MC RAS PAROKO
JF-Expert Member
- Feb 14, 2013
- 623
- 606
Nitaandika kwa kifupi sana kwa kuwa hii ni hoja isiyo hitaji maelezo mengi. Hoja yangu ya msingi ni hii Badala ya serikali kuwafungia ndani wafungwa na kuwatumia kufanya usafi mara moja kwa wiki tuwatumie wafungwa hawa kuzalisha chakula cha wanafunzi mashuleni na kitolewe bure pia, kwa wanafunzi wote.
Serikali itenge mashamba ya shule kila wilaya Nchi nzima na mashamba hayo yahudumiwe na magereza yaliyopo katika wilaya husika.
Hii itasaidia kupatikana kwa chakula cha uhakika kwa wanafunzi wanaosoma katika shule za kutwa katika wilaya husika na kuwaondolea wanafunzi adha ya kurudi nyumbani kula mchana au kushinda na njaa shuleni kwa sababu kama tujuavyo sote ukiwa na njaa ni ngumu kuweza kutuliza akili uelewe unachofundishwa.
Pia wazazi wanaotozwa pesa kwa ajili ya chakula cha watoto wao katika baadhi ya shule watakua wamesaidika na wataweza kukidhi mahitaji mengine ya kielimu kwa watoto wao kama vitabu n.k
Kwa upande wa magereza itawasaidia kuongeza uwajibikaji na pia kuwasaidia kujifunza kushirikiana na wenzao na pia njia bora za kilimo ambazo zitawasaidia pindi warudipo uraiani wajue nini cha kufanya ili wabaki kuwa raia wema kwa kipindi chote cha maisha yao.
Na mwisho wa yote JAMII nzima itakua imefanikiwa kwa kuwa watoto watafanya vizuri shuleni,wazazi watapunguziwa gharama za kuwasomesha watoto wao na serikali itakua imewalisha wanafunzi bila gharama yeyote kubwa.
Ni aibu leo mfungwa anauhakika wa milo mitatu kwa siku huku mwanafunzi tunayeamini ndo future yetu hawana uhakika wa kupata milo mitatu. Yaani tunawajali wafungwa zaidi ya kizazi cha kesho.