Tuwe makini na biashara za mtandaoni Intelligence (IFX) ni wezi kama wezi wengine tu

Na

mm najua ivyo wako royal na customers naona huu Uzi nimeshtuka ila najua wengi wanaona kulipia izo ela wanapigwa wakati ni darasa kama madarasa ya economics📌
Wale wanafundisha mpaka vitu advanced sana...

Kama anahitaji kufundishwa juu juu, wapo wanaofundisha mpaka kwa dola 20, aende kwa hao..
 
Anastasia21 na Kingsmann hoja ya mleta mada Iko valid kama ilivyo ya kwenu pia.

Anachokataa ni kuambiwa kuwa ni lazima mtu apate faida. Ni kama vile ukifundishwa mambo ya Forex basi ukishajua ndiyo fedha zinatiririka tu kimfululizo.

Alipokuwa anamjibu Anastasia21 kaelezea vizuri tu kwamba forex ni ubashiri (Speculation)na ubashiri hauwezi kuwa sahihi wakati wote.

Na pia kwenye maelezo yake kaweka mambo yanayoongoza huo ubashiri. Ukweli wa mambo forex siyo biashara rahisi kama hao "brokers" na "mentors" wanavyotaka ionekane.

Halafu mleta mada ana hoja. Kama hao wafundishaji wanaona forex ni rahisi kujioatia fedha kwa nini wao wasijikite kuzipata hizo fedha toka kwenye forex badala ya kuhangaika na hizo dola 200-300 za wanaowaalika wajifunze mambo ya Forex?

Nakubaliana na mleta mada: Hakuna upatikanaji wa fedha kirahisi.
Ni kweli kabisa..

Lakini ile ni lugha ya kuvutia wateja, kila biashara ina pickup line zake ili uvute wateja..

Kazi yako ww kama customer ni kujiongeza kujua uhalisia wa jambo husika ukoje..

Ila kusema IFX ni matapeli, sio kweli. Hapo anaharibu biashara ya vijana wanaojipambania.
 
View attachment 3274641
Sikubaliani na wewe hata kidogo, pia hao jamaa si wakweli hata kidogo, wana watapeli watu wenye elimu ndogo juu ya biashara za online, hauwezi kumwambia mtu nakufundisha kilimo fulani na kufanikiwa ni lazima. Na wakati kuna factors za muhimu ambazo kilimo chako kinategemea kwa asilimia kubwa kama mvua, ukame na bei ya sokoni, ambazo hazipo under your control. Hapo utakuwaje na kilimo cha uhakika? Tukirudi kwenye Forex, kuna factors ambazo hazipo kwenye mikono yako, yaani hazipo under-your control (economic events, political events, global events na market sentiment) n.k. Hapo utamwambiaje mtu kufanikiwa ni lazima na consintently? Kama sio wizi na udanganyifu wa mtandaoni.

Hakuna biashara yenye faida tu, na ambayo haina hasara! Kama ingekuwa hivyo wakina Azam Bakhresa, Mo-Dewji basi wangewekeza huko mapesa kwa mapesa. Huo ni udanganyifu wa mtandaoni.​
Sasa bwashee, ulitaka hapo waandike "Become Inconsistent & Non-Profitable Trader?".

Maneno waliyotumia ni for encouragement tu, ukiingia hata bio za wauza simu na vyombo wameandika vitu ambavyo wewe kama mteja unajua kabisa hizi ni lugha za kuvuta wateja, ila uhalisia unaujua mwenyewe..

Ndiyo maana kuna "Risk Management". Kwa kuzingatia kwamba hakuna alijuaye soko litaenda wapi, ndiyo maana kuna vitu kama Stop Loss ili endapo mambo hayataenda kama ulivyopredict basi mtaji wako uwe salama.
 
Ni kweli kabisa..
Ila kusema IFX ni matapeli, sio kweli. Hapo anaharibu biashara ya vijana wanaojipambania.
Sidhani kama maudhui ya mleta mada ni kuonesha mambo ya Forex ni utapeli. Ila utapeli anaouna yeye ni kumwambia mtu kuwa afundishwe Forex na akihitimu basi yeye kazi yake itakuwa ni kuvuna mamilioni ya pesa.

Matangazo yao kwa kweli huwa yanaashiria kwenye forex Kuna upatikanaji fedha kirahisi na watu wa forex ni matajiri wanaopata fedha kwa kukaa tu nyumbani na kutumia vifaa vya kielektronik kujitajirisha.
 
Nenda kasome uzi wake upya..

Ameshindwa kutofautisha lugha ya biashara na uhalisia.

Mfanyabiashara anaweza kutumia lugha laini ili akuvute ila ww mteja kazi yako ni kutafuta ukweli wa mambo ukoje.
 
Nani alisema ni rahisi? Mnawalisha watu maneno. Lile ni darasa uelewa na ufanisi wa mtu ndio utakaomlipa anaejifunza. Tukubali tu sio kila biashara ni ya kila mtu. Mambo mengine yanachagizwa hata na personality ya mtu.

Kuna mtu akisikia jambo fulani linalipa basi anadhani linalipa kwa kila mtu atakaelifanya, dunia haiko hivyo. Wale ambao wakifanya hicho kitu kisha wakachemsha wanaanza kuita jambo kuwa ni gumu sa, ni utapeli na kadhalika.

