Ryan Holiday
JF-Expert Member
- Jul 25, 2018
- 3,499
- 5,956
"As-salamu alaykum," kwa ndugu zangu Waislamu.
“Bwana Yesu Kristo Asifiwe,” kwa ndugu zangu Wakristo
Bila kupoteza muda, nimekuja kwenu hili kuwajuza juu ya wimbi la biashara za online ambazo kila kukicha zinazidi kuibuka kama uyoga. Vitu vingi vinaama kutoka kwenye ulimwengu wa kawaida na kwenda kwenye ulimwengu wa Kidigitali kwa kasi ya 5G. Mabadiliko haya yanatokana na maendeleo ya teknolojia, hasa kwa upanuzi wa mtandao, vifaa vya kielektroniki, na programu mbalimbali zinazobadilisha jinsi tunavyofanya kazi, kuwasiliana, na kushiriki maisha yetu.
Wizi wa mtandaoni na udanganyifu wa kidijitali (online scams) umekuwa ni changamoto kubwa kutokana na kuenea kwa teknolojia na biashara za mtandaoni. Watu wengi, hasa wale wenye uelewa mdogo wa mazingira ya kidijitali, wamekuwa wahanga wa udanganyifu huu.
Kuna kikundi cha watu kinajiita IFX (Intelligence FX), hicho kikundi kinachukua pesa za watu kwa lengo la kuwafundisha Forex na kwamba kina wahakikishia wanafunzi wao kuwa na faida ya uhakika sokoni (consintently) kitu ambacho ni uongo. Huku wakichaji gharama ya kiasi cha chini ni dola 200 – 300 fedha za kimarekani, yaani ni shilingi za kitanzania 529,577 - 794,366.
Mimi kama mdau wa JF nitoe tu, angalizo tuwe makini na watu wanaoibuka online na kujiita Mentor sijui Guru. Hivi wewe kaa chini na ufikiri soko lina-offer millions to millions of dollars kama huyo mtu anajua Forex kwa nini asitumie muda wake mwingi sokoni kutengeneza mamilioni badala yake aanze kuangaika na dola 200 au 300 ya kwako. Huku kwa maisha ya mtanzania dola 200 mpaka 300 sio pesa ndogo ni mtaji mkubwa sana. Nasisitiza na kusema “Ukiona unaitiwa fursa ujue wewe ndio fursa.”
Tuwe makini na biashara za mtandaoni, na siku zote hakuna pesa rahisi.