Sisi sio Rwanda huwezi fananisha nchi iliyojengwa katika misingi ya umoja, amani, mshikamano, uhuru, haki za binadamu na demokrasia na nchi waliouana wenyewe kwa wenyewe kwenye mauaji ya kimbari.Suluhu pia sio kukata watu vidole vyao, kuchoma mali za watanzania wenzako wanaotafuta kama wewe, kuchoma miundombinu tuliyojenga kwa misaada na mikopo inayotumiwa na watanzania wa kawaida kabisa. Kama ukifanya hivyo unaactivate mode ya the survival of the fittest. Ukishindwa kwenye mpambano jitahidi kubali yaishe bila kutoa milio ya kuomba huruma za dunia. Kwakuwa dunia pia inafahamu kwanini yamekupata.
Kama mbinu zako zisipofua dafu kaa kimya mshukuru mungu na ukubali matokeo ya kamali uliyoicheza.
Tuache vitendo vinavyoidumaza nchi yetu, fedha nyingi inaweza kutumika kulinda dola isianguke badala ya kutumika kwenye miradi ya mkakati yenye manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi. Rwanda inawasaka maadui wake hata kama wamejificha kwenye matumbo ya samaki majini, kwa ni swala la muda kumpata adui yao. Kufanya hivyo wakati mwingine kunatumia fedha nyingi sana, tena za kigeni.
Rwanda inabidi wajifunze siasa kwetu na si vinginevyo