Twaha Kiduku aondoka na gari baada ya kumtwanga Dullah Mbabe

Twaha Kiduku aondoka na gari baada ya kumtwanga Dullah Mbabe

Dulla mbabe kituangusha

Wanaume wa dar waache kula chipsi, na miguu ya kuku

images (8).jpeg

Mtakuwa mnabondwa kila cku
 
Mtoto wa kilugulu anatafutia pumzi milimani, baada ya hapo anakula mkembe na delega.
 
Business kuu ya Mdhamini ni kuuza Magari. Akitoa gari anakuwa ana tangaza biashara kirahisi kuliko kutoa fedha.
Ina maana wanatoka mikono mitupu? Aliyepigwa hapati hata mil 5??? Au mshindi haondoki na pesa zaidi ya Gari??
 
Gari la kwenye promo ni tofauti na uhalisia wa alilopewa mshindi.
 
Dula mbabe hamna kitu kabisa...round zote katwangwa ukitoa hiyo ya kwanza...staaa Kiduku alivyokosa balance na kudondoka
 
Ina maana wanatoka mikono mitupu? Aliyepigwa hapati hata mil 5??? Au mshindi haondoki na pesa zaidi ya Gari??
Kabla ya pambano mabondia wanaingia mkataba na mdhamini na wanakubaliana malipo kabisa na wakati mwingine wanalipwa kabisa.
Lile gari lilikuwa ni zawadi ya ziada tu. Alitokea mdau mwingine akaongeza zawadi ili kuwahamasisha mabondia wajifue zaidi kupendezesha pambano.
Malipo ya mabondia yanategemea uhodari wa bondia.
Katika pambano la Dulla na Kiduku, Kiduku amelipwa zaidi kwakuwa ndiye mshindi wa pambano lililopita.
 
Ila ile ngumi ya mbabe ilikuwa kali naona alifungia power bank ndani ya gloves
 
Mi sijaelewa hizo pointi zinahesabiwaje! Kiduku kuanzia raundi ya pili, kamtandika sana mpinzani wake. Nilitegemea pointi za Dula, zingekuwa nusu ya za Kiduku. Lakini mwishoe, imekuwa 98 kwa 91.
Hata hivyo, Dula, angekaza mwendo, alikuwa amalize mchezo raundi ya kwanza tu!
Huwa wanafanya hivi,ukishinda round unapewa point kumi na ukishindwa round unapewa point 9!Na ikitokea ukaangushwa basi mwenzako anapewa point 10 na wewe unapewa point 8 katika round husika!
So Twaha kashinda round 9 kati 10 so ni 9*10=90,ongeza na point 8 za ile round ya kwanza aliyoangushwa inakuwa 98!

Dulla mbabe kapigwa round 9 so ni 9*9=81,jumlisha na round ya kwanza aliyoshinda so inakuwa 10+81=91!

NB:Hata kama umepigwa ngumi 15 na wewe hujapiga ngumi katika round husika basi aliyepiga ngumi nyingi anapewa point 10 na aliyepigwa 9!Ukipigwa na kuanguka zinatolewa point 2!
 
Ila ile ngumi ya mbabe ilikuwa kali naona alifungia power bank ndani ya gloves
Mchezo haukuwa mzuri,ule wa awali kabla hawajapanda akina Twaha ndio ulikuwa mchuano haswaa!
 
Kabla ya pambano mabondia wanaingia mkataba na mdhamini na wanakubaliana malipo kabisa na wakati mwingine wanalipwa kabisa.
Lile gari lilikuwa ni zawadi ya ziada tu. Alitokea mdau mwingine akaongeza zawadi ili kuwahamasisha mabondia wajifue zaidi kupendezesha pambano.
Malipo ya mabondia yanategemea uhodari wa bondia.
Katika pambano la Dulla na Kiduku, Kiduku amelipwa zaidi kwakuwa ndiye mshindi wa pambano lililopita.
Hivi Yule aliekimbiaga na hela za Mabondia Yupo?
 
Pambano lingenoga angewekwa Yule alie chukua mkanda, na twaha kiduku, Yule jamaa anaenda kwa wanaume kasuka, twaha kanipa raha sana, usiku wa Leo!
 
Gari la kwenye promo ni tofauti na uhalisia wa alilopewa mshindi.
Azam wapo vizuri sana hawataki dhuluma wala ujanja ujanja, hilo gari lipo vizuri na kwenye hali nzuri. Msangi alileta ujanja ujanja wake kwa kuwadhulumu mabondia, Azam wakamwambia hawato onyesha mapambano yoyote yanayo andaliwa na yy na ndio maana siku hizi Msangi kapoa sana.

Huyo promota aliye andaa hilo pambano ni Kepteni wa JWTZ hana huo ujinga wa kutoa zawadi famba.
 
Back
Top Bottom