Pre GE2025 Tuwe wa wazi; Hakuna chama cha upinzani chenye uwezo wa kupata walau 20% ya kura zaidi ya CHADEMA

Pre GE2025 Tuwe wa wazi; Hakuna chama cha upinzani chenye uwezo wa kupata walau 20% ya kura zaidi ya CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Kinjekitile Jr

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
566
Reaction score
1,583
Wakuu Habarini/salaam/Shalom

Ukitazama kwa mwenendo wa siasa zetu ndani ya miaka takribani 10 mpaka sasa,utaona jinsi watu walivyo kuwa na mwamko mdogo sana kuhusu siasa,hii inakuja baada ya kufungiwa kwa harakati za kisiasa chini ya Hayati J.P. Magufuli, Madhara ndo yanaonekana leođź©´

Hali imewaendea mrama sana Wanasiasa karibu wote,sio wa upinzani ata wale wa Chama tawala,Hali bado imekuwa ile ile, Ila kwa CHADEMA kidogo inaonekana bado wana ile power hata wakiita mkutano unaona watu wanakusanyika, tofauti na CCM ambao inahitajika nguvu ya Wasanii na usafiri wa bure kuwaleta watu na kuwarudisha majumbani kwao

Leo ukitembea sehemu yoyote ile TZ bara,ukisema neno Mpinzani wao wanajua ni CHADEMA pekee,kidogo labda na ACT, japo ACT Wazalendo wanahitaji wafanye kazi ya ziada sana kupata legitimacy kwa watu,vinginevyo wataishia kuwa Chama cha kuchukulia ruzuku Kama ilivyo kwa CHAUMA,TLP,NCCR au CUF

CHADEMA wametawala siasa za upinzani kwa kipindi kirefu sana mpaka sasa takribani miaka 20,hakuna chama chochote cha upinzani kilichopita kwenye msoto mkali na kilichodumu na nguvu hiyo toka tupate uhuru

Uchaguzi unaofuata bado naiona CHADEMA ikienda kuchukua majimbo mbalimbali ndani ya nchi hii

Sioni kama kuna Mpinzani aliyenyooka kama CHADEMA hapa TZ bara

LET’S GIVE THE CREDIT WHERE THE CREDIT IS DUE✅
 
Back
Top Bottom