TV1 Kurusha Live ligi kuu ya Uingereza(EPL)

Itakuwa poa, kama wanaweza kuonyesha mechi anagalau 3 kwa siku zinazoonyeshwa muda tofauti itakuwa safi.
 
Wengi wanafikiri kuwa sasa TV1 inaenda kurusha mechi zote za epl kama supersports.Haki ya matangazo yakulipia kwa ukanda wa jangwa la sahara bado dstv wana exclusive right.Njia hii ya kununua ili kuuza ndiyo pekee inampa muuzaji haki yakurusha mechi zote kwa wateja wake kupitia chaneli atakazozichagua.Hapa sasa ndo unaona dstv wanarusha kupitia supresports channels.

Njia nyingine ni kununua mechi moja ya jumamosi itakayochezwa kati ya saa nane mchana mpaka saa kumi za uingereza.Mnunuaji wa haki hii yeye analazimika kutouza hizo mechi,anatakiwa kuzirusha kupitia free to air channels(FTA) ambazo atakuwa ameingia nazo makubaliano ya kibiashara.Hapa sasa unawakuta ECOMAT wa Zimbabwe ambao wamepewa haki hizo mpaka msimu wa 2018/19.Wao watarusha hiyo mechi moja ndani ya muda huo tajwa siku ya jumamosi kupitia hizo TVs.Moja ya hizo TV ni TV1 ambao wamekubaliana na ecomat kurusha mechi moja siku ya jumamosi kwa hapa Tanzania na popote inapofika TV1 ndani ya kusini mwa jangwa la sahara.

Kwahiyo sio kama watu wengi walivyoelewa.Ukiangalia ratiba ya epl mechi nyingi kali hazichezwi jumamosi.Na hata zile kali chache zilizopangwa jumamosi hazichezwi muda huo ulioruhusiwa kwa tv za FTA.Hii inafanywa makusudi ili kuto wakosesha wateja watu wa pay TV kama dstv ambao wanalipa pesa nyingi kununua hizo haki.

Kwa hiyo umuhimu wa dstv kwa hapa bongo bado hauwezi kupunguzwa hata kidogo na hili suala la TV1.Kuna jumamosi zitakuwa hazina mechi hata moja kwa watu wa FTA kwakuwa tu mechi siku hiyo zinaanza late,zaidi ya ule uliokuwa stated kwenye mkataba wao na epl board.

Kwa makadirio ya mechi moja kila wiki tv1 wangerusha mechi 33 tu kwa msimu mmoja.Lakini kwa sababu ya limitation ya muda ni dhahiri zitakuwa chini ya 33.Sasa unawezaje kuibana dstv mwenye mechi 330 kwa season za epl huku wewe unapewa mechi chini ya asilimia 10 tena za kuchaguliwa kimkakati?
nimekuelewa VEMA
 
Ajitokeze na mwingine aoneshe CHAMPIONS LEAGUE aisee tuache kwenda kwenye vibanda umiza usiku ndoa zinatetereka sana
 
1470301671564.jpg

Mmeliwa
[emoji125] [emoji125] [emoji125]
............
 
Wengi wanafikiri kuwa sasa TV1 inaenda kurusha mechi zote za epl kama supersports.Haki ya matangazo yakulipia kwa ukanda wa jangwa la sahara bado dstv wana exclusive right.Njia hii ya kununua ili kuuza ndiyo pekee inampa muuzaji haki yakurusha mechi zote kwa wateja wake kupitia chaneli atakazozichagua.Hapa sasa ndo unaona dstv wanarusha kupitia supresports channels.

Njia nyingine ni kununua mechi moja ya jumamosi itakayochezwa kati ya saa nane mchana mpaka saa kumi za uingereza.Mnunuaji wa haki hii yeye analazimika kutouza hizo mechi,anatakiwa kuzirusha kupitia free to air channels(FTA) ambazo atakuwa ameingia nazo makubaliano ya kibiashara.Hapa sasa unawakuta ECOMAT wa Zimbabwe ambao wamepewa haki hizo mpaka msimu wa 2018/19.Wao watarusha hiyo mechi moja ndani ya muda huo tajwa siku ya jumamosi kupitia hizo TVs.Moja ya hizo TV ni TV1 ambao wamekubaliana na ecomat kurusha mechi moja siku ya jumamosi kwa hapa Tanzania na popote inapofika TV1 ndani ya kusini mwa jangwa la sahara.

Kwahiyo sio kama watu wengi walivyoelewa.Ukiangalia ratiba ya epl mechi nyingi kali hazichezwi jumamosi.Na hata zile kali chache zilizopangwa jumamosi hazichezwi muda huo ulioruhusiwa kwa tv za FTA.Hii inafanywa makusudi ili kuto wakosesha wateja watu wa pay TV kama dstv ambao wanalipa pesa nyingi kununua hizo haki.

Kwa hiyo umuhimu wa dstv kwa hapa bongo bado hauwezi kupunguzwa hata kidogo na hili suala la TV1.Kuna jumamosi zitakuwa hazina mechi hata moja kwa watu wa FTA kwakuwa tu mechi siku hiyo zinaanza late,zaidi ya ule uliokuwa stated kwenye mkataba wao na epl board.

