Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza

Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza

Ntafanya hivo, ila kwa Magufuli sekta ambayo ilifanya vizuri ni sekta ya Ujenzi, ambayo ndo imekuwa ni driver ya uchumi wa Magufuli kwa miaka 5 iliyopita, enzi ya Kikwete naweza sema sekta zote ziikuwa vibrant ndo maana watu walikuwa na pesa mfukoni.
Sekta ya ujenzi na sekta ya Madini,mwaka 2019 kwenye ukaji wa Sekta ujenzi alizidiwa na Madini.
 
Kafa ukali wa maisha umepungua unakula milo mingap kwa siku vip maisha yako ya me badilika!?
Achen unafki fanyeni kazi njaa zitawaua mkiendelea kukaa umu jamiforums na kuubil kua maisha Mazur unalelewa na kiongozi ngoja tuwaone
 
Kinacho nishangaza ni Philipo mpango kusema lazima mapato yaongezeke ..
Wakati kashiriki kuumiza huu uchumi..

Angekuwa na akili angesema tuanze upya..
Nna wasiwasi Mpango anaweza asimsaidie Sana..Mama
Mpango bado ana "hegemony" ya utawala uliopita wa Magu.
Wampige "reset mode" aanze upya.

Nasubiri kwa hamu bajeti hii hasa kwenye sera za fedha na kodi tuone vitendo na maneno
 
Magufuli a.k.a Jiwe alikosa kuwa na vipaumbele alitaka afanya vyote amalize utadhani namna kiongozi atayekuja baada ya yeye.

Hata mataifa yenye Rasilimali za kumwaga za kila namna kama USA,China,Russia hawafanyi mambo yote kwa Mara moja-mwisho wa siku utafeli na utaonekana kituko kwa werevu.

Swala la Serikali kuwepo hapa duniani ni kurahisishia watu maisha-watu wapate kwanza mahitaji yao ya msingi (basic needs) vitu vingine vitafanyika taratibu-hata Roma haikujengwa kwa simu 1.

Laiti Magufuli angekomaa let's say na Bwawa la umeme tu au SGR tu na ingelamilisha kwa miaka take 5 angecha legacy kubwa sana,tatizo alijawa na tamaa alitaka akumbukwe kuliko Marais wote mwisho wake amefanya hovyo kuliko wote.
 
Kwamtizamo wangu hapa umefanya self seeking; numbers au statistics can be used any how to justify your desire...It depends on how you define your objective functions...Uchumi siyo mathematics una njia mbili za kuuelezea na katika hizo kuna judgements amabzo zinatokana na intuitions za mchumi anayezitafsiri ndiyo maana unayo field nyingi sana na kukuhakikishia hata duniani hakuna utangamano (makubaliano ya pamoja) katika maswala ya uchumi...Hata leading policy ya sustainability ina definitions zaidi ya 1000 na dunia ikaamua kuchukua ile ya UNCED 1992...

Usipotoshe watu kwa sababu zako kwenye short term na hasa unapofanya investiments kwenye uchumi hasara lazima zionekane kuwa kubwa...Nikichukulia mfano wa ATCL hilo siyo private company uifanyie financial analyses kujustify hasara zake...Project hiyo siyo mutually exclusive na zingine kama za utalii na kuongeza movements za executives katika kuwafikia projects zilizosambaa nchi nzima; tena hazi exclude umuhimu wa vyakula kama samaki ambavyo vina short shelf life na suplies wenye small capital kama small fisherfolks kumfikia consumer wa Dar ambaye ana purchasing power ndogo...Inamaana serikali imesubidies some how hizo incomes za both suppliers na consumers ambao iliwatafsiri wanyonge kwakufanya transfer kutoka kwa wale wenye uchumi mkubwa ambao ni wachache lakini wanauwezo wa kutumia ndege kuongeza tija kwenye shughuli zao (kiasi cha transfers within economy kinajionyesha kwenye hiyo gap ambayo wewe unaiita hasara kwakua unaiangalia kwa financial eye na siyo economic benefit kwa nchi kwakua zimeenda kwa hao wanyonge kuonheza welfare) ...Alichofanya hayati JPM kiuchumi ni aibu kukianza kukifanyia analyses katika hii short tem period hasa ukichukulia miaka ambayo generation ya Tanzania itaishi... Na hata huko mbele tafsiri sahihi ni kama awamu ya sita itaendelea katika trajectory ile ile aliyoianzia otherwise Tanzania haina nafasi tena ya kumhukumu hayati Dr. JPM kwakua hakumaliza term zake zote mbili ambazo ndizo alizitumia ku frame projects zake...Tutamhulumu kwa hisia na wala si kwakutumia principles za uchumi...

