Tuwe wazi, kupata mtoto mwenye ulemavu au magonjwa ya kuwa tegemezi maisha yake yote ni zawadi kutoka kwa Mungu?

Kiimani tutajifariji kwa kusema ni majaribu kutoka kwa mwenyezi Mungu. Ila kwa ujumla wake uwa ni mtihani mkubwa sana kwa wazazi unaoambatana na gharama kubwa katika mfumo wa fedha, muda, huruma, uvumilivu n.k. katika kumlea mtoto wa aina hiyo. Kukosekana kwa mojawapo ya vitu hivyo kunaweza kupelekea mzazi kukufuru na/au kufanya tukio lisilopendeza kwa mtoto husika.
 
Wewe hapo unaesoma uzi huu ukipata mtoto ama tayari unae :
  • haoni na hasikii
  • hajitambui
  • utindio wa ubongo
  • ugonjwa wa kumfanya ahudumiwe kila kitu

Kwako wewe kutoka moyoni mwako, hii ni zawadi kutoka kwa Mungu ?
Ni Mtihani kutoka kwa Mungu, unapaswa uushinde kwa kumhudumia kama mtoto aliye mzima
 
Zamani Wamasai wlikuwa na mila ya kuuwa watoto walemavu, sijuwi siku hizi kama wameawacha.
Kwa sehemu kubwa bado wanafanya hivyo vijijini...ulemavu wowote wa viungo na ualbino pia
 
Fungua tuu mkuu,unaweza kupata kitu,kuna shuhuda za watu kama huyo mtoto kwa sasa wako vizuri,Mungu ni mwema wakati wote.
 
Halafu eti kuna wamama wanaua watoto wao kisa 500/=
 
sio zawadi kutoka kwa Mungu, ila ni bahati mbaya tu hawatakiwi kunyanyapaliwa,

watakuja kusema hizo ni laana, sasa ndo ujiulize ni Mungu gani mwenye upendo anaadhibu kiumbe kisichokua na hatia kwa makosa ya mababu/wazazi wake😂
Kazi za wachawi hizo kama mzazi haupo na Mungu,
Ukiwa na Mungu hayakukuti hayo
 
Kwa dunia ya sasa hata sio changamoto.
Kwa mfano wasioona wanaweza kusoma vizuri kabisa kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu na anaweza akawa msaada mkubwa kwa mzazi pia.

Maendeleo ya teknolojia yameleta nyenzo wezeshi za kumsaidia kusoma na hata kufanya kazi sawa sawa na mtu mwingine.
Mfano darasani anaweza kuwa na uwezo mzuri kuliko wasio na changamoto.
Hata hapa JF kuna asiyeona mmoja nimemsahau jina na alikuwa anachangia mada sawa na sisi tu.
 
Zamani Wamasai wlikuwa na mila ya kuuwa watoto walemavu, sijuwi siku hizi kama wameawacha.
Sio wamasai tuu makabila yote ya kaskazini yaani wamasai,wambulu,barbeig,waarusha,wameru,wachaga na wataita hawakuruhusu watoto walemavu hadi albino waishi,wakunga walikuwa wanamaliza kazi na kumwambia mama mzazi kuwa mtoto ni bahati mbaya.Nawafahamu mapacha peter na paulo waliozaliwa 1924 na pona yao walikimbizwa kutunzwa na father James Maghan mholanzi.Hoja ilikuwa je vita vikija utabeba mlemavu au utakimbia na mifugo ambayo itakusaidia huko mbele ya safari?Ukweli ni kwamba maendeleo na tangazo la haki za binadamu limeokoa wengi.
 
MTOTO NI MTOTO.
Hakuna mama anayemchukia mwanae kisa mlemavu.
Au baba anayemchukia mwanae kisa mlemavu.
Ni vile tu wanakuwa masikini.wengine uamua kukimbia na kuacha watoto
 
Kutokana na ukuaji wa sayansi hasa katika field ya biology specifically in genetics huko mbele kwenye nchi za ulimwengu wa kwanza imewezekana kuona namna mtoto atakavyokuwa kupitia study of genes.

So wazazi hushauriwa juu ya possible outcomes na kupewa options za either ku abbort .

Mjadala unakwenda mbali zaidi juu ya "je, mtoto anaweza kumshtaki mzazi kwa kumleta ulimwenguni kupata mateso MAISHA take yote Hali akijua kuwa atateseka???

Na Kama wazazi watakubali kumleta duniani mtoto anayesumbuliwa na matatizo Kama hayo, gharama za matibabu ziondolewe kutoka kwenye bima ya afya?? Kwa sababu Ni kubwa mno.

I don't know wamefika wapi lakini Mambo yapo hivyo.
 
mpe pole,,tupo pamoja ❤️❤️❤️❤️❤️‍
 
Wewe hapo unaesoma uzi huu ukipata mtoto ama tayari unae :
  • haoni na hasikii
  • hajitambui
  • utindio wa ubongo
  • ugonjwa wa kumfanya ahudumiwe kila kitu

Kwako wewe kutoka moyoni mwako, hii ni zawadi kutoka kwa Mungu ?
Muue, utazaa mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…