Kwa makadirio ya mechi moja kila wiki tv1 wangerusha mechi 33 tu kwa msimu mmoja.Lakini kwa sababu ya limitation ya muda ni dhahiri zitakuwa chini ya 33.Sasa unawezaje kuibana dstv mwenye mechi 330 kwa season za epl huku wewe unapewa mechi chini ya asilimia 10 tena za kuchaguliwa kimkakati?
Ww Kichwa Bwa Sheeee
daaah bora, ila watarusha mechi ngapi kwa siku au week?
 
Very expensive Ni shilingi ngapi, usiongee kitu usichokijua, maana hujui hata bei ya kulipia kuonesha EPL, usiongee chochote Kama huna facts.

Aliposema itakuwa bure (ingawa sina uhakika) Alimaanisha kuwa ligi itaoneshwa bure, hapo amekonsida watu wenue ving'amuzi vya startimes ambapo gharama za king'amuzi zimeshajumlishwa na ndiyo maana ukaambiwa hawaraongeza gharama yoyote kwa ajili ya Tv one.

Issue ya kununua Na kufunga (ingawa siyo vyote vinatumia dish) ving'amuzi vya startimes Ni issue moja, Na kulipia Ni issue nyingine, so usitake kuonekana wajua

Sawa meneja mauzo wa Startimes.

Kwa faida yako tu ni kuwa;

1. Kama kweli jamaa zako wamepata exclusive right ya kurusha matangazo ya mpira - EPL, maana yake ni kuwa wamelipia. Wao watakakuwa wanafanya biashara ya wapi wakuruhusu wewe uangalie bure tu?

Hakuna cha bure dunia ya leo wewe. Narudia tena kusema, kwamba, jiandae kutoroshwa na baadae ni lazima tu ulipe price ya kutoroka!!

2. Sasa hapo bure iko wapi iwapo wameongeza channels ikiwemo hiyo ya kurusha EPL bureeee??

I am sorry mimi situmii king'muzi cha Startimes. Labda naomba unielimishe, kwamba wateja wa Startimes hawana monthly subscription fee kulingana vifurushi anachopenda mteja?

Kama ipo, then tell me. Utatenganishaje monthly subscription fee, gharama ya kununua dish/king'amuzi na gharama za ufundi kwa ku conclude kuwa ni mtatazama ligi kuu ya Uingereza bure eti kupitia kituo cha runinga cha TV1?

Nimefanya research mkubwa. Na kwa faida yako ni kuwa, mimi ni subsriber wa DSTV kwa zaidi ya miaka kumi sasa

Sijui wao wamelipia kiasi gani kupata haki ya kurusha mechi zote za EPL, LA LIGA na ligi zingine. Lakini ni wazi wamelipia fedha nyingi tu kwa kuthibitishwa na bei ya vifurushi vyao kwa mwezi ambavyo ni;

1. PREMIUM- TZS 216,000/= utaona zadi ya channel 300 na EPL mechi zote

2. COMPACT PLUS - TZS 147,000/= na utaona zaidi ya channel 250 na EPL mechi zote

3. COMPACT - TZS 84,500/ na utaona zaidi ya channel 120 na EPL mechi zote

4. FAMILY - TZS 51,000= na utaona zaidi ya channel 90 na baadhi ya mechi za EPL na LA LIGA kati ya mechi mbili au tatu kwa wiki

5. ACCESS - TZS 23,500/= na utaona baadhi ya mechi za EPL na La Liga kati ya moja hadi mbili kwa wiki

Kwa kigezo cha bei ya vifurushi vyao tu hawa jamaa wa DSTV/MultChoice ni wazi kuwa hata wao wanalipa fedha nyingi kutoka kwa wamiliki wa vituo vya runinga ambavyo wameviingiza ktk king'amuzi chao!!

Unataka utafiti gani tena zaidi ya hii fact?
 
Sina uhakika sana lakini nakumbuka kama hii TV1 ina ufadhili kutoka serikali ya Denmark kwahiyo yawezekana wamewapiku DSTV.
Tv1 wana channel moja tu sio rahisi wao kuonyesha mechi zote, hapa itakuwa kama TBC ya Tido muhando mechi 1 kwa wiki
 
Hiyo match moja azamtv huwa tunaona kwenye crtv au ktn huwa wanaonyesha ya jumamosi saa 12 jioni na ndiyo hiyo pia ting wanaonyeshaga.
 
Hapa utakuta kuna Big match mfano Liverpool na Man wao wanaonyesha Hull na Sunderland
 
Ninachohisi me nikiwa hawa Tv1 watakuwa wanaonyesha match day 1 kila wiki kama ambavyo dstv huwa wanarusha match moja moja katika kifurushi cha bomba kupitia supersport select hivyo hata Tv1 wanaweza kuwa na package hiyo ambayo sio mbaya kwa kuanzia ila kuniambia match zote siamini wakati wao wanastation moja tu,me sikurupukii hivyo vifurushi ntaendelea kustream online mpaka nione hayo mambo ya bure yapo stable,Japo Kuna jambo linaniacha mdomo wazi nimelipia dstv bomba nashangaa wamefungua ss5,ss7 na ss12 sijajua kama ni kwangu au kwa wateja wote na lengo Lao nini kwani hizi channel zilikuwa bouquet ya Compact plus

Exactly mkubwa!