Tuache blame games tuijenge nchi yetu kwakumtakia amani Hayati JPM na kuendelea kumsaidia HE mama Samia katika kuiendeleza nchi yetu; yeye amefarki, apumzike kwaamani kwakua sasa historia pekee ndiyo itamhukumu. Sisi bado tunayo nafasi ya kurekebisha alipokosea na sisi pia tutakapoondoka historia mbili zitajilinganisha na kutoa hukumu ya haki.
 
Hii ni sehemu ya kwanza, nta cover sekta ya biashara, uwekezaji wa nje, viwanda, na ntaelezea kwa kina kuusu madeni ya taifa..

Ila conclusion kabisa ni kwamba 'Magufuli alichofanya ni kukopa pesa nying nje na kufanya plundering ya pesa za wafanya biashara kupitia kodi za kidhalimu ili kujenga uchumi ambao ulielemea katika projects kubwa za miundo mbinu ambayo bado hatujajua itakamilika lini'
Kwa Lugha Nyepesi tuseme ; Baba wa familia hatoi pesa ya matumizi nyumbani, watoto hawali, hawavai, ni mwendo wa Pasi ndefu na kuvaa midambwada ili pesa zote zitumike ktk ujenzi wa nyumba ya kisasa! Kipato cha Baba ni kidogo kuafford ujenzi wa nyumba hiyo ya kisasa hivyo Baba anajiingiza ktk madeni kimyakimya huku akiilaghai familia kua anajenga kwa kipato chake, Nyumba inafikia kwenye renta Baba anatangulia mbele za haki..
 
Kwa Lugha Nyepesi tuseme ; Baba wa familia hatoi pesa ya matumizi nyumbani, watoto hawali, hawavai, ni mwendo wa Pasi ndefu na kuvaa midambwada ili pesa zote zitumike ktk ujenzi wa nyumba ya kisasa! Kipato cha Baba ni kidogo kuafford ujenzi wa nyumba hiyo ya kisasa hivyo Baba anajiingiza ktk madeni kimyakimya huku akiilaghai familia kua anajenga kwa kipato chake, Nyumba inafikia kwenye renta Baba anatangulia za haki..


Hahaha You can say this again
 
Yeye alimwombea beni Saanane? Risasi 16 za lisu mbona alikataza uchunguzi huru ? Azory gwanda unadhani mkewe na watoto wako kwenye trauma kiasi gani kupotea kwa baba Yao mpaka Leo siwezi kumuombea muuwaji alieuwa watu jambazi la chato Lile Mungu ka mmute milele.
Lkn kumbuka binadamu kukosea ni kawaida yetu,mhurumie tu Mkuu
 
Kwamtizamo wangu hapa umefanya self seeking; numbers au statistics can be used any how to justify your desire...It depends on how you define your objective functions...Uchumi siyo mathematics una njia mbili za kuuelezea na katika hizo kuna judgements amabzo zinatokana na intuitions za mchumi anayezitafsiri ndiyo maana unayo field nyingi sana na kukuhakikishia hata duniani hakuna utangamano (makubaliano ya pamoja) katika maswala ya uchumi...Hata leading policy ya sustainability ina definitions zaidi ya 1000 na dunia ikaamua kuchukua ile ya UNCED 1992...

