Twaha Mwaipaya: Namna ya kujilinda, hatupo salama, chukua hatua hizi

kama mamlaka yote hutoka kwa Mungu!

Je ni Mungu ndiye amewapa mamlaka ya kuwaumiza, kuwapoteza na kuwaua raia wao?
mamaka ya u-Rais (nafasi hiyo) imewekwa na Mungu, ila mtu atakayekaa kwenye nafasi hiyo anaweza kuwekwa na mashetani.
 
Wakuu, wasiojulikana wakianza kuvunja mlango (kama ni usiku) hakikisha unazima umeme kwenye main switch ndani panakuwa giza kwenye giza kisu cha jikoni huwa kianishinda smg unawaambush.
 
Maisha ya kutekana na kuuana.
nimemwona mama Abduli anachekacheka tu, hajali ni watz wangapi wana majonzi mioyoni mwao. Hajali kina familia za kina Soka, Mbise, Kibao, Mdude, ... wengine amewafungia magerezani kwa kesi za kisiasa. mwanche aendelee kucheka-cheka. Mungu hadhihakiwi!!!!!
 

Ni ushauri mzuri kuzingatiwa

Lakini wote kabisa tunapaswa tutambue Wazi kabisa kwamba, katika nchi yenye Utawala Uliofitina na yenye Jamii za Watu walioparaganyika na kuhasimiana, Usalama wa kila Mtu mmoja mmoja huwa upo hatari muda wote kabisa. Hakuna Mtu ambaye yupo salama, hata ujiwekee Ulinzi mkali kiasi gani. Watu wabaya na Wadhalimu wakiamua kukupata lazima watakufikia tu hata kama utajificha pangoni!
Ogopa Sana kuishi kwenye jamii za Watu walioparaganyika, kuchukiana, kuhasimiana, Jamii za Watu waliokosa upendo, wasio na huruma, Watu wenye kubaguana, jamii za watu zilizojaa chuki kubwa na Visasi, n.k., n.k. Kwa bahati mbaya Sana, hapa Tanzania kwa sasa Watawala wa nchi hii tayari wametufikisha kwenye hatua hii ya kuwa na Jamii za watu wanaochukiana Sana kupita kiasi kutokana na misingi ya Itikadi za Siasa au Imani za Kidini.

Tanzania kwa Sasa kuna Mpasuko wa Wazi kabisa katika Jamii kutokana misingi ya Vyama vya Siasa na Itikadi za Dini. CCM wanawachukia Wapinzani wao wa kisiasa, hasa CHADEMA, Wanawatendea uovu na Udhalimu mbaya Sana Kama wanyamapori.

Aidha, kwa upande mwingine, Watu Wapenda Haki na Demokrasia wanapoamua kuukosoa Utawala uliopo kwa kutumia Hoja za nguvu zenye mashiko. Upande wa Wafuasi wa Mtawala aliyopo madarakani wanajitokeza kujibu kwa niaba ya Mtawala kwa kutumia Utetezi wa Dini ya Mtawala bila ya Kujibu Hoja za Msingi zilizoelekezwa kwa Mtawala mwenyewe!
Malumbano haya na Mpasuko huu naona kama mwisho wake hautakuwa mzuri kwa Usalama wa Watu katika nchi hii!
 
Kuna watu wana roho za ajabu hawajali hata Mungu, wao ni kuagiza watu wavunje milango nyumbani kwa akina Mdude, wapige, kuteka na kuua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…