Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza

Wewe jamaa, tukutane pale wizara ya pesa kitengo cha uchambuzi tusaidiane.
Ni mimi msaidizi wa Mh. Mwigullu, waziri wa fedha.
 
Tuseme ule ukweli utawala wa Magufuli ulikuwa na kasoro kubwa sana hasa kwenye utawala bora.
 
Ujamaa wa ccm unatokana na Rais aliye madarakani na si itikadi ya chama.

Mfano halisi ni matendo tofauti na mwelekeo tofauti wa kisera kwa awamu ya 4 na ya 5. Hatua nyingi za Kikwete zilifuata ubepari na kuacha sekta binafsi kukua na kukuza uchumi. Hatua za Magufuli , alihimiza zaidi sekta ya umma kukuza uchumi.

CCM ilifuata upepo wa maelekezo ya mwenyekiti.

La pili, huko kwenye welfare economy kanuni za kiuchumi zinatumika pia kuanzia "marginal analysis" hadi "pareto optimality" pia hufanyi jambo kwa hisia tu.

Analysisi yako ya Welfare economy ingehusu zaidi mipango ya kusawazisha kipato kusiwe na gap kubwa kati ya masikini na matajiri. Unafuu wa huduma kama za shule, maji, afya.

Miradi ya ndege haihusiani na uchumi wa wanyonge
 
Kwa lugha rahisi magufuli aliwatumia kama mtaji wa kisiasa bila kujali sheria za mazingira na biashara zinasemaje. Changamoto iliyopo wakiondolewa sasa hivi wataona kama wanaonewa.
 
well said,nitakuchagua kuwa waziri wangu wa uchumi sijaridhika na uteuzi wa Yule mwanachama wa yanga aliyeipoteza singida united
 
Ntafanya hivo, ila kwa Magufuli sekta ambayo ilifanya vizuri ni sekta ya Ujenzi, ambayo ndo imekuwa ni driver ya uchumi wa Magufuli kwa miaka 5 iliyopita, enzi ya Kikwete naweza sema sekta zote ziikuwa vibrant ndo maana watu walikuwa na pesa mfukoni.
Mkuu tafadhali usichelewe kutuwekea "sehemu ya pili"
Kwa heshima ya Ili bandiko lako tumelisambaza kwenye majukwaa mbalimbali mfano WhatsApp, Facebook, Twitter nk. Na kote huko watu watu wanaulizia sehemu ya poli ya bandiko hili.

Honestly kote huko niliposambaza sikusita kukutambulisha .
 
Yeye ndie alikuwa anasema wamachinga wasisumbuliwe wafanye biashara popote. Watendaji wake unawaonea tu.
 
Acha kupotosha, tulikuwa tunapata kodi kwa mashirika binafsi ya ndege wakati sasa hivi tunapata hasara kwa ATCL. Maelezo meengi lakini nikwambie tu hakuna kinachofanyika na ATCL sasa hivi ambacho kilikuwa hakifanyiki na mashirika binafsi. ATCL itakuwa na maana kama itatengeneza faida na si vinginevyo.
 
Mwandiko wako tu unakutanabaisha ulivyo mweupe kichwani pure mataga
Hata kama sijui kuandika,ila ujumbe umefika, serikali ya Jk ilijaa majizi wapigaji,wala rushwa,na wauza madawa ya kurevya,inawezaka nawewe ulikuwa miongoni,eti mnajifanya wachambuzi wa uchumi, wakati WB walisema uchumi wa Tanzania umekua mpaka kupifiki wa kati na GDP imepanda,eti anatoka mtu ajiita Namtombe anasema Jpm amealibu uchumi,na kuna watu wanashangiria, ukiuliza kwa takwimu zipi!unaambiwa ukuna pesa mtaani,utafikiri pesa ni mabomba ya maji kupatika kila nyumba.
 
Umeandika kistaarabu nitakujibu

Kwenye siasa za CCM umesema kweli na hili linapaswa kuangaliwa na wenye chama ili kweli kuwe na ideological differences kwa vyama vyetu na consistency isiwe individuals preferences....

Kwenye welfare economics na hasa principle ya Pareto naomba kukumbusha hizo optimal points ni multiples inategemea hiyo tangency inatokea wapi ndiyo maana siyo Pareto principle tu ndiyo itakayoamua wapi na kipi kifanyike...Kwasababu za shortfalls hizo, New instistution economics ikarekebisha kidogo na kuweka levels za social analyses, marginal increament inakuwa valid level 4 baada ya kuziweka institution environment sawa...Hiki ndicho alichoanza kukifanya Hayati Magufuli alianzia level ya chini kabisa ambayo ni social behaviour kisha akaja level 2 kuweka sheria ambazo ni appropriate; aliifanya kwenye madini kwaku define ownership ya natural resources zetu na kuwezesha bargain ili tuweze kufikia winwin positions kwa kila resources zetu, Bunge letu sasa lina uwezo wa kujadili na ku review mikataba yote ya mali asili; alitengeneza jeshi Usu kwenye renewable natural resources kuzuia uharibifu kwakua watu bado ni poor kwahiyo wana high time preferences hivyo they would be tempted kutumia mali asili kwa njia haribifu n.k kisha kilichobaki sasa ilikuwa ni kwenye mifumo yetu ya public services ambayo haina coordination zinaongeza transaction costs hakuna ufungamanishaji katika utendaji na kuna a lot of duplications na hakuna information sharing ya kutosha, hili bado ni changamoto baada ya levels hizo sasa ndiyo angeweza sasa kuja kwenye kupima ufanisi kwa marginal analysis je unatenda kwa faida au hasara? So utaona hata ndani ya miaka yake mitano na nusu kufanya hayo yote ni big plus; amejenga misingi imara katika kuelekea kwenye taasisi imara...Hata nyumba haijengwi siku moja seuze nchi?

Ulaya iliwachukua karne kufikia hapa leo tangu walipo fanya industrial revolution...Sisi nchi hii ilivurugwa misingi yake tulipo institute structural adjustments programe zizlizo re-orient nchi zote duniani katika strategic plan ya globalization...Magufuli aliitengeneza misingi upya kwakurudisha yale yaliyoharibiwa infact aliweza kuona hizo gaps na ku act accordingly...Ni jukumu letu sasa ku pick from where he left; hata hivyo mpaka sasa tupo vizuri kwakua the brain behind this ameongezwa power kwahili mama HE Samia Suluhu ameonyesha busara ya hali ya juu and I salute her...Ni jukumu sasa la Mh. Mpango kuendeleza maono yake kwa uhuru zaidi kwakuwa kapewa kazi hiyo kama mkono wa kuume wa Rais wetu Mh. Samia Suluhu Hassan...Ninawaombea utumishi mwema wa miaka yao hii 4.5
 
Okay calm down hizo kodi zilichangia kiasi gani ya GDP?

Maana mchango wa ndege kwa haraka unauonankwenye utalii na unachangia kama namba 2 kwenye GDP tena kwa figure ya 6Trillions...Hayo mashirika yalichangia kiasi gani cha kodi? Je investments zao zimo humu Tanzania? Walikuwa wanaweka pesa zao humu? Je haikuwa njia ya capital flight?
 
Hongera kwa uchambuzi yakinifu 👊
 
Uongo wa mchana EFD imeanza kipindi cha mwinyi!!!
Kwa sababu unajua ya saa sita mchana tu na hujui ya saa 11 asubuhi!! Nilikuwa na marafiki zangu tuliosoma nao ambao walikuwa maafisa wa kodi waliokuwa assigned kwenye project ya taxation computerization wakati wa Mwinyi. Kwa vile hujui hilo, basi usipige kelele; ni uungwana kukubali kuwa ulikuwa hujui hayo. siyo kwamba EFD ilizaliwa usiku mmoja tu, ni process iliyochukua zaidi ya miaka kumi!!!
 
Kodi zilichangia GDP kama zilivyo kodi nyingine. Unaposema mchango wa ndege za ATCL unaonekana kwenye utalii nashindwa kukuelewa sababu hadi sasa hatuna ndege inayoenda Marekani wala Ulaya, na hizo ndizo sehemu wanazotoka watalii au wewe mchango wa hizi ndege unauona kutoka Dar kwenda Arusha tu? Unauliza investments zao kama zipo Tanzania wakati ulikuwa unaona fast jet na precision air zinafanya kazi.
Kama kampuni inalipa wafanyakazi na kodi ya serikali kwanini uwalazimishe waweke pesa Tanzania? Kwani wameiba
 
Unatulisha matango pori alafu tukubali tu.
 
Great analysis,

Asante sana kwa bandiko zuri.
 
Jomba umejitahidi kuchambua ila sina uhakika kama wewe ni mchumi...umechambua chambua lakini sijaona namna gani revenue ya Taifa kupitia madini na maeneo yanayofanana yalikuwaje...na hujatoa forecast ambayo in relate na Mali zetu tulizonazo na namna ambavyo tutazitumia..I believe investment ilikua inafanyika kwa sababu ya assurance ya assets na Mali nyingine tulizonazo kama mineral deposits .na for sure tuna uhakika wa kukopesheka popote duniani..of which sio kitu cha ajabu..hata Marekani inakopa, hata China inakopa...na balance sheet zinakaa sawia kabisa...hujazungumzia pia tuko middle income level, how do we progress and become sustainable. This is very important .how do we foresee in the next ten to twenty years...sijui kama umesoma FYDP 2020-2025..umeifanyia analysis? Mambo yako mengi uliyozungumza yana majibu mazuri tu mule..sasa jomba jipange sawasawa...njoo na a comprehensive analysis tupate picha ya uhakika na ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…