Tuzo Ndg. Yeriko Nyerere itupe funzo kuthamini 'big brains' wa ndani ya nchi

Tuzo Ndg. Yeriko Nyerere itupe funzo kuthamini 'big brains' wa ndani ya nchi

Wewe mpuuzi sasa wote tukiwa waandishi wa vitabu mambo yataenda? Wengine tubaki kuwa wateja wa vitabu
Hata wewe unatakiwa uandike kitabu ikiwa Kuna Cha maana umewahi kufanya duniani, watu wajifunze.

Anyway, kitabu Gani umewahi kukisoma ukamaliza pages zote na kukielewa.
 
Mkuu umeshawahi kusoma hicho kitabu? Yeriko kakopi makala nyingi za Mzee Mihangwa. Hakuna alichotunga pale.
Tuzo zilizotolewa ni za mtunzi bora au mwandishi bora?
Tuelewe content jamani.
 
Kitabu kisomwe na wataalamu wa uchumi tungekuwa mbali???

Hivi wachagga wanasoma kitabu gani Cha uchumi?
Mtu anaandika kitabu Cha ujasusi wa uchumi wa academia !
Kuna kina mangi wako Dar es salaam stock exchange wanakimbiza ni Hatari ,hao ndio wafanye review ya hicho kitabu Kisha watushauri.
Mentorship mentorship mentorship
Huu ndio ujasusi wa kichagga.
Sio watu wa academia kupromote legacy ya mwalimu eti Yericko na kitabu chake na hata kiduka hajawahi miliki.
Good read though 🥴

Acha kelele Yakhe😀
 
Mwandishi Bora wa vitabu Afrika.
Niliuliza makusudi,ili huyo jamaa aliyekua anapinga utolewaji wa tuzo husika,aone asivyojua alichokomenti.Ni mjinga tu,atakayebeza hiyo tuzo na jitihada za Yericko,katika uandishi wa vitabu.
 
Niliuliza makusudi,ili huyo jamaa aliyekua anapinga utolewaji wa tuzo husika,aone asivyojua alichokomenti.Ni mjinga tu,atakayebeza hiyo tuzo na jitihada za Yericko,katika uandishi wa vitabu.
Uchama ni cancer ingine inayosambaa Kwa Kasi kubwa sana nchini.
 
Salaam, Shalom!!

Nchi yetu imeng'ara tena katika bara la Afrika baada ya kijana Mahiri, ndugu Yeriko Nyerere kutuletea Tuzo Bora kabisa ya uandishi Bora wa vitabu kwa Afrika nzima.

Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi iitwayo, ZIKOMO AFRICA AWARDS yenye maskani yake nchini Zambia iliyotokewa November 2023, Yericko Nyerere akiwa mtanzania pekee aliyechaguliwa kushiriki.

Tuzo hiyo imekuja miaka 6 baada ya kitabu alichoandika ndugu yetu Yeriko Nyerere juu ya Ujasusi wa kidola na kiuchumi.

Ujasusi kidola katika Usalama kama nchi tupo vizuri, Hilo halipingiki, ila Ujasusi kiuchumi, naona Bado tunasuasua. Ikiwa kitabu hiki kingesomwa na wataalamu wetu wa Uchumi Kwa kipindi Cha miaka 6 iliyopita na kifanyiwa KAZI, naamini tusingekuwa hapa tulipo.

Yaani ndugu Philip Mpango na ndugu Mwigulu nchemba, wangechukua haraka ushauri na madini katika kitabu cha mtanzania mwenzetu, tusingekuwa Bado tunafanya na kupita njia tunayopitia kiuchumi.

Tungesoma kitabu hiki kisawa sawa, tusingekubali kukodisha Bandari zetu kwa wageni, kuuza misitu na madini kiholela.

Najua hatujachelewa, tunaandika Katiba mpya, pia tunaelekea Uchaguzi, vyama vinaandaa Ilani zao Kwa mwaka 2025-2030, chonde chonde, msiache kuchungulia kitabu hiki Hasa kuhusu Ujasusi wa kiuchumi, kuona namna gani mtatoa dira nzuri kuhakikisha raslimali zetu zinatunufaisha na kututajirisha Watanzania.

NB: Roho mbaya haijengi, linapokuja suala la Maslahi mapana ya nchi, tuwe kitu kimoja bila kujali, Yeriko Nyerere ametoka CHADEMA au la, Tanzania kwanza.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿.

Aamen.

Cc: Yericko Nyerere.
Kupongeza na kusujudia tumuachie Nani?
 
ni kataasisi ka hovyo kwe ye tuzo zake

mpaka ommy dimpoz kawekwa et msanii bora wa mwaka

mtu ambaye hana wimbo mwaka mzima



msanii bora wa hip hop pia joh makini yupo sijui kama mnakubaliana nayo hii


msanii bora wa kike irine Robert naye kashiriki

mi hata kumjua simjui


so yeriko kupewa haka basi apewe tu taasis ambayo imemtunuku sio ya kitaaluma kabisa

ni kama kill music award kwa kwetu enzi hizo
hakuna jopo la maprof wataalamu walaaaaa
 
ushahidView attachment 2833390View attachment 2833391
Screenshot_20231205-001213_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom