana akijifingua future yake na mtoto itakuwaje
Ndiyo akianza kuuza matunda uwe mteja wake kaka .
 
Nakutana na kundi kubwa la wanawake wakiwa wamebeba watoto wadogo wakitembeza matunda mazingira ya jua Kali sana nawaonea huruma ukikuta dada anateseka juani na mtoto fanya kama unatoa sadaka tu kwa kununua matunda yake utabarikiwa sana

Kweli mkuu ,ukibarikiwa kidogo share na wenye uhitaji ,usile peke yako tu.
 
Tuwaunge mkono ata ukiandaa buku yako yakula tunda kila siku ni jambo jema Kuna kitu kitaongezeka maishani mwako hauwezi kubaki bure
Sio lazima lakini.

Ukisema uonee huruma kila mtu utapata msongo wa mawazo.

Huwezi tatua kila tatizo kwamba ujitwishe mzigo wa dunia nzima mgongoni mwako.
 
Nilikuwa na house girl mshamba mbutika kamaliza gongo la mboto mwisho wa lami. Anavaa vitenge mpaka kwenye unyayo..
Baada ya mwezi akaanza kunawiri
Baada ya mwezi mwingine akapata simati foni. Shida ilianzia hapo
Jamani kama kuna binti ambaye nilimuasa kuhusu maisha yule anaongoza..
Lakini sasa hivi analea mimba aliyojaribu kuitoa mara tano ikishindikana.. Kapanga chumba cha giza kula yake ya kubahatisha.. Kakonda kabaki kichwa
Nawaza sana akijifingua future yake na mtoto itakuwaje
wanawake/wadada hawahoni mbali.

Unaweza kuwa na umpa ushauri mwanamke aache mwenendo wake mbaya lasivyo mbeleni anaweza kupitia ktk hali ngumu, akakujibu wewe ni Mungu. Wakati maisha yana asili ya vitu, ukikosea baya linaweza kukupata!
 
Tatizo wengi wao kama sio wote ni wale waliokuwa wakishauriwa juu ya mienendo yao walikuwa wana jibu kwa dharau kuwa wasiingiliwe na kupangiwa maisha.
Na wengine walisha fuatwa na wanaume sahihi na wenye nia thabiti ya kuanzisha nao familia waka wakataa tena kwa nyodo badala yake wakaenda kudete na waume za watu na vijana wachoma CD na vijana wanyoa viduku.

Acha walipie upumbavu wao walio ufanya labda wanaweza kuwa mfano mzuri kwa hao watoto wao na mabinti ambao bado ni wadogo.
 
Serikali isisitize uzazi wa mpango na kuhamasisha njia za uzazi wa mpango
 
Vijana wadogo wanihitaji kupata elimu na huduma za uzazi wa mpango
 
Back
Top Bottom