Twaha Mwaipaya: Namna ya kujilinda, hatupo salama, chukua hatua hizi

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,815
Reaction score
103,955
NAMNA YA KUJILINDA- HATUPO SALAMA.

1746513387144.png

NAMNA YA KUJILINDA HATUPO SALAMA

.1.Usipende kuwasha location ya simu yako kila mara.

2.Usipende kutembea mwenyewe nyakati za usiku.

3.Hakikisha kabla hujalala kuna mtu umempa taarifa au umemtakia usiku mwema na amejua upo wapi.

4.Wakija watu kukukamata hata wakijitamburisha kwamba wao ni Polisi hakikisha kuna mtu amejua, wakitaka kukuchukua kwa nguvu lia kilio cha kufiwa na mama.

5.Ukitongozwa na Binti au Binti akijilengesha kirahisi kaanae mbali.

6.Rafiki yako akikupigia simu mkutane, hakikisha kuna mtu amejua, anaweza akakamatwa yeye ili wakupate wewe.

7.Usipende kununua Luku kwa njia ya simu kwani, watekaji wana uwezo wa kujua unaishi maeneo gani kirahisi zaidi.

8.Ukipita maeneo ukiwa na mashaka chukua simu mpigie mtu uwe unatembea huku unaongea nae ukigushwa tu, mwambie huyo mtu kwamba unatekwa.

9.Usiishi kama mfu, muombe Mungu, pia ishi vizuri na watu watakusaidia siku moja.

UTAJUAJE KAMA UNAELEKEA KUPOTEZWA.

1.Hata kama umekamatwa na watu waliojitamburisha kwamba ni Polisi ila ukienda kituoni hautaingizwa kwenye reja book.

2.Ukiona umeenda kituo cha Polisi umewekwa chumba cha peke yako na vyumba vingine vikiwa na watu hakikisha ukipata upenyo unatoa ujumbe wakusema wewe ni nani na umetokea wapi, kwani hapo utakua umehifadhiwa tu wazee wa kazi watakuja kukuchukua.

3.Utahifadhiwa kwenye maeneo yasiyofahamika.

4.Ukipandiswa kwenye gari utafungwa pingu na utawekwa katikati, kulia kwako na kushoto atakaa mtu, tambua haupo salama.

KWA LEO TUISHIE HAPA.

Twaha Mwaipaya 05.5.2025

View: https://x.com/Twaha_Mwaipaya/status/1919363194079924526/photo/1
 
NAMNA YA KUJILINDA- HATUPO SALAMA.

View attachment 3325850

CCM wanasababisha nchi isiwe na furaha. Haya ni maisha ya aina Gani?
 
kweli watanzania tujilinde wenyewe kwani hawa polisi kiukweli hawana time na sisi walalahoi
Hao wasiojulikana hawakamati walalahoi wanakamata wanasiasa ama mabosi wa upinzani

Sisi walalahoi tunaishi kwa amani tu maana hatuna cha kuwafanya
 
kweli watanzania tujilinde wenyewe kwani hawa polisi kiukweli hawana time na sisi walalahoi
Mlinzi bora ni Mungu. Ingawaje nae anasema jisaidie nami nikusaidie. Sasa kujisaidia kuliko Bora ni kutokuichokoza Serikali. Huwezi kutekwa au kuumizwa kwa makusudi burebure tu lazima kuna jambo umefanya au kauli mbovu umetoa kwa mamlaka, ukiacha ajali ya AKWILINA na yule mwandishi wa habari kule Morogoro jina limenitoka kidogo.
AA, Nimekumbuka ni MWANGOSI
 
kama mamlaka yote hutoka kwa Mungu!

Je ni Mungu ndiye amewapa mamlaka ya kuwaumiza, kuwapoteza na kuwaua raia wao?
 
Fear should be feared; Tatizo tumetoka kwenye reli na tunaendelea kucheka na Kima mwisho wake tunavuna mabua..., Polisi, Ulinzi wa Jamii ni muhimu sana katika Jamii ya aina yoyote ile kwahio hakuna shortcut zaidi ya kurudisha imani ya Ulinzi wetu zaidi ya hapo ni kuzima moto kwa mafuta ya taa.....

Back
Top Bottom