Kuna watu wanalima mahindi wnapata hela nzuri, na kuna watu washalima sana hadi wanathubutu kusema ukulima ni upuuzi kwa kuwa hakufanikiwa katika njia hizo
Asante sijui nikupe zawadi gani😍
 
Wale wanafundisha mpaka vitu advanced sana...

Kama anahitaji kufundishwa juu juu, wapo wanaofundisha mpaka kwa dola 20, aende kwa hao..
Sina haja ya kufundishwa kitu ambacho ni reflection of yourself. Kila mtu ana malengo na viwango tofauti vya kujifunza. wanaotaka maarifa ya msingi wanaweza kuanza popote kwanza, lakini sio kwao ma-pro ambao wanadanganya watu kwamba kufanikiwa ni lazima kwenye biashara ya FX. Kitu ambacho sio kweli kuna miezi unaweza kufanikiwa na kuna miezi mtu unaweza kuwa kwenye hasara (ku-experience Drawdown).

Usidanganyike ndugu yangu, hao wapo kimaslahi zaidi na sio kibiashara. Mwambie mtu ukweli, kwa sababu anatoa pesa yake aliyoitolea jasho, kwa kile wewe unachotaka kumpa. Hili mwisho wa siku, ni maamuzi yake mwenyewe wapi atawekeza pesa yake."​
 
Sasa bwashee, ulitaka hapo waandike "Become Inconsistent & Non-Profitable Trader?".

Maneno waliyotumia ni for encouragement tu, ukiingia hata bio za wauza simu na vyombo wameandika vitu ambavyo wewe kama mteja unajua kabisa hizi ni lugha za kuvuta wateja, ila uhalisia unaujua mwenyewe..

Ndiyo maana kuna "Risk Management". Kwa kuzingatia kwamba hakuna alijuaye soko litaenda wapi, ndiyo maana kuna vitu kama Stop Loss ili endapo mambo hayataenda kama ulivyopredict basi mtaji wako uwe salama.
"Sawa bwashee, lakini kumbuka kuwa trading siyo marketing—hapa hakuna maneno ya kuvutia tu bila msingi. Ukweli ni kwamba consistency na profitability for the long run ni uongo. Ndiyo maana Stop Loss ipo, lakini hiyo pekee haitoshi kama strategy yako haina edge. Mwisho wa siku, trader mzuri anajua kuwa hakuna uhakika wa 100%, kila trading anayoenda anajua ni 50%-50%.
 
Kwa hiyo hapo kwenye bio unasuggest wangeandika nini mkuu!
 
Changamkia fursa kula Hela tembea ona hiyo
 
Attachments

  • IMG-20250318-WA0215.jpg
    IMG-20250318-WA0215.jpg
    42.3 KB · Views: 31
"As-salamu alaykum," kwa ndugu zangu Waislamu.

“Bwana Yesu Kristo Asifiwe,” kwa ndugu zangu Wakristo

Bila kupoteza muda, nimekuja kwenu hili kuwajuza juu ya wimbi la biashara za online ambazo kila kukicha zinazidi kuibuka kama uyoga. Vitu vingi vinaama kutoka kwenye ulimwengu wa kawaida na kwenda kwenye ulimwengu wa Kidigitali kwa kasi ya 5G. Mabadiliko haya yanatokana na maendeleo ya teknolojia, hasa kwa upanuzi wa mtandao, vifaa vya kielektroniki, na programu mbalimbali zinazobadilisha jinsi tunavyofanya kazi, kuwasiliana, na kushiriki maisha yetu.

Wizi wa mtandaoni na udanganyifu wa kidijitali (online scams) umekuwa ni changamoto kubwa kutokana na kuenea kwa teknolojia na biashara za mtandaoni. Watu wengi, hasa wale wenye uelewa mdogo wa mazingira ya kidijitali, wamekuwa wahanga wa udanganyifu huu.

Kuna kikundi cha watu kinajiita IFX (Intelligence FX), hicho kikundi kinachukua pesa za watu kwa lengo la kuwafundisha Forex na kwamba kina wahakikishia wanafunzi wao kuwa na faida ya uhakika sokoni (consintently) kitu ambacho ni uongo. Huku wakichaji gharama ya kiasi cha chini ni dola 200 – 300 fedha za kimarekani, yaani ni shilingi za kitanzania 529,577 - 794,366.

Mimi kama mdau wa JF nitoe tu, angalizo tuwe makini na watu wanaoibuka online na kujiita Mentor sijui Guru. Hivi wewe kaa chini na ufikiri soko lina-offer millions to millions of dollars kama huyo mtu anajua Forex kwa nini asitumie muda wake mwingi sokoni kutengeneza mamilioni badala yake aanze kuangaika na dola 200 au 300 ya kwako. Huku kwa maisha ya mtanzania dola 200 mpaka 300 sio pesa ndogo ni mtaji mkubwa sana. Nasisitiza na kusema “Ukiona unaitiwa fursa ujue wewe ndio fursa.”

Tuwe makini na biashara za mtandaoni, na siku zote hakuna pesa rahisi.
Kila siku nawaambia hapa JF
 
Katika ulimwengu wa sasa wa kidijitali, watu wengi wanadanganywa na ahadi za faida ya uhakika kwenye Forex na biashara nyingine za mtandaoni.

Ukweli ni kwamba hakuna pesa rahisi, na yeyote anayekuhakikishia utapata faida bila hatari ni tapeli.

Tuwe makini tufanye uchunguzi wa kina pale tunapotaka kuwekeza, tusikubali kutumiwa kama daraja la wengine kujitajirisha.
 
Back
Top Bottom