Usipotoshe watu kwa sababu zako kwenye short term na hasa unapofanya investiments kwenye uchumi hasara lazima zionekane kuwa kubwa...Nikichukulia mfano wa ATCL hilo siyo private company uifanyie financial analyses kujustify hasara zake...Project hiyo siyo mutually exclusive na zingine kama za utalii na kuongeza movements za executives katika kuwafikia projects zilizosambaa nchi nzima; tena hazi exclude umuhimu wa vyakula kama samaki ambavyo vina short shelf life na suplies wenye small capital kama small fisherfolks kumfikia consumer wa Dar ambaye ana purchasing power ndogo...Inamaana serikali imesubidies some how hizo incomes za both suppliers na consumers ambao iliwatafsiri wanyonge kwakufanya transfer kutoka kwa wale wenye uchumi mkubwa ambao ni wachache lakini wanauwezo wa kutumia ndege kuongeza tija kwenye shughuli zao...Alichofanya hayati JPM kiuchumi ni aibu kukianza kukifanyia analyses katika hii short tem period hasa ukichukulia miaka ambayo generation ya Tanzania itaishi... Na hata huko mbele tafsiri sahihi ni kama awamu ya sita itaendelea katika trajectory ile ile aliyoianzia otherwise Tanzania haina nafasi tena ya kumhukumu hayati Dr. JPM kwakua hakumaliza term zake zote mbili ambazo ndizo alizitumia ku frame projects zake...Tutamhulumu kwa hisia na wala si kwakutumia principles za uchumi...

Tuache blame games tuijenge nchi yetu kwakumtakia amani Hayati JPM na kuendelea kumsaidia HE mama Samia katika kuiendeleza nchi yetu; yeye amefarki, apumzike kwaamani kwakua sasa historia pekee ndiyo itamhukumu. Sisi bado tunayo nafasi ya kurekebisha alipokosea na sisi pia tutakapoondoka historia mbili zitajilinganisha na kutoa hukumu ya haki.

Naomba nichangie hapo kwenye ATCL.

Kwanini magufuli na serikali yake walikua wanasema ATCL inapata faida na tena inatoa mpaka gawio lakini juzi CAG akasema shirika halijawahi kupata faida?

Je kwanini walikua wanadanganya umma wa watanzania?
Screenshot_20210328-162203.jpg
Screenshot_20210328-145853.jpg
 
Hii hapa siyo kweli kwa sababu kutokuongeza kwa mishahara kulisababisha inflation Tanzania ibaki kuwa ya chini sana. Aliingia madarakani kukiwa na 5.59% na wakati anaondoka inflation ilikuwa 3.56% Kwa hiyo madai ya gharama za maisha kupanda siyo ya kweli. Tatizo lililokuwepo na mzunguko hafifu wa fedha kutokana kna kudhibiti matumizi ya pesa za serikali. Uchumi wa Tanzania umekuwa unategemea sana pesa za serikali kuliko pesa za watu binafsi; serikali ikibana matumizi ya pesa zake basi watu wanalia hawana hela. Ilikuwa hivyo enzi za Mkapa mwanzoni, na enzi za magufuli. Serikali ikishaanza kulegeza usimamaizi wa matumiz yake basi ndipo unaona pesa zinakuw nyingi mitaani na inflation inaongezeka.

View attachment 1741777
Jumlisha hizo inflation rate kuanzia 2016.. ndo mana nikasema real income imeanguka zaidi ya 18% kwa sababu serikali haikuwa inaongeza mi
shahara
 
Amejenga masoko alafu wamachinga wapo kila sehemu, nini faida yake?
Kabisa, nadharia ya machinga ni urahisi wa kutembea na bidhaa kufuata wateja walipo.

Ila kwenye hili la machinga, suala la bidhaa wanazouza liangaliwe upya. Wanauza pasi, tv, bidhaa mbalimbali zinazouzwa pia madukani tena bila risiti ya kodi. Hii imeua biashara rasmi ya rejareja pamoja na kushusha kodi.

