Katika soko huria sioni hii kitu kama inaweza kufanya kazi.
Pia ushirika ni watu waliojiunga sio watu wakiolazimishwa kuwemo.
Ushirika uliopo si enclusive kwahiyo wakulima wanalazimishwa kuwemo.
Fikiria mkulima amelima kwa gharama zake halafu unampangia auze kwa mfumo gani. Je unajua wakati analima alipata wapi mtaji wa kulimia?
Hizi sheria hazijazingatia hali halisi ya mkulima, ushirika sio ujamaa, na kama ziundwa kipindi cha Ujamaa ambao umeshindwa kufanya kazi zifumuliwe upya zifanywe kuzingani hali ya mkulima mdogo pia.
Kila sehemu Ushirika haujapata kuungwa mkono na walio wengi si kwa sababu ni mbaya lakini ni kwa sababu unanyang'anya power ya mkulima juu ya mazao yake.
Mfano ikiwa mkulima amepata Pamba yake kidogo na anahitaji kupeleka mtoto wake shule kwa hela hiyo hana asses nayo kwa haraka, atalazimika asubiri mnunuzi au mnada kupitia ushirika ambaye hatampa pesa siku hiyo, atalazimika kufungua akaunti na kukatwa riba ya benki
Maafisa ushirika watoe elimu kwa wakulima ili wauelewe na kuupokea sasa hivi ni mfumo unaoshuka toka juu kuja chini kwa utekelezaji, wakulima ambao ndio wahusika hawajui kinachoendelea.
Soko ndio jambo nyeti. Ushirika wajiulize lengo la kuunganisha watu ni nini?
Je wanaibiwa na makampuni kwa kukosa uelewa wa masoko?
Je wanapata jukwaa ambalo wanaweza kukuza uwezo wa kuzalisha?
Yaani kwanini mkulima awe na ushirika?
Majibu wajibu yakiwa na manufaa chanya, sio chanya kwa serkali, la sivyo ushirika utabaki wa serkali sio wananchi