Hata mimi kwa kuwa msimu wa ligi kuu hasa za Spain na England haujanza, niliamua kulipia kifurushi kidogo kabisa cha ACCESS/DSTV BOMBA na nimeshangaa wametuachia na channels tatu za sports (SS5, SS7 na SS12) wakati kabla ya hapo channels hizi zilikuwa zinapatikana kuanzia kifurushi cha Compact, Compact Plus na Premium tu ambayo monthly subs fee zake ni kubwa zaidi inayo range kuanzia 84,500 - 216,000!!

Kwenye kifurushi hiki i.e ACCESS/DSTV BOMBA, channels za sports zilikuwa tatu tu; SS BLITZ, SS select33 na SS Select34. Kama wameongeza na hizi, niwapongeze DSTV na Multchoice kwa ujumla kwa kutujali na kutupenda wateja wao.

Hata hivyo, naona SS12 ni maalumu kwa habari na matukio ya Olympic Games huko Rio De Janeiro, Brazil

All in all nadhani wameamua kuboresha vifurushi vyao na mimi nasema wamefanya jambo jema. Kumbu kumbu zangu zinaniambia kuwa SS5 huwa wanarusha mechi nyingi tu za EPL kwa wiki na SS7 huwa ni maalumu kwa mechi za La Liga.

Natumaini hata subscribers wa DSTV BOMBA/ACCESS nao wataweza sasa kuona mechi zaidi nyingi za EPL na La Liga kwa msimu huu na misimu ijayo
 
Ngoja nikalipie Dstv fasta, najua pesa yangu itarudi kupitia viingilio vya mashabiki.

Wabongo wanapenda sana mpira wa mbele..
 
Sawa meneja mauzo wa Startimes.

Kwa faida yako tu ni kuwa;

1. Kama kweli jamaa zako wamepata exclusive right ya kurusha matangazo ya mpira - EPL, maana yake ni kuwa wamelipia. Wao watakakuwa wanafanya biashara ya wapi wakuruhusu wewe uangalie bure tu?

Hakuna cha bure dunia ya leo wewe. Narudia tena kusema, kwamba, jiandae kutoroshwa na baadae ni lazima tu ulipe price ya kutoroka!!

2. Sasa hapo bure iko wapi iwapo wameongeza channels ikiwemo hiyo ya kurusha EPL bureeee??

I am sorry mimi situmii king'muzi cha Startimes. Labda naomba unielimishe, kwamba wateja wa Startimes hawana monthly subscription fee kulingana vifurushi anachopenda mteja?

Kama ipo, then tell me. Utatenganishaje monthly subscription fee, gharama ya kununua dish/king'amuzi na gharama za ufundi kwa ku conclude kuwa ni mtatazama ligi kuu ya Uingereza bure eti kupitia kituo cha runinga cha TV1?

Nimefanya research mkubwa. Na kwa faida yako ni kuwa, mimi ni subsriber wa DSTV kwa zaidi ya miaka kumi sasa

Sijui wao wamelipia kiasi gani kupata haki ya kurusha mechi zote za EPL, LA LIGA na ligi zingine. Lakini ni wazi wamelipia fedha nyingi tu kwa kuthibitishwa na bei ya vifurushi vyao kwa mwezi ambavyo ni;

1. PREMIUM- TZS 216,000/= utaona zadi ya channel 300 na EPL mechi zote

2. COMPACT PLUS - TZS 147,000/= na utaona zaidi ya channel 250 na EPL mechi zote

3. COMPACT - TZS 84,500/ na utaona zaidi ya channel 120 na EPL mechi zote

4. FAMILY - TZS 51,000= na utaona zaidi ya channel 90 na baadhi ya mechi za EPL na LA LIGA kati ya mechi mbili au tatu kwa wiki

5. ACCESS - TZS 23,500/= na utaona baadhi ya mechi za EPL na La Liga kati ya moja hadi mbili kwa wiki

Kwa kigezo cha bei ya vifurushi vyao tu hawa jamaa wa DSTV/MultChoice ni wazi kuwa hata wao wanalipa fedha nyingi kutoka kwa wamiliki wa vituo vya runinga ambavyo wameviingiza ktk king'amuzi chao!!

Unataka utafiti gani tena zaidi ya hii fact?
Vizuri, ila facts ulizitoa Ni khs DSTV, Startimes wana monthly subscription fee ambayo Ni ndogo Sana, Na Wao hawaoneshi EPL, hapa anayeonesha (kulingana Na maelezo yake) Ni TV1, siwezi jua wametumia njia gani kupata hiyo right Na wanalipa kiasi gani.
 
Back
Top Bottom