Ushauri
machinga waundiwe sera yao itakayobainisha ni bidhaa/huduma gani wanaruhusiwa kutoa na hadi kufikia kiwango kipi cha mapato ili watoke sekta isiyo rasmi na kuingia sekta rasmi. Bidhaa ninazoona zinafaa kuuzwa na machinga ni bidhaa ghafi za kilimo, matunda mbogamboga na vyakula. Kazi/huduma za mikono yao ususi, fundi viatu, ufumaji.

Hapo juu, utaratibu wa vitambulisho uendelee n kuboreshwa ili kuwapa mazingira bora ya kufanya biashara zao

Bidhaa za viwandani (na mitumba kutoka nje ya bidhaa kama hizo) ziachiwe zifanywe na sekta rasmi kwani ndio sehemu ya kupata mapato na kuchochea ukuaji wa viwanda vya ndani.
 
Naomba nichangie hapo kwenye ATCL.

Kwanini magufuli na serikali yake walikua wanasema ATCL inapata faida na tena inatoa mpaka gawio lakini juzi CAG akasema shirika halijawahi kupata faida?

Je kwanini walikua wanadanganya umma wa watanzania?View attachment 1741943View attachment 1741944
Faida na hasara zina fuata preferences i.e stated au revealed; na inategemea zaidi jinsi unavyofanya valuation...Hakudanganya kwakua katika hotuba zake alishasema nchi haiwezi pata hasara which is correct kwenye perspective ya uchumi iwapo tu hakuna kilichotoka nje kama capital flight...Hizo zinabakia kuwa tranafers ndani ya uchumi mkubwa ni kama wewe uamue kumpa masikininpesa akanunue chakula useme eti nimepata hasara...Tusipotoshwe...Nchi miradi yake ni public na uchumi una principles zake kuna welfare economics ambayo ni tofauti kabisa na uchumi unaotokana na assumption za akina Adam Smith za theory of the agency...Na hizo pia zinatofauti na kufanya auditing za cash flows zinaweka costs ambazo kiuchumi zinaweza kuwa benefits...Hii ni taaluma ya watu na Rais alikuwa na wataalamu...Unaposema kadanganya unamkosea kwakua ungemuuliza angekujibu vizuri tu kwakua CCM ni chama cha kijamaa siyo cha kibepari...Mabepari hasara na faida wanazitafsiri tofauti na wajamaa...Hasara ya firm iliyoko Norway haiwezi kufananishwa na iliyoko America...Lakini pia hata huko America kuna public investments huwezi hata siku moja kusema eti jeshi la marekani limepata hasara kwakua uchumi wao unabebwa na jeshi...Tuache upotoshaji
 
Mtafanya Kibarua Cha Kuongoza Malaika Kiote Mbawa
 
Sekta ya ujenzi na sekta ya Madini,mwaka 2019 kwenye ukaji wa Sekta ujenzi alizidiwa na Madini.
Hatua za kuanzisha masoko ya madini kila mkoa, ukuta wa mirerani zimedhibiti utoroshaji, kuwezesha upatikanaji wa takwimu sahihi na kuongeza mapato ya sekta hii
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hongera mleta, umetuchambulia mambo ya kitaalamu kwa lugha rahisi na nyepesi kueleweka.
Ukiacha makosa ya kiuandishi (mfano; which badala ya hiki) pamoja na matumizi ya maneno (mfano; imepelekea badala ya imesababisha), uzi umeutendea haki kwa uchambuzi wako mujarabu. Hata hivyo, ningependa unapofanya comparison ya uchumi wa swami ya 5 na ule wa awamu ya 6, uangalie pia aspect ya purchasing power katika awamu hizo 2. Vilevile, jitahidi kuweka vyanzo vya takwimu unazotumia kwenye Andiko lako. Ni hayo tu, Mkuu.
 
Amejenga masoko alafu wamachinga wapo kila sehemu, nini faida yake?
Mh. Rais yeye kama individual hakuwa mchumi, kazi ya ubunifu ni ya watendaji ambao ndiyo walalamikaji wakubwa na wanaotaka kula wasichokizalisha...Tunashida kubwa kwenye wataalamu wetu katika kutafsiri njia sahihi ya kutumia public investments...Hili ni tatizo la wataalamu kutafsiri maendeleo siyo la taasisi ya u Rais na Bunge ambazo zinafanya maamuzi kwakuangalia kura
 
Kafa ukali wa maisha umepungua unakula milo mingap kwa siku vip maisha yako ya me badilika!?
Achen unafki fanyeni kazi njaa zitawaua mkiendelea kukaa umu jamiforums na kuubil kua maisha Mazur unalelewa na kiongozi ngoja tuwaone
Kuwa humu, bando linatumika uchumi unakua.
 
Hii ni sehemu ya kwanza, nta cover sekta ya biashara, uwekezaji wa nje, viwanda, na ntaelezea kwa kina kuusu madeni ya taifa..

Ila conclusion kabisa ni kwamba 'Magufuli alichofanya ni kukopa pesa nying nje na kufanya plundering ya pesa za wafanya biashara kupitia kodi za kidhalimu ili kujenga uchumi ambao ulielemea katika projects kubwa za miundo mbinu ambayo bado hatujajua itakamilika lini'
Ulichoandika kuhusu uwezekano wa miradi mikubwa kutokamilika kina ukweli aisee.

Kuna siku hapa juzi kati nilikuwa naongea na mtu fulani ambae yupo deep kabisa ndani ya mfumo - akaniambia bila kupepesa macho kuwa mama Samia amerithi bomu linalosubiri kulipuka wakati wowote kwani serekali haina pesa kabisa ya kukamilishia hiyo miradi mikubwa iliyoanzishwa na Magufuli. Kwamba Magufuli tayari alishamaliza kukamua maziwa yote kila mahali na hakuna cha kukamua tena, so jamaa akawa anajiuliza sijui mama Samia atafanya fanyaje maana hata deni letu la taifa ni kubwa sana (in fact ni kubwa kuliko hata alivyokopa JK kwa miaka yake yote 10).

A bump ride awaits. Brace yourselves up ndugu wanyonge!
 
Jumlisha hizo inflation rate kuanzia 2016.. ndo mana nikasema real income imeanguka zaidi ya 18% kwa sababu serikali haikuwa inaongeza mi
shahara
You cannot eat what you did not produce hii ni sheria mama ya uchumi...Mshahara uupate kwenye nini wakati wewe umeshindwa ku add value kwenye miundombinu uliyojengewa kwa kodi za raia? Watu wanasema hapa Machinga complex imebaki wazi; hamsaidii raia waweze kutengeneza corprates waweze kuwa na mjtaji itakoyoendana na projects hizo kubwakubwa...are you not ashamed kuwa cry baby? Ukishindwa wewe usitusingizie wenzako step down give others chance to do what you failed to do...Kuna vijana wengi mtaani wenye uelewa mkubwa ambao hawana ajira wewe salary yako ni cost kwa nchi ndiyo maana tunaona inefficiency ya hali ya juu kwenye uchumi...Sector pekee iliyokubwa ni service sector hakuna ubunifu katika hiyo sector zaidi ya kupokea mishahara na kuongeza statusquo; hata kutengeneza ajira ni shida, wao kila siku ni kufikiria posho na safari zisizo na tija; kuwaza lini zile hawks investments zao za hotel zitaanza kutumia public funds kujiendesha; what a poor mind?

.....Katibu mkuu kiongozi kaliona hilo na ndiyo maana kasema in a way kuna coordination failure...Infact Mh. Magufuli alitupa big push lakini kwakua sector ya employees ilikuwa non coordinated ikawa ina transaction costs kubwa sana ndiyo maana hata alishindwa kuongeza mishahara...
 
Hizi takwimu mbona zinaishia kwa kikwete, tupe za magufuli.
Kama hujui kusoma chati omba watu wakusadie chati hizo zipo kwenye vipindi vya miaka mitano mitano. Kikwete alimaliza utawala wake mwaka 2015, je aliacha inflation ya kiasi gani? Chati hiyo inaishia mwaka mwanozni mwa 2020 ikiwa ni miaka takriban mitano tangu Kikwete aondoke madarakani.
 
Back
Top Bottom