Tuweke ukweli hapa; nini hasa chimbuko la ugomvi wako na jirani yako?

Uchawi, nasikia ukimpa shs 10,000/= huyo mama anakutembelea usiku.
 
Wengine Ni mazoea wengine Ni urithi

Kuna mdada ni mke wa mtu akimuona mtu hamjui anamuomba amnunulie soda,anaowajua ni balaa anapenda kuomba omba sijui kwanini na anaona kawaida na sio kwamba hana uwezo
 
nililewa kwakua milango yetu inafata nkajkuta nmelala seblen kwake et akamaind mpaka leo atusemeshan nangoja mkesha wa pasaka nilewe nkanye mlangon kwake
Lete mrejesho vipi pasaka ulishusha mzigo mlangoni kwa jirani?
 
Kuna mdada ni mke wa mtu akimuona mtu hamjui anamuomba amnunulie soda,anaowajua ni balaa anapenda kuomba omba sijui kwanini na anaona kawaida na sio kwamba hana uwezo
Huyo mkuu,kifupi -
Ana tatizo la kisaikolojia
au kirefu-
anajitakisha kwa nguvu
 
fensi ipo na bado mnagombana.je ingekuwa changanyikeni uswahilini?[emoji3][emoji3][emoji3]
 
pole mkuu......majirani ni mitihani kwa nchi zetu hizi africa...
 

Mm napenda kunywa pombe kwa raha zangu lkn nikijinywea pombe zangu bila kugombana na mtu nikifika zangu nyumbani najiimbiaga nyimbo zangu usiku kucha lkn cha ajabu et wamenipeleka serikari za mitaa et nawapigia kelele yaan majilani ni wakorofi sn iv namawazo ya huhama zangu.
 
😂😂😂 We jamaa kwa vijinyimbo vyako Ni kajiukorofi ka chinichini
 
Kwahiyo nani mkorofi kati yako na wao?
Naomba jibu pombe ikiisha kichwani
 
Ukijaaliwa
1- mke mwema
2- Jirani mwema
3- Kipando kizuri

Aisee shukuru sanaa na na maisha utaenjoy sanaaaa
 
Mimi BADO ni mwanafuzi na sijajenga, Naishi room ya kupanga. Kwenye haya maisha nilichojifunza ni kwamba majirani wengi hawana shida. Tatizo litaibuka mkishazoeana. Mwanzoni Mazoea huonekana mema lakini baadae huleta dharau na magomvi yasiyo na ulazima. dawa ni ku hide details zako majirani wasikujue kwa undani. Na katika Hili Mimi nimefaulu. Ni mwaka wa tatu hapa nilipopanga lakini hakuna jirani anayenifahamu kwa jina langu halisi Wala kazi ninayoifanya hapa mjini. Wanafunzi wenzangu wanajua kuwa Mimi Ni Mkurya wa Mara wakati Hata Sina vinasaba vya Wakurya Wala sijawahi kufika Mara. Hide_your_details

Unakuta mtu anafahamiika kwa undani kiasi kwamba mtu yeyote anaweza kumuelezea in and out plus personal future plans! Mtu wa aina hii ni rahisi kuwekewa vikwazo kwenye safari yake ya maisha kwa sababu maadui wapo na hawana alama na shida ni kwamba maadui wengi ni miongoni mwa ndugu na watu unaocheka nao kila siku. Hide_your_details_as_much_as_you_can
 

Hii ya kuuziwa njia inakuwaje mdau
 
Usipende kugawa hela utafungiwa riziki mpe mtu anachohitaji sio hela utakuwa masikini wa kutupwa
 
Wapo pia majirani wanaojenga hadi kiwanja wanamaliza halafu paa la nyumba linamwaga maji kwa jirani ilimradi tu wawakere!
Kwenye nafikiri iwepo haja ya kuwa na public sewage system na uwepo wa vibali vya ujenzi.
 
Nipo na jirani yangu paka wangu alihamia kwake mwanzoni alikuwa anaonesha kumjali lakini alipozaa akaanza kuuza vitoto vyake kimya mya sasa na jana nimemtolea uvivu nikamwambia najua paka wangu amezaa ole wako uviuze utajuta binadamu kazi kweli kweli mi nadhani bora kuonekana kauzu kuliko kuwa na watu wabovu eti